Tafuta

Papa Francisko ameridhia ombi la kujiuzulu madarakani lililowasilishwa kwake na Kardinali Giovanni Angelo Becciu, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Kuwatangaza Waamini kuwa wenyeheri na watakatifu. Papa Francisko ameridhia ombi la kujiuzulu madarakani lililowasilishwa kwake na Kardinali Giovanni Angelo Becciu, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Kuwatangaza Waamini kuwa wenyeheri na watakatifu. 

Kardinali Becciu Ajiuzulu; Aondolewa Haki Za Ukardinali!

Papa Francisko ameridhia ombi la kujiuzulu kutoka madarakani lililowasilishwa kwake na Kardinali Giovanni Angelo Becciu, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la kuwatangaza waamini kuwa Wenyeheri na Watakatifu pamoja na kumwondolea haki zote alizokuwa nazo kama Kardinali. Hiyo ni taarifa iliyotolewa mjini Vatican. Kardinali Giovanni Angelo Becciu, alizaliwa tarehe 2 Juni 1948.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko Alhamisi tarehe 24 Septemba 2020 ameridhia ombi la kujiuzulu kutoka madarakani lililowasilishwa kwake na Kardinali Giovanni Angelo Becciu, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la kuwatangaza waamini kuwa Wenyeheri na Watakatifu pamoja na kumwondolea haki zote alizokuwa nazo kama Kardinali. Hiyo ni taarifa iliyotolewa mjini Vatican. Itakumbukwa kwamba, Kardinali Giovanni Angelo Becciu, alizaliwa tarehe 2 Juni 1948 huko Pattada, Sassari, mkoa wa Sardegna, Kusini mwa Italia.

Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, kunako tarehe 27 Agosti 1972 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Kunako tarehe 15 Oktoba 2001, Mtakatifu Yohane Paulo II akamteuwa kuwa Askofu mkuu na hatimaye kuwekwa wakfu hapo tarehe 1 Desemba 2001 katika Ibada ya Misa Takatifu iliyoongozwa na Kardinali Angelo Sodano. Tarehe 28 Juni 2018, Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa kuwa Kardinali. Katika maisha na utume wake, amewahi kuwa Balozi wa Vatican nchini Angola, Sao Tome na Principe; Cuba na Katibu mkuu msaidizi mjini Vatican. Tangu mwaka 2018 hadi tarehe 24 Septemba 2020 amekuwa ni Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la kuwatangaza waamini kuwa Wenyeheri na Watakatifu.

Kardinali Becciu
25 September 2020, 07:21