Tafuta

2020.04.22 Watu wa asilia wa Amazonia 2020.04.22 Watu wa asilia wa Amazonia 

Vatican-Ask.Mkuu Jurkovič: Kudumisha haki kwa ajili ya watu asilia!

Wito umetolewa na Askofu Mkuu Ivan Jurkovic,mwakilishi wa Kidumu wa Vatica katika Ofisi za Umoja wa Mataifa zilizoko Geneva,katika Kikao cha 45 za Baraza kwa ajili ya haki za binadamu katika muktadha wa watu asilia.Wasiwasi mkubwa ni kuhusu athari kubwa ambayo imetokana na janga lipo na linaendelea kuwakabili jamii hizi.

Na Sr. Angelo Rwezaula- Vatican News,

Askofu Mkuu Ivan Jurkovic mwakilishi wa kudumu wa Vatican katika ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Geneva Uswiss, ametoa rai ya kurejeshwa tena haki za kitaifa na kimataifa zilizo hatarini kupotea kutokana na Janga la ugonjwa wa Corona au covid-19.  Akichangia katika Mkutano wa Umoja wa Mataifa uliofanyika tarehe 24 Setemba 2020 katika kikao chake cha 45 cha Baraza la Ushauri la haki za binadamu, amekazia kuwepo kwa haki hasa haki za watu asilia. Askofu Mkuu Jurkovic amesema, ni haki za binadamu na uhuru ambazo kimsingi zinaendelea kupingwa na Mataifa yenye nguvu kwa kisingizio cha 'mwamvuli wa kutetea maelekezo ya kupambana na majanga asili' kutoka tawala za watu wanaotumia nguvu katika kufikia muafaka.

Askofu Mkuu Jurkovič  akiendelea aidha ameonesha wasiwasi wa Papa  Francisko juu ya janga la ugonjwa wa Corona au Covid-19 ambalo linaonesha kuwa asilimia sita (6%) ya watu wote ulimwenguni wameathirika, hasa wale wanaoishi katika mzingira ya umaskini uliopindukia janga hili limedhoofisha jitihada za utoaji huduma.  Kukosekana kwa huduma za kiafya ni viashiria vya kukosekana kwa usalama na uhuru wa kutoka sehemu moja kwenda nyingine.  Sehemu kubwa ya jamii wakiwemo wanawake wanaofanya kazi katika sehemu za usambazaji habari, viwandani, wakati wa Janga wamekumbwa na kuzungumkuti na hadi sasa hawajui adhama ya kazi zao.  Mwakilishi wa kudumu wa  Vatican katika ofisi za Umoja wa Mataifa, Askofu Mkuu, Jurkovič amewataka wafanyakazi wapatao asilimia 80 wa mazingira duniani kuchangia katika kutoa njia zinazoweza kukuza ushiriki katika kuyalinda mazingira.

Ulimwengu siyo biashara bali ni zawadi kutoka kwa Mungu, ni sehemu takatifu ya kushirikishana vipaji na kulindana alikazia Askofu Mkuu Jurkovič. Na zaidi amezidi kuwatetea wakazi kutoka katika uharibifu wa kiuchumi unaosongwa kwa mashinikizo makali ya kisheria za kitaifa na kimataifa yanayopelekea kuwepo kwa hujuma za kiutendaji katika kutumia lasirimali za nchi. Mashinikizo hayo yanapelekea kukua na kuongezeka kwa uvunjifu wa haki za utu na kuweka vizuizi katika upatikanaji wa haki.

Askofu Mkuu Ivan Jurkovič  amewakumbusha pia wanajumuiya asilia kuwa wasijisikie wao ni wachache bali wajishughulishe katika harakati zote za uamuzi wa kisiasa, hasa zile zinazoendana na maadili ya Kanisa. Bila kuzisahau familia zilizoathirika vibaya na janga la Corona ambazo zinasongwa na mtindo mpya wa maisha. Matumaini ya Kanisa ni kutengeneza miundo mipya ya namna za kuishi  na sera mpya za  kisiasa za kimataifa, kitaifa na kimahalia zikiwashirikisha wakazi na kuheshimu utambulisho na mila katika kufikia maendeleo ya kweli na fungamani.

26 September 2020, 16:46