Tafuta

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu Marcello Semeraro kuwa Mwenyekiti mpya wa Baraza la Kipapa la Kuwatangaza wenyeheri na watakatifu. Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu Marcello Semeraro kuwa Mwenyekiti mpya wa Baraza la Kipapa la Kuwatangaza wenyeheri na watakatifu. 

Askofu M. Semeraro: Mwenyekiti Baraza la Kutangaza Watakatifu

Askofu Marcello Semeraro, mwenye umri wa miaka 72 alizaliwa tarehe 22 Desemba 1947 huko Lecce, Kusini mwa Italia. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 8 Septemba 1971 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Kunako mwaka 1998 akateuliwa na Mtakatifu Yohane Paulo II kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Oria na kuwekwa wakfu tarehe 29 Septemba 1998.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu Marcello Semeraro, Askofu wa Jimbo Katoliki la Albano na ambaye ni Katibu mkuu wa Baraza la Makardinali Washauri, kuwa Mwenyekiti mpya wa Baraza la Kipapa la Kuwatangaza waamini kuwa wenyeheri na watakatifu, ili kuziba pengo lililoachwa wazi na Kardinali Giovanni Angelo Becciu aliyeng’atuka madarakani tarehe 24 Septemba 2020. Askofu Marcello Semeraro, mwenye umri wa miaka 72 alizaliwa tarehe 22 Desemba 1947 huko Lecce, Kusini mwa Italia.

Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 8 Septemba 1971 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Kunako mwaka 1998 akateuliwa na Mtakatifu Yohane Paulo II kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Oria na kuwekwa wakfu tarehe 29 Septemba 1998. Kuanzia mwaka 2004 hadi mwaka 2020 amekuwa ni Askofu wa Jimbo Katoliki la Albano. Na kunako mwaka 2013 akateuliwa na Baba Mtakatifu Francisko kuwa Katibu mkuu wa Baraza la Makardinali Washauri.

Papa: Uteuzi

 

16 October 2020, 15:58