Tafuta

Kardinali Fridolin Ambongo Besungu, Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Kinshasa DRC ameteuliwa kuwa ni kati ya Wajumbe wa Baraza la Makardinali Washauri. Kardinali Fridolin Ambongo Besungu, Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Kinshasa DRC ameteuliwa kuwa ni kati ya Wajumbe wa Baraza la Makardinali Washauri. 

Baraza la Makardinali Washauri: Kardinali Fridolin Besungu, DRC.

Baraza la Makardinali Washauri linamsaidia Baba Mtakatifu kutekeleza majukumu yake ya kuliongoza Kanisa la Kiulimwengu kwa njia ya ushauri mwanana. Kwa wakati huu, kazi kubwa mbele yao ni muswada wa Katiba Mpya ya Kitume: “Predicate evangelium” yaani “Hubirini Injili” ambayo baada ya kukamilika, itachukua nafasi ya Katiba ya Kitume “Pastor Bonus” yaani “Mchungaji mwema”

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko ameridhia wajumbe wa Baraza la Makardinali Washauri pamoja na kumteua Kardinali Fridolin Ambongo Besungu, Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Kinshasa, DRC., kuwa ni mjumbe wa Baraza la Makardinali Washauri. Makardinali wanaoendelea kuwa washauri ni pamoja na: Kardinali Óscar A. Rodríguez Maradiaga, S.D.B., Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Tegucigalpa, Honduras, Kardinali Reinhard Marx, Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Munich na Freising, Ujerumani. Wengine ni Kardinali Sean Patrick O’Malley, O.F.M. Cap., Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Boston, Marekani pamoja na Kardinali Oswald Gracias, Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Bombay, India. Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican, Kardinali Giuseppe Bertello, Gavana wa Mji wa Vatican, pamoja na Askofu Marcello Semeraro, Katibu mkuu wa Baraza la Makardinali Washauri.

Mwingine ni Askofu Marco Mellino Katibu Mwambata. Baraza la Makardinali Washauri linamsaidia Baba Mtakatifu kutekeleza majukumu yake ya kuliongoza Kanisa la Kiulimwengu kwa njia ya ushauri mwanana. Kwa wakati huu, kazi kubwa mbele yao ni muswada wa Katiba Mpya ya Kitume: “Predicate evangelium” yaani “Hubirini Injili” ambayo baada ya kukamilika, itachukua nafasi ya Katiba ya Kitume “Pastor Bonus” yaani “Mchungaji mwema” inayojihusisha zaidi na masuala ya uongozi wa Sekretarieti kuu ya Vatican.

Makardinali Washauri
16 October 2020, 15:38