Tafuta

2019.11.16 Kardinali Michael Czerny 2019.11.16 Kardinali Michael Czerny 

Kard.Czerny:Waliohamishiwa ndani wanaweza kuwa nguvu chanya ya mabadiliko!

Kardinali Michael Czerny SJ katika fursa ya mkutano kuhusu Siku ya wahamiaaji na Wakimbizi ulimwenguni inayoatarajiwa kufanyika tarehe 27 Septemba 2020 kwa kuongozwa na kauli mbiu“Kama Yesu Kristo alivyolazimika kukimbia”,amebainisha kuwa waliohamishiwa ndani wanaweza kuwa nguvu chanya ya mabadiliko.

Na Sr. Angela Rwezaula-Vatican.

Ushauri wa nguvu uliotolewa na viongozi wa Kanisa kwa sababu washirikiane katika kujibu changamoto za watu waliorundikana kwa ndani na ndiyo ilikuwa ni kiini cha hotuba ya Kardinali Michael Czerny, Jumatano tarehe 23 Septemba 2020 katika tukio lilioandaliwa na Huduma ya Waijesuit kwa Wahamiaji(JRS), Umoja wa kimataifa wa mama wakuu wa mashirika (UISG) na ushirikiano wa kitengo cha wahamiaji na wakimbizi cha Baraza la Kipapa la Huduma ya maendeleo ya binadamu. Kwa mujibu wa Kardinali amesema ukaribu wao unaweza kuhamasisha usikivu zaidi na makini kwa kile ambacho watu waliolundikana kwa ndani wanahitaji, wanatarajia na inawezekana kuwapa chachu ya ushiriki wa watu waliohamishwa ndani kwa kila mmoja na uwezo wa kufanya maamuzi ambayo yanawatazama, katika lugha mafunzo yanayowezekana.

Siku wahamiaji na wakimbizi  ulimwenguni inafafanua kwa uwazi

Siku ya Wahamiaji na Wakimbizi Ulimwenguni, ambayo kwa kawaida imewekwa wiki ya mwisho ya mwezi Septemba, ilianzishwa ili kukuza uelewa wa maisha na hatima ya watu walio katika mazingira magumu kwenye safari, kuwaombea wanapokabiliwa na changamoto kubwa, na kuonyesha fursa ambazo uhamiaji unaweza kutoa. Watu waliohamishwa ndani  wanatupatia nafasi ya kugundua sehemu zilizofichika za ubinadamu na kukuza uelewa wetu wa ugumu wa ulimwengu huu, amesema Kardinali huyo. Ni kupitia wao ndiyo tunakutana na Bwana hata ikiwa macho yetu yanakuwa na ugumu wa  kumtambua amesisitiza.

Ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko

Kwa kuzingatia siku hiyo Papa Francisko amechapisha ujumbe uitwao “Kama Yesu Kristo alivyolazimika kukimbia” Kardinali Czerny anarudi kwenye maandishi haya elekezi huku akielezea kuwa, kwa sababu ya changamoto zinazosababishwa na janga linaloendelea, Papa ampanua wigo wa ujumbe wake ili kukumbatia si tu wakimbizi wa ndani, lakini pia wale wote ambao wanapata hali mbaya, kutelekezwa, kutengwa na kukataliwa kama matokeo ya Covid-19. 

Jozi sita za vitenzi vinahusiana na vitendo vya dhati

Katika ujumbe huo, Kardinali huyo amekumbuka kuwa Papa tayari mnamo 2018 alikuwa amemwalika kila mtu kujibu changamoto hii ya kichungaji na vitenzi vinne: kukarimu, kulinda, kuhamasisha na ujumuishe”. Kwa msingi huo, katika ujumbe wa mwaka huu, Papa Francisko ametaka kuongeza thamani yake na vitendo halisi vilivyo unganishwa na kila mmoja wa tendo hili mtu lazima ajue ili kuelewa; kuwa karibu ili kutumikia; ili kupatanishwa, lazima kusikiliue; ili kukua, ni lazima kushirikisha; lazima tuhusishwe kuhamasisha  na mwishowe lazima tushirikishane na   kujenga. Katika kila jozi ya vitendo vinavyohusiana na vitenzi, kardinali alisema, Papa Francis anawasilisha “mtazamo wa kimsingi au uwezo wa kufikia malengo muhimu kama vile upatanisho na ukuaji” na anaelezea hamu ya kuwa na ujasiri wa kuunda nafasi za kuruhusu aina mpya za ukarimu, undugu na mshikamano

Ushirikiano kati ya watendaji wa Kanisa

Akitoa msukumo kutoka kwa maneno ya Baba Mtakatifu Francisko na kutokana na uzoefu wa mtu aliyehama makazi, Kardinali Czerny ameshirikisha mambo mawili. Kwanza, amesisitiza umuhimu wa kushiriki malengo sawa kati ya watendaji wa Kanisa kuhusiana na kusaidia watu waliohamishwa ndani. Akitazama kuwa ulinzi wao ni jukumu la kimsingi la mamlaka za kitaifa, na kususitiza kwamba jibu la uhamisho wa ndani ni mfumo kwa ngazi ya mkakati ili kuinua suala hili kiulimwengu. Katika suala hili, amefafanua kuwa Kitengo cha wahamiaji na Wakimbizi cha Vatican kimeandaa miongozo ya kichungaji juu ya makazi yao ya ndani na msaada wa shirika la Wajesuit (JRS) na mashirika mengine,ambayo yanaweza kusaidia kazi ya kushirikiana. Kardinali pia amehimiza ushiriki wa Baraza lake (IDP) katika kupanga, kutoa ulinzi na majibu ya msaada kwao, na pia kuandaa sheria na sera zinazohusiana na makazi yao ya ndani.

Nguvu nzuri ya mabadiliko

Kardinali Czerny pia amesisitiza kuwa uamuzi, ustadi na uwezo ambao Baraza la Kipapa la maendeleo fungamani ya binadamu katika kitengo cha wahamiaji na wakimbizi IDP hujenga tena maisha yao inaweza kusaidia kuboresha jamii ambazo zinakuwa hali halisi mpya za maisha. Kwa kubainisha  kuwa wakimbizi wa ndani wanaweza kuwa nguvu nzuri ya mabadiliko, na kwamna kuunga mkono mwingiliano wao na jamii za wenyeji kutasaidia kukuza mshikamano wa kijamii, amani, usalama na maendeleo. Kwa kuwa karibu na ndugu na dada zetu waliohama ndani, tunaitwa kufunua uzuri na ustadi walionao, amebanisha. Kwa kumalizia, Kardinali amekumbusha ujumbe wa Papa ulioongozwa na Mt 25: 31 - 46 ambayo inatuhimiza kumtambua Mungu katika nyuso za wenye njaa, wenye kiu, wagonjwa, wageni na wafungwa.

24 September 2020, 15:09