Tafuta

Vatican News
Balozi Patrick Renault kutoka Ubelgiji, tarehe 4 Septemba 2020 amewasilisha hati zake za utambulisho kwa Baba Mtakatifu Francisko mjini Vatican. Balozi Patrick Renault kutoka Ubelgiji, tarehe 4 Septemba 2020 amewasilisha hati zake za utambulisho kwa Baba Mtakatifu Francisko mjini Vatican.  (AFP or licensors)

Papa Apokea Hati za Utambulisho Kutoka kwa Balozi wa Ubelgiji

Balozi Patrick Renault alizaliwa tarehe 22 Septemba 1960 huko Rabat, nchini Morocco. Ameoa na amebahatika kupata mtoto mmoja. Ni mwanadiplomasia mwenye shahada ya uzamivu katika sheria kutoka Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Louvain. Tangu mwaka 1986 amewahi kufundisha masuala ya uhusiano wa kimataifa pamoja na kushika nyadhifa mbali mbali katika masuala ya kidiplomasia.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, Ijumaa tarehe 4 Septemba 2020 amepokea hati za utambulisho kutoka kwa Bwana Patrick Renault, Balozi mpya wa Ubelgiji mjini Vatican. Itakumbukwa kwamba, Balozi Patrick Renault alizaliwa tarehe 22 Septemba 1960 huko Rabat, nchini Morocco. Ameoa na amebahatika kupata mtoto mmoja. Ni mwanadiplomasia mwenye shahada ya uzamivu katika sheria kutoka Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Louvain  “Université Catholique de Louvain” kilichoko nchini Ubelgiji. Tangu mwaka 1986 amewahi kufundisha masuala ya uhusiano wa kimataifa; Katibu Ubalozi wa Ubelgiji nchini Pakistan, Msemaji msaidizi wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mshauri katika Ubalozi wa Ubelgiji nchini Italia na China.

Kati ya mwaka 1996 hadi mwaka 2002: Mshauri wa Ubalozi wa Ubelgiji nchini China, Mkurugenzi msaidizi, Ofisi ya Makamu Waziri Mkuu,  Ofisi ya Waziri wa Fedha na Mambo ya nchi za nje na baadaye akateuliwa kuwa Msahauri mkuu wa Ubalozi wa Ubelgiji nchini Australia. Kati ya mwaka 2002 hadi mwaka 2006 akateuliwa kuwa ni Balozi wa Ubelgiji nchini Pakistan na Afghanstan. Kati ya Mwaka 2006 hadi mwaka 2008 akateuliwa kuwa ni Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje. Kati ya mwaka 2008 hadi mwaka 2009 aliteuliwa kuwa Mshauri wa Kidiplomasia katika Ofisi ya Makamu Waziri Mkuu, Wizara ya Kazi na Haki Sawa. Kati ya mwaka 2009 hadi mwaka 2013 akateuliwa kuwa ni Balozi wa Ubelgiji, New Zealand pamoja na Visiwa vya Pasific.

Kati ya Mwaka 2013 hadi mwaka 2017 akateuliwa kuwa ni Balozi wa Ubelgiji nchini: Argentina, Uruguay pamoja na Paraguay. Kati ya Mwaka 2017 hadi mwaka 2018 akateuliwa kuwa ni Mkurugenzi mkuu wa Mawasiliano. Na hatimaye kati ya Mwaka 2018 hadi mwaka 2020 aliteuliwa kuwa ni Mkurugenzi wa huduma za kiuchumi duniani; diplomasia katika mitandao ya kijamii; mapambano dhidi ya uhalifu wa kupangwa, ufadhili kwa vitendo vya kigaidi, rushwa na ufisadi katika Wizara ya Mambo ya nchi za nje.

Balozi

 

05 September 2020, 08:13