Tafuta

Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko, tarehe 5 Septemba amekutana na kuzungumza kwa faragha na viongozi wakuu wa Jamhuri ya Watu wa San Marino. Baba Mtakatifu Francisko, tarehe 5 Septemba amekutana na kuzungumza kwa faragha na viongozi wakuu wa Jamhuri ya Watu wa San Marino.  (ANSA)

Papa Francisko akutana na Viongozi Wakuu wa San Marino

Papa na viongozi wakuu wa San Marino katika mazungumzo yao, wamechambua zaidi mchango wa Kanisa kwa ajili ya ustawi, maendeleo na mafao ya watu wa Mungu nchini San Marino. Kwa namna ya pekee, wamegusia matatizo, changamoto na fursa zinazoendelea kuibuka kutokana na janga la homa kali ya mapafu inayosababishwa na Virusi vya Corona, COVID-19 nchini San Marino.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, Jumamosi tarehe 5 Septemba 2020 amekutana na kuzungumza na viongozi wakuu wa Jamhuri ya Watu wa San Marino Bwana Alessandro Mancini na Mama Grazia Zafferani pamoja na ujumbe wao. Viongozi hawa baadaye wamekutana pia na kuzungumza na Askofu mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu mkuu wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa mjini Vatican. Baba Mtakatifu pamoja na wageni wake, wamezungumzia kuhusu mahusiano na ushirikiano wa kidiplomasia baina ya nchi hizi mbili.

Katika mazungumzo yao, wamechambua zaidi mchango wa Kanisa kwa ajili ya ustawi, maendeleo na mafao ya watu wa Mungu nchini San Marino. Kwa namna ya pekee, wamegusia matatizo, changamoto na fursa zinazoendelea kuibuka kutokana na janga la homa kali ya mapafu inayosababishwa na Virusi vya Corona, COVID-19 nchini San Marino. Baadaye, viongozi hawa wamejielekeza zaidi katika masuala ya Kimataifa kwa kuangalia masuala ya kidiplomasia katika mafao mapana zaidi kwa Jumuiya ya Kimataifa.

San Marino

 

07 September 2020, 15:03