Tafuta

2020.07.30 2016.07.30 Papa Francisko akitembea na vijana wakati wa siku ya vijana nchini Poland 2020.07.30 2016.07.30 Papa Francisko akitembea na vijana wakati wa siku ya vijana nchini Poland 

Francisko azidundua tena Mkataba wa Mfumo Mpya kuhusu Elimu Kimataifa

Tarehe 15 Oktoba utatangazwa ujumbe kwa njia ya video wa Papa huko Laterano,Roma, kifuatiwa na hotuba za watu wa Kanisa na wa kiutamaduni.Tukio litatangazwa moja na Vatican News na majaukwaa yake yote.

VATICAN NEWS

Papa Francisko anarudia kushughulikia suala la elimu, kitovu cha mafundisho yake na mazungumzo na ulimwengu. Atafanya hivyo siku ya Alhamisi tarehe 15 Oktoba 2020 saa8.30 mchana  na ujumbe wake kwa njia ya  video, ambapo utakuwa ni muhtasari wote wa kile kilichopendekezwa juu ya mada hii wakati wa upapa wake na programu yake  ya utume kwa sababu, kama vile Papa  alivyorudia rudia mara nyingi kusema kuwa “ kuelimisha ni tendo la tumaini”.

Mwisho wa Ujumbe kwa njia ya video, Papa Francisko atapendekeza kwa watu wote wenye mapenzi mema kushikamano na Mkataba huo wa Elimu kimataifa, mkataba ambao unaleta pamoja  mabadiliko kwa kiwango cha sayari, ili elimu iwe muundaji wa undugu, amani na haki. Ndiyo haja ya haraka zaidi katika wakati huu uliowekwa na janga zito.

Ujumbe wa video wa Papa utatangazwa wakati wa tukio litakalo kuwa linaendelea katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Laterano, mjini Roma  lililoandaliwa na na Baraza la Kipapa la Elimu ya Katoliki, kwa kujikita hasa katika ulimwengu wa masomo, ambao pia unaweza kufuatiliwa moja kwa moja mtandaoni , pia kupitia jukwaa la Vatican na Youtube( www. vaticannews.va) (utiririshaji mkutano huo utakuwa na tafsiri ya moja kwa moja kwa lugha ya Kiingereza, Kifaransa, kihispania na Kireno).

08 October 2020, 15:25