Tafuta

Kardinali Tagle Kardinali Tagle 

Ufilippino:Kard.Tagle-Mazungumzo ni chombo cha kushinda janga!

Katika hotuba yake kwenye Warsha ya Walimu katoliki nchini Ufilippino,Kardinali Tagle,Rais wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa watu na Caritas Internationalis amesisitizia juu mazungumzo kuwa ni chombo pekee cha kuwezesha kushinda janga la sasa la covi-19.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Njia pekee ya kuweza kuondokana tukiwa wenye nguvu zaidi na janga hili baya la virusi vya corona ni ile ya mazungumzo. Ndiyo ilikuwa kiini cha hotuba ya Kardinali Antonio Luis Tagle, Rais wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa watu na Caritas Internationalis, katika Warsha ya Walimu katoliki nchini Ufilippino, iliyohitimishwa tarehe 25 Septemba 2020.

Tukio hili liliandaliwa na Chama Katoliki cha Elimi nchini Ufilippino  (Ceap), kiungo ambacho kinaunganisha mashule 1,500 katoliki, nchini humo. Kutokana na janga la virusi vya corona, warasha huu imfanyika kwa njia ya mitanao ya moja kwa moja kupitia tovuti na facebook. Mada iliyoongoza warsha hii ilikuwa ni “ utume: mazungumzo ya imani, maisha na utumaduni zaidi ya kukiri,mipaka na zaidi ya covid”.

Akiendelea na hotuba yake Kardinali Tagle amesema “Mazungumzo endelevu katikati ya shida ya kiafya ni muhimu kwa sababu janga linahitaji  kunfaya zaidi ya 'janga' sawa na hili ambalo ni, mwitikio wa ulimwengu". Bila utamaduni wa mazungumzo, Kardinali amebainisha, dharura itazidi kuwa mbaya na sio tu kwa suala la kuambukiza, lakini pia kwa sababu ubinadamu mbaya zaidi unaibuka, badala ya kuwa na ubora uliomo ndani ya kila mmoja na ubora ambao lazima ugawanywe kwa wote.

Kardinali aidha amewambia watu wasifanye mchezo na janga kati ya makundi na sekta za kijamii badala yake wakimbilie katika ushirikishwaji wa mawazo, kwa sababu kukabiliana kwa ujenzi tayari ni hatua madhubuti kuelekea kupata jibu la ulimwengu. Kardinali Tagle baadaye akasimulia uzoefu wake wa kibinafsi, hasa baada ya kupata matokeo mazuri, katikati ya Septemba ya Covid-19, Kardinali huyo alipitia kipindi cha kujitenga, ikifuatiwa na kupona kabisa. "Katika kujitenga, niligundua kuwa kuishi kweli hali ya kina ya uhusiano wa ndani na Mungu inahitajika ambayo inatusaidia kugundua tena kuwa hatuko peke yetu”. Kwa sababu hii, aliongeza, mazungumzo ni muhimu sana. Hatimaye ametoa shukrani kwa watu wote waliomwombea  afya yake.

26 September 2020, 16:35