Tafuta

Vatican News
Katika miezi ya mwisho kizazi kizima cha wazee kimelipa sana gharama ya matokeo ya janga la corona, kwa maana hiyo ni lazima kulinda tunu hii yenye thamani. Katika miezi ya mwisho kizazi kizima cha wazee kimelipa sana gharama ya matokeo ya janga la corona, kwa maana hiyo ni lazima kulinda tunu hii yenye thamani.  

Vatican:Ask.Mkuu-Jurkovič asema kuna haja ya kutetea haki za wazee na ikawa ndiyo dira!

Wazee ni kizazi chenye thamani na rasilimali muhimu ambayo lakini imeharibiwa na hali ngumu na hatari.Ni lazima kulinda haki za wazee hao na kuzifanya kuwa ndiyo dira.Ni wito wa Askofu mkuu Ivan Jurkovič,Mwakilishi wa kudumu wa Vatican kwenye Ofisi za Umoja wa Mataifa zilizoko mjini Geneva Uswiss,wakati wa kutoa hotuba yake tarehe 21 Septemba 2020.

Na Sr. Angela Rwezaula-Vatican

Katika Askofu mkuu Ivan Jurkovič, Mwakilishi wa kudumu wa Vatican kwenye Ofisi za Umoja wa Mataifa zilizoko mjini Geneva, akihutubia kwenye mkutano wa 45 wa Baraza kwa ajili ya haki na amani amesema ni vema kutetea haki za wazee hata katika kipindi cha Janga. Akihutunia Askofu Mkuu  Jumatatu, tarehe 21 Septemba 2020, jijini Geneva Uswiss, amesema Kizazi msingi na rasimali ambayo imekumbwa na jaribio gumu sana kiko hatarini. Kwa maana hiyo inahitajika kulinda kwa dhati haki zote za wazee na kuzifanya kuwa kama dira. Haki za binadamu hazina umri kwa njia hiyo afya ya watu wazee lazima ilindwe kama ilivyo haki za wote hasa katika kipindi cha janga la Covid-19.

Askofu Ivan Jurkovič, katika hotuba yake kwenye kikao cha 45 cha Baraza la Haki za kibinadamu na ambacho kimejikita juu ya  uhusiano wa ripoti ya mtaalam juu ya kufurahia haki za binadamu kwa upande wa wazee. Awali ya yote Askofu Mkuu Jurkovič ameweza kuangazia hitaji la kuwa na takwimu fulani na kamili juu ya ukweli wa wazee. Takwimu, kiukweli, hazijakamilika na ni za kawaida na huwa zinawaonyesha kama kundi moja, wakati ukweli ni tofauti sana amesema.

Mtazamo huo wenye vizuizi hairuhusu tathmini sahihi ya mahitaji yao, wala uthamini wa kutosha wa mchango muhimu wanaotoa kwa jamii. Kwa njia hiyo wito wa Askofu Mkuu ni juu ya hitaji la data halisi za haraka, na kwa wakati unaofaa na za kuaminika, ili mapungufu katika ulinzi wa haki za binadamu katika nyanja hii ya idadi ya watu yatambuliwe na kujazwa. Takwimu hizo ni muhimu sana amesisitiza Askofu Mkuu kwa sababu, kama janga lilivyoonyesha, zinawakilisha chombo muhimu kwa ufuatiliaji wa dharura ya kiafya ambayo inaweza kutoa majibu maalum.

Kwa mujibu wa mawazo ya Askofu Mkuu pia ni masikitiko ya michango ambayo Covid-19 imetakiwa kutoka kwa wazee waliolazwa katika nyumba za uuguzi na vituo vya makazi ulimwenguni kote. Kwa kuzingatia hali hii mbaya Askofu mkuu amesisitiza kuwa inahitajika kuripoti kwa usahihi juu ya maambukizi ya ugonjwa wa mapafu wa Virusi vya Corona na vifo vinavyotokea katika hali hii, ili kuboresha ufuatiliaji wa ndani ya vituo hivyo. Kuhusu upatikanaji wa huduma za matibabu, mwakilishi wa Vatican aidha ameonesha wasiwasi juu ya ukweli kwamba maamuzi juu ya ugawaji wa rasilimali za matibabu, pamoja na vifaa vya kupumua, inawezekanaa au tayari imefanywa tu kwa misingi ya umri wa wagonjwa. Kwa maana hiyo, ni muhimu sana kwamba itifaki za afya zinaongozwa na tathmini ya kina ya kliniki na kuwepo uwazi wa kulinda haki na utu wa kila mtu.

Katika miezi ya hivi karibuni, ameongeza kusema Askofu Mkuu Jurkovič, kwamba kizazi kizima cha wazee kimelipa sana gharama ya matokeo ya janga la corona, licha ya kizazi hiki kuwa chenye rasilimali ya thamani kubwa kwa familia ya wanadamu, kwa historia, uzoefu na ufundishaji wenye wenye maana. “Mizizi na kumbukumbu ya watu, wazee lazima walindwe; haki na utu wao lazima vilindwe, amesisitiza Askofu Mkuu. Lakini ili kufikia lengo zuri na la lazima, takwimu kamili, za kuaminika na za maana zinahitajika, ili kuondoa vizuizi vilivyopo na kutathmini ufanisi wa hatua zilizopo tayari.

21 September 2020, 17:12