Tafuta

Vatican News
2020.09.11 Askofu Rudolf Nyandoro 2020.09.11 Askofu Rudolf Nyandoro 

Papa Francisko amemteua Askofu wa jimbo la Gweru,Zimbabwe

Askofu Rudolf Nyandoro,aliyekuwa Askofu wa Gokwe ameteuliwa na Papa kuwa Askofu wa jimbo la Gweru,nchini Zimbabwe.

VATICAN NEWS

Baba Mtakatifu amemteua Askofu Rudolf Nyandoro, kuwa Askofu mpya wa Gweru,nchini  Zimbabwe hadi uteuzi huo alikuwa askofu wa Gogwe. Askofu Nyandoro alizaliwa Gweru  kunako mwa  1968 na akapewa daraja la upadre  mwaka 1998. Majiundo yake ya ujandokasisi ni katika mafunzo ya falsafa tangu 1991 hadi 1994 katika seminari kuu ya Mtakatifu Charles Lwanga huko Chimanimani, Mutare na kumaliza masomo yake ya kitaalimungu huko Chishawasha, Harare nchini Zimbabwe.

Mwaka  2015 alipata shahada ya udaktari (PhD) katika ushauri wa kichungaji katika Chuo Kikuu cha Afrika Kusini. Katika harakati za maisha yake ya huduma ya kichungaji ameshikilia nafasi mbali mbali za majukumu yafuatayo ya kichungaji katika jimbo la Masvingo: makamu katika utume wa Mukaru (1999), msimamizi wa Kanisa Kuu (2000-2006), na msimamizi wa seminari ndogo (2007-2009) na ya Chuo cha Ualimu cha Bondolfi (2010-2015). Mnamo mwaka 2015 amekuwa kama kansela wa jimbo la Masvingo na profesa katika Chuo cha Ualimu cha Bondolfi. Baada ya kung’atuka kwa Askofu Angel Floro Martínez, I.E.M.E., kama Askofu wa Gokwe mnamo 2017 akachaguliwa yeye.

11 September 2020, 18:41