Tafuta

Vatican News
Askofu mkuu Wojciech Zaluski ameteuliwa na Papa Franciko kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Malaysia, Timor ya Mashariki pamoja na kuwa ni Msimamizi wa Kitume Brunei Darusalam. Askofu mkuu Wojciech Zaluski ameteuliwa na Papa Franciko kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Malaysia, Timor ya Mashariki pamoja na kuwa ni Msimamizi wa Kitume Brunei Darusalam.  (Vatican Media)

Askofu mkuu Wojciech Zaluski: Balozi: Malaysia, Timor na Brunei

Askofu mkuu Wojciech Zaluski alizaliwa mwaka1960 huko Poland. Akapadrishwa kunako mwaka 1985. Tarehe 15 Julai, 2014, Papa Francisko akamteuwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Burundi. Akawekwa wakfu tarehe 9 Agosti 2014. Tarehe 29 Septemba 2020 akamteuwa kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Malaysia, Timor ya Mashariki na Mwakilishi wa Kitume wa huko Brunei, D.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Wojciech Zaluski kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Malaysia, Timor ya Mashariki na Mwakilishi wa Kitume huko Brunei Darusalam. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu Wojciech Zaluski alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini Burundi. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu Wojciech Zaluski alizaliwa kunako tarehe 5 Aprili 1960 huko Lomza, nchini Poland. Baada ya masomo na majiundo yake ya kikasisi, akapadrishwa kunako mwaka 1985 na tangu wakati huo, akajiunga na Taasisi ya Kipapa Diplomasia pamoja na kuendelea na masomo yake ya Sheria za Kanisa kwenye Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregoriana na hapo akajipatia shahada ya uzamivu.

Tarehe 15 Julai, 2014, Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Burundi na kumpandisha hadhi na kuwa Askofu mkuu. Akawekwa wakfu tarehe 9 Agosti 2014 na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican. Tarehe 29 Septemba 2020 Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Malaysia, Timor ya Mashariki na Mwakilishi wa Kitume wa huko Brunei Darusalam. Itakumbukwa kwamba, Baada ya masomo yake mwaka 1989 alianza kutoa huduma kwenye Balozi za Vatican kama Katibu mkuu wa Balozi huko: Burundi (1989 - 1991), Malta (1991 - 1994), Albania (1994 - 1996), Zambia (1996 - 1997), Sri Lanka (1997- 2000), Georgia (2000 - 2003), Ucrain (2003 - 2006) na Ufilippini (2006 - 2010). Kunako mwaka 2010 akateuliwa kuwa ni mshauri wa Ubalozi wa Vatican nchini Guatemala.

29 September 2020, 14:56