Tafuta

Hakuna lolote linaweza kuwa mbadala wa familia au kulinganishwa na jukumu lake. Hakuna lolote linaweza kuwa mbadala wa familia au kulinganishwa na jukumu lake. 

Ask.Paglia:Ndani ya familia ni mahali penye msimamo hata katika tukio la janga!

Mwenyekiti wa Taasisi ya Kipapa ya Elimu kwa ajili ya Maisha ametoa hotuba yake kuhusu mada ya familia katika kipindi cha janga la corona na baada ya janga kwa wawakilishi wa kichungaji wa familia katika jimbo la Colombia.Ni ndani ya familia pamoja na udhaifu wake wote kuwa mahali pa kimbilio na msimamo thabiti.

Na Sr. Angela Rwezauala - Vatican

Familia, licha ya kupata mashambulizi mengi, inabaki kuwa imara, kwa sababu ya nguvu yake ya kina  ya ndani. Hakuna lolote linaweza kuwa mbadala wa familia au kulinganishwa na wajibu wake kama familia. Amethibitisha hayo Askofu Vincenzo Paglia, Mwenyekiti wa Taasisi  ya Kipapa ya Elimu ya Maisha, akizungumza na wawakilishi wa kichungaji wa familia wa Jimbo katoliki la Colombia, katika mchakato wa mkutano wao kwa njia ya mtandao uliofanyika tarehe 21 Oktoba 2020 kwa kuongozwa na mada “familia katika kipindi cha janga la corona na baada ya janga”. Mbele ya kukabiliwa na Covid-19 ni ndani ya  familia na udhaifu wake wote kwamba ni mahali pa kimbilio na msimamo thabiti. Kipindi cha virusi vya corona kimeonsha wazi kuwa familia ni mtindo wa pekee wa kijamii, amesisitiza Askofu Paglia.

Familia ni mahali pa uhusiano wa nguvu

Familia katika ulimwengu ambamo daima uchaguzi na mang’amuzi yanakuwa ni ya kushitukiza au ghafla lakini  bado inabaki kuwa mahali pa mahusiano ya nguvu ambayo yanaendana na kutegemea maisha ya kina kwa kila mjumbe ndani mwake. Aidha Askofu Paglia amebainisha kuwa hata Makanisa lazima yawe na sura ya muungano wa familia na ambayo ni muhimu katika shughuli nzima ya kutimiza ufalme wa Mungu  kwa namna mpya ya kuwa Kanisa, na  maana ya ya  Kanisa moja la  familia ya Mungu. Kwa maana hiyo  amekumbusha kwamba hata Papa Francisko katika Wosia wa Kitume wa Amoris Laetitia, yaani furaha ya upendo ndani ya familia, anaomba upyaisho wa kina katika Kanisa. Kwa upande wa famiglia, kinyume chake amewashauri  wahisi uwajibikaji  wa  kutangaza katika Ulimwengu Injili ya familia kama jibu la kina na mahitaji ya familia yaliyo andikiwa katika moyo wa kila  binadamu na katika kila jamii.

Inabidi kutengeneza jumuiya

Askofu Paglia akiendelea na hotuba yake hakusita kuonesha kwamba leo hii kuna pengo kubwa linalotenganisha familia kutoka jumuiya ya kikristo, familia ambazo kidogo siyo za kikanisa, kwa sababu, mara nyingi zimejifungia ndani mwake binafsi na vile vile, jumuiya za parokia ambazo kidogo hazina ufamilia kwa sababu mara nyingi wanafanya ukiritimba wa ajabu. Kwa maana hiyo hapo ndipo kuna haja ya kuwa na  maono mapya ambayo yaweze kuunda  kwa hakika msimamo wa parokia kama jumuiya  moja ambayo ni familia ya kweli.

Kuna haja ya kubuni uchungaji mpya "udugu katikati ya familia

Askofu Paglia anaamini kwa hakika kuwa kuna haja ya kubuni uchungaji ampya mbao ungeitwa udugu katikati ya familia hasa kwa kufikiria shughuli za kichungaji zinazofanywa kwa ajili ya familia na ambazo  zinaweza kweli kuendeshwa kwa mantiki ya kifamilia. Ni lazima kuhamasisha mantiki ya udugu kati ya familia, kwa ujumla ngazi zote amesisitiza na kuhusisha parokia zote na vyama mbali mbali vya kitume ndani ya parokia. Hii ina maana ya kuwa ndani ya maisha ya parokia, lakini pia ndani ya maisha ya uzalendo, ndani ya jamii mahali ambamo familia zinaitwa kutoa chango mkubwa kama  chachu ya kimafamilia katika jamii.

23 October 2020, 14:56