Tafuta

Vatican News
 Balozi Rahman Farhan Abdullah Al-Ameri wa Iraq tarehe 11 Septemba 2020 amewasilisha hati za utambulisho kwa Baba Mtakatifu Francisko mjini Vatican. Balozi Rahman Farhan Abdullah Al-Ameri wa Iraq tarehe 11 Septemba 2020 amewasilisha hati za utambulisho kwa Baba Mtakatifu Francisko mjini Vatican.  (Vatican Media)

Balozi wa Iraq Awasilisha Hati za Utambulisho kwa Papa Francisko

Balozi Rahman Farhan Abdullah AL-AMERI alizaliwa tarehe Mosi Januari 1962 huko Diyala, nchini Iraq. Kunako mwaka 1983 alitunukiwa shahada ya uzamivu kutoka Chuo Kikuu cha Baghdad. Tangu mwaka 1983 hadi mwaka 1986 alikuwa mwalimu wa kemia. Katika maisha yake, amewahi kuwa mfanyakazi wa wizara ya vijana na michezo; mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko hivi karibuni, amepokea hati za utambulisho kutoka kwa Bwana Rahman Farhan Abdullah AL-AMERI, Balozi mpya wa Iraq mjini Vatican. Balozi Rahman Farhan Abdullah AL-AMERI alizaliwa tarehe Mosi Januari 1962 huko Diyala, nchini Iraq. Kunako mwaka 1983 alitunukiwa shahada ya uzamivu kutoka Chuo Kikuu cha Baghdad. Tangu mwaka 1983 hadi mwaka 1986 alikuwa mwalimu wa kemia. Katika maisha yake, amewahi kuwa mfanyakazi wa wizara ya vijana na michezo; mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa. Mwanadiplomasia katika Ubalozi wa Oman.

Tangu mwaka 2010 hadi mwaka 2014 aliteuliwa kuwa Mkurugenzi Kitengo cha Ghuba ya Uajemi na Ukanda wa Mashariki ya Kati; Falme za Nchi za Kiarabu na Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Kati ya Mwaka 2014 hadi mwaka 2018 aliteuliwa kuwa mshauri mkuu kwenye Ubalozi wa Iraq nchini Uingereza. Alianza kama Mkurugenzi msaidizi na hatimaye akateuliwa kuwa Mkurugenzi mkuu anayeratibu mikutano ya kimataifa, Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, kati ya mwaka 2018 hadi mwaka 2020. Tarehe 11 Septemba 2020 akawasilisha hati zake za utambulisho kwa Baba Mtakatifu Francisko mjini Vatican kama Balozi mpya wa Iraq mjini Vatican.

Iraq
13 September 2020, 12:15