Tafuta

Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu Roberto Bergamaschi, SDB kuwa Vika wa Kitume wa Jimbo la Gambella nchini Ethiopia. Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu Roberto Bergamaschi, SDB kuwa Vika wa Kitume wa Jimbo la Gambella nchini Ethiopia.  (AFP or licensors)

Askofu Roberto Bergamaschi, Vika wa Kitume Jimbo la Gambella!

Askofu Roberto Bergamaschi, SDB alizaliwa tarehe 17 Desemba 1954. Baada ya masomo na majiundo yake ya kitawa na kikasisi, tarehe 13 Septemba 1981 akaweka nadhiri zake za daima na kupadrishwa hapo tarehe 2 Oktoba 1982 Jimboni Brescia na Askofu Armido Gasparini, M.C.C.J, Vika wa kwanza wa kitume Jimboni Awasa, Ethiopia. Sasa amehamishiwa Jimbo la Gambella.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu Roberto Bergamaschi, SDB, kuwa ni Vika wa Kitume wa Jimbo la Gambella nchini Ethiopia. Kabla ya uteuzi huu, Askofu Bergamasschi alikuwa ni Vika wa Kitume wa Jimbo la Awasa, nchini Ethiopia. Askofu Roberto Bergamaschi, SDB alizaliwa tarehe 17 Desemba 1954, Jimbo kuu la Milano, Italia. Baada ya masomo na majiundo yake ya kitawa na kikasisi, tarehe 13 Septemba 1981 akaweka nadhiri zake za daima na kupadrishwa hapo tarehe 2 Oktoba 1982 Jimboni Brescia na Askofu Armido Gasparini, M.C.C.J, Vika wa kwanza wa kitume Jimboni Awasa, Ethiopia.

Mara baada ya kupadrishwa katika maisha na utume wake amewahi kupelekwa huko Ethiopia kuanzia mwaka 1982 hadi mwaka 1993 huko Dilla. Mwaka 1993- 2000 alikuwa Paroko wa Zway, Vikarieti ya Kitume ya Meki. Mwaka 1998- 2010 alikuwa ni Mkuu wa Shirika la Wasalesiani wa Don Bosco nchini Ethiopia na Eritrea. Aliwahi pia kuwa mkurugenzi wa Adwa kuanzia mwaka 2000 – 2004: Mkurugenzi wa shughuli za kitume za Wasalesiani huko Gotera Addis Ababa kuanzia mwaka 2004 hadi mwaka 2007 na Mkurugenzi wa Mekanissa, Addis Ababa kuanzia mwaka 2007 – 2009 na mwishoni, Paroko wa Parokia ya Bikira Maria Msaada wa Wakristo huko Dilla na Vika wa kitume Awasa. Alikuwa ni mjumbe wa Baraza la Kitume na Baraza la Wakleri. Tarehe 29 Juni 2016 Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa kuwa Vika wa Kitume Jimbo Katoliki la Awasa nchini Ethiopia.

29 September 2020, 15:12