Tafuta

Vatican News
VATICAN:PAPA AMEKUTANA RAIS WA POLAND Andrzej Duda VATICAN:PAPA AMEKUTANA RAIS WA POLAND Andrzej Duda 

Papa Francisko amekutana na Rais wa Poland,Andrzej Duda!

Tarehe 25 Septemba 2020,Papa Francisko amekutana na Rais wa Jamhuri ya Poland Bwana Andrzej Duda,ambaye mara baada ya Mkutano huo amekutana na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican akiambatana na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher,Katibu wa Vatican kwa ajili ya Mahusianao na ushirikiano na na nchi za nje.

Salam zao zimejikita kwenye muktadha wa Miaka 100 tangu kuzaliwa kwa Mtakatifu Yohane Paulo II na katika Mwaka wa 40 tangu kuanzishwa kwa mfuko wa Meya wa kujitegemea “Solidarność”. Katika mazungumzo yao  viongozi hawa yamekuwa na mada zinazohusiana na utume wa Kanisa, miongoni mwake ni uhamasishaji wa familia na elimu ya vijana. Na hatimaye wamezungumzia juu ya mantiki zinazohusiana na kimataifa ambazo kama vile dharura ya kiafya inayo endelea hadi sasa  na katika kutazama masuala ya kanda nzima na usalama.

25 September 2020, 15:24