Tafuta

Vatican News
2020.06.08 India, harakati za kusaidia walio wadhaifu katika kipindi cha virusi vya corona 2020.06.08 India, harakati za kusaidia walio wadhaifu katika kipindi cha virusi vya corona 

Hakuna aliyesahaulika katika sehemu yoyote!

Kitengo cha Wahamiaji na Wakimbizi cha Baraza la Kipapa la Maendeleo fungamani ya watu kila wiki wanatoa taarifa juu ya watu walio katika hatari na wenye udhaifu katika mzunguko wa kipindi cha Covid-19.Katika taarifa iliyotolewa tarehe 8 Septemba 2020 wanabainisha kuwa dharura ya virusi vya Corona imezidisha mizozo iliyokuwa ipo tayari,ambayo mizizi yake ni ukiukwaji endelevu wa haki za binadamu.

Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya binadamu katika kitengo chake cha wahamiaji na wakimbizi, wanatoa kila wiki juu taarifa zaidi zinazohusu watu walioathirika na wadhaifu kwa kipindi cha Covid-19. Katika taarifa iliyotolewa tarehe 8 Septemba 2020 wanabainisha kuwa dharura ya virusi vya Corona imezidisha mizozo iliyokuwa ipo tayari, ambayo mizizi yake ni ukiukwaji endelevu wa haki za binadamu. Wakati wa Katekesi ya Papa alisisitiza ukosefu wa usawa wa kijamii ambao umeangaziwa na kuchochewa na janga hilo. Wale walio hatarini zaidi wameona udhaifu wao ukiongezeka na idadi ya watu maskini ulimwenguni inazidi kukua. Kwa maana hiyo Papa  Francisko amekuwa akiwasihi Wakristo kushirikishana mali zao, wakizitumia kwa faida ya wengine pia na sio kwa ajili yao tu. Baba Mtakatifu ville vile ameona na kubaini  mara kwa mara kuwa tunaweza kuondokana kwenye shida hii tu lakini kwa  pamoja kama familia moja ya kibinadamu. Aidha  amekuwa akisisitiza kwamba Makanisa mahalia lakini pia mashirika Katoliki ya kimataifa yachukue njia hii kwa kuwasaidia wale wanaohitaji sana, bila ubaguzi au kutengwa kwa aina yoyote.

Kitengo cha wahamiaji na wakimbizi, cha Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo Fungamani  vile vile katika taarifa hii ya wiki wanasema, kwa ngazi ya Ulimwenguni, Manos Unidas, imetenga zaidi ya euro milioni 4.3 kwa ajili ya kupunguza athari za COVID-19 kati ya watu walio katika mazingira magumu zaidi  barani Asia, Afrika na Amerika Kusini. Kwa namna ya pekee Shirika lisilo la Kiserikali (NGO) liliunga mkono mipango ya  dharura 94 na kurekebisha mipango ya maendeleo177, ambayo ilikuwa imeanzisha hapo awali, ili kujumuisha huduma za kipekee za kushughulikia janga hilo.

Kitengo cha wahamiaji na wakimbizi,cha Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo Fungamani ya watu katika  taarifa hiyo wanabainisha kuwa nchini Brazil, Jimbo la  Grajaú, huko Maranhão, limefanya ishara thabiti ya kusaidia watu asilia  na walio hatarini zaidi kukabiliana na shida zinazosababishwa na janga hilo (PT). Kwa njia ya Video kumi zinaonyesha safari za watu wa kujitolea kusambaza karibu kilo 30,000 za chakula na vifaa vya usafi, zilizowekwa kwenye malori na magari na kuwakabidhi moja kwa moja binafsi. Askofu, Rubival Cabral Britto, amesema kuwa “Zawadi kuu tunayoweza kumpa mwingine ni kurudia matendo ya Yesu, ambaye aliona, na alikuwa na huruma na alimtunza mwingine. Mshikamano ndiyo suluhisho ambalo linatuweka huru kutoka gereza  kujilimbikiza  na ubinafsi. Mshikamano huu unatoa chachu ya ushirikiano kati ya Kanisa la Brazil, mashirika mbali mbali , serikali na mtandao wa parokia na jamuiya.

Nchini Kenya, Utume jamii Katoliki wa Mtakatifu Martin umezindua Mpango wa Jibu  katika  Dharura ili kusaidia jamuiya zilizo katika mazingira magumu wakati wa janga hilo, wanabainisha Kitengo cha Wahamiaji na Wakimbizi cha Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya watu. Ili kufikia mwisho huu, limeungana na Arche Kenya na Talitha Kum katika kutoa chakula na dawa muhimu kwa familia zilizo katika mazingira magumu, na wanasaidia vikundi vilivyo hatari na msaada wa kilimo kwa watu ambao wamepoteza mapato yao kwa sababu ya COVID. -19. Utume Jamii Katoliki wa Mtakatifu Martin kwa namna ya pekee anaangazia sana watu walio na ugonjwa wa akili, ulemavu na wale wa madawa ya kulevya kwa sababu COVID-19 inazidisha mateso yao. Miongoni mwa malengo ya mpango  huo ni kukuza uelewa kati ya jamuiya kwa mtazamo wa athari za janga hilo na kuelezea ni jinsi gani jamuiya inaweza kushughulikia shida ambazo zinaweza kutokea kama hiyo hiyo

Katika taarifa hiyo ya wiki ya watu walioathirika na wadhaifu kwa kipindi cha Covi – 19, Kitengo cha wahamiaji na wakimbizi, cha Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo  Fungamani ya watu wanasisitiza kuwa kwa upande wa nchi ya i Uingereza, hasa London, wasio na kazi na wasio na makazi wanakabiliwa na shida kubwa baada ya kuzuka kwa janga hilo. Kwa kujibu, JRS Uingereza inasambaza vifurushi vya chakula vya dharura kwa wasio na makazi, bila kujali hali ya kawaida ya uhamiaji. JRS yenyewe imesisitza juu ya  hitaji la kuhakikisha nyumba salama kwa watu wanaohitaji makazi ya dharura wakati wa janga hilo, tena bila kuzingatia hali yao ya uhamiaji. Kama Kadinali Vincent Nichols, Askofu Mkuu wa Westminster alivyosema: “Tunahitaji kujibu ubinadamu ulio hapa hapa, mbele yetu, kwa kutambua hadhi ya kuzaliwa ya kila mtu, na siyo kuwatupa tu ndani ya shimo”

Nchini India, jamuiya za Wakatoliki wa Jimbo kuu la Bombay wamefanya bidii yao ili kukidhi mahitaji ya watu maskini zaidi na walioathirika zaidi, ambao hali zao za kijamii na za kufanya kazi zimekuwa mbaya sana kutokana na janga hili. Kitengo cha wahamiaji na wakimbizi, cha Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo  Fungamani ya watu katika taarifa ya  wiki juu ya watu walioathirika na wadhaifu kwa kipindi cha Covi – 19,wanasisitiza kuwa miongoni mwa shughuli nyingi, ni mpango wa "Manna kwenye Magurudumu" unastahili kutajwa. Umepangwa  na waamini wa Kanisa la Mtakatifu Peter katika eneo la Bandra. Mpango huo umehakikisha kusambazwa kwa chakula zaidi ya 40,000, ili kusaidia kukidhi mahitaji ya chakula ya wahamiaji, wasio na makazi na wengine wanaohitaji. Parokia ya Mamajusi Mtakatifu wa Gorai-Culvem ni mfano mwingine wa kujitolea kwa hisani katikati ya shida, kufikia wakulima na wavuvi katika shida za kiuchumi. Kwa zaidi ya miezi mitatu. Karibu miezi mitatu Wakatoliki vijana  80, wanaume na wanawake, wamekuwa wakilinda eneo hilo, ili kuhakikisha mtandao mzuri wa mshikamano. Wanatoa chakula na vifaa kwa watu wa dini zote, wazawa, wahamiaji, wajane na wengine wanaohitaji, kwa ushirikiano wa serikali za mitaa na asasi za kiraia.

09 September 2020, 16:22