Tafuta

Kardinali Parolin Katibu wa Vatican Kardinali Parolin Katibu wa Vatican  

Miaka 75 ya UN-Kard.Parolin:Ni kufanya kazi pamoja ili kushinda mateso ya ulimwengu!

Katika hotuba ya Katibu wa Vatican kwa njia ya video katika fursa ya kumbukizi la tangu kuanzishwa kwa UN amehimiza kufanya kazi pamoja ili kushinda mateso yanayotikisa dunia.Ugumu wa kazi ya kutafuta ustawi wa pamoja uwe msukumo kwa wajumbe wa Umoja wa Mataifa ambapo hata mara baada ya miaka 75 ya historia yake,jitihada kwa ajili ya haki, usawa na amani bado ni ndoto ya matumaini ya watu.

Na Sr.Angela Rwezaula – Vatican

Katika kilele cha kumbukizi  ya miaka 75 wa Umoja wa Mataifa UN, tarehe 21 Septemba 2020, Kardinali Pietro Parolin ametoa ujumbe wake kwa njia ya video akionesha shukrani ya kushiriki mkutano huo wa kiwango cha juu ili kuadhimisha miaka 75 ya Umoja wa Mataifa na kupyaisha uungwaji mkono na Vatican kwa Taasisi hii ya kifahari. Kardinali amesema kwa miaka 75 iliyopita, watu wa ulimwengu wameona Umoja wa Mataifa kama chanzo cha matumaini ya amani na maelewano ulimwenguni kati ya Mataifa. Kwa Shirika hili wameleta shauku ya kumaliza migogoro na ugomvi, heshima zaidi kwa hadhi ya mwanadamu, kupunguza mateso na umaskini na kuendeleza haki ambacho ni kielelezo cha matarajio msingi ya Umoja wa Mataifa kwamba hili Shirika halitathibitisha tu maadili ambayo yamejengwa juu yake, lakini pia litafanya kazi na azimio kubwa zaidi la kufanya maoni haya kuwa ya kweli katika maisha ya kila mwanamke na mwanamume.

Kardinali Parolin akiendelea na hotuba yake amesema tangu kutambuliwa kwake kama mwakilishi wa Taifa mnamo 1964, Vatican imeunga mkono na kuchukua jukumu kubwa ndani ya Umoja wa Mataifa. Mapapa waliofuatana wametambua mbele ya Mkutano Mkuu huu wakisisitiza Taasisi hii adhimu kuwa  ni‘kituo cha maadili’ ambapo kila nchi iko nyumbani, kwamba  familia ya mataifa inakusanyika na ambapo jamuiya ya kimataifa katika roho ya udugu na mshikamano wa wanadamu  inaonesha maendeleo pamoja na suluhisho za kimataifa kwa changamoto za ulimwengu. Kama ilivyo kwa janga la COVID-19 ambalo limeweka wazi kabisa, Kardinali amesesma “hatuwezi kuendelea kufikiria tu juu yetu wenyewe au kukuza migawanyiko; badala yake, lazima tushirikiane kushinda mapigo mabaya zaidi ulimwenguni, tukikumbuka kwamba mzigo uliobebwa na wengine huathiri ubinadamu na familia nzima ya Mataifa”.

Kwa zaidi ya miaka 75, Umoja wa Mataifa (UN) umelinda na kutumikia sheria za kimataifa, huku ukihamasisha ulimwengu kwa kuzingatia sheria na haki badala ya silaha na kutumia nguvu. Umoja wa Mataifa (UN) umeleta chakula kwa wenye njaa, umejenga nyumba kwa wale wasio nazo na, umejitolea kulinda nyumba yetu ya pamoja  na umeendeleza ulimwengu wa maendeleo muhimu kwa binadamu. Kardinali Parolin aidha amesema “Umoja wa Mataifa umejitahidi kutetea haki za binadamu za ulimwengu, ambazo pia zinajumuisha haki ya kuishi na uhuru wa dini, kwani ni muhimu kwa utangazaji unaohitajika wa ulimwengu ambapo hadhi ya kila mwanadamu inalindwa na imeendelezwa. Shirika limejitahidi kumaliza vita na mizozo, kurekebisha kile ghasia na ugomvi  na kuleta pande zinazopingana kwenye meza moja ili kwa pamoja, diplomasia na mazungumzo yaweze kushinda siku hiyo”.

Kumekuwa na changamoto na kurudi nyuma, hata kupingana na kushindwa, amebainisha Kardinali Parolini. Umoja wa Mataifa siyo mkamilifu na hauishi kila wakati kulingana na jina na maadili yake, na umejiumiza wakati wowote wa masilahi fulani yaliyoshinda faida ya wote. Umoja wa Mataifa daima utahitaji kuhuisha roho ya asili ili kufanya kanuni na madhumuni ya Mkataba iwe yake mwenyewe, katika muktadha wa ulimwengu unaobadilika. Kuna haja pia ya wanadiplomasia hapa na kwa nchi wanazowakilisha kujitoa tena kwa kazi ngumu ya kutafuta faida na ustawi wa wote kwa nia njema kupitia makubaliano ya kweli na maelewano” amesisitiza Kardinali Parolin. “Shirika la Umoja wa Mataifa, ambapo watu wa ulimwengu huungana katika mazungumzo na hatua za matedno ya pamoja  linahitajika leo hii kuliko  wakati wowote kujibu matumaini ambayo hayajapotea ya watu ulimwenguni”, amehitimisha Katibu wa Vatican.

22 September 2020, 14:58