Tafuta

2020.09.08 ASKOFU. JOSEPH CHENNOTH 2020.09.08 ASKOFU. JOSEPH CHENNOTH  

Askofu Mkuu Joseph Chennoth aliaga dunia tarehe 8 Septemba

Tarehe 8 Septemba aliaga dunia Askofu Mkuu Joseph Chennoth,Balozi wa Vatican nchini Japan ambapo tarehe 17 Septemba 2020 misa ya kumwombea ilifanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro,Vatican kwa kuongozwa na Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican.Katika misa hiyo waliudhuria Wakuu wa Serikali na Maafisa wa huduma ya kidiplomasia.

Na Sr. Angela Rwezaula-Vatican

Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican, tarehe 17 Septemba aliongoza misa ya kumwombe Marehemu Askofu Mkuu Joseph Chennoth aliyekuwa Balozi wa Vatican nchini Japan na ambaye aliaga dunia tarehe 8 Septemba 2020. Katika kuanza mahubiri alitaka kuunhanika kwa namna ya pekee na Kanisa la Japan ambao walikuwa pamoja wakati huo wakiadhimisha misa ya ya mazishi na ambaye kwa miaka mwisho 9 amehudumua kama Balozi wa kitume katika Nchi hiyo. Na kutoka huko walipokea habari  za uchungu kutoka katika kambi ya kimisionari na ambazo zinahitaji kuunganika pamoja katika sala na kuokea katika mwanga wa imani.

Alizaliwa mnamo 1943 nchini India, na kuingia katika  huduma ya kidiplomasia ya Vatican  mnamo 1977, akafanya kazi katika Uwakilishi wa Kipapa huko Kamerun, Uturuki, Iran, katika Baraza la Masuala ya Umma ya Kanisa, na tena katika nchi ya Ubelgiji, Uhispania, nchi za Scandinavia na Uchina. (Taiwan) kama Mkuu wa masuala ya nje na  mnamo 1999, katika Kanisa hili, alipata kuwekwa wakfu kuwa askofu Mkuu, akiwa ameteuliwa kuwa Mwakilishi wa Kipapa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati na nchini Chad. Baadaye, alikuwa Balozi wa Vatican nchini  Tanzania kwa miaka sita na huko Japan kwa miaka tisa.

“Miaka miwili iliyopita, akiwa na umri wa miaka sabini na tano, aliwasilisha barua ya kung’atuka kwake ofisini kwa Baba Mtakatifu. Alikuwa na hamu ya kustaafu kwenda India, ili hatimaye kutoa  huduma ya kichungaji kwa watu wake. Walakini, Baba Mtakatifu alimwomba afanye bidii ili kuendelea, hasa kwa kuzingatia safari ya Kitume ya kwenda Japan, ambayo ilifanyika mnamo Novemba mwaka jana. Baba Mtakatifu Francisko na sisi tulioshiriki tunaweka hai kumbukumbu ya Askofu Mkuu Joseph mpole, mwenye ukarimu, aliyejitoa kikamilifu na hatimaye alifurahi sana kwa kufanikiwa  ziara ya papa, ambayo kwa maana fulani ilitawala utume wake huko Japan”. Kwa kuongozwa na Injili iliyosoma ambayo Yesu alikuwa akiwaomba wafuasi wake kuwa tayari inabainsha ushauri kwa namna ya pekee “ kuweni tayari na mikanda viunoni” (Lc 12,35).  Kila ambacho Yesu anataka ni vazi maalum. Vazi lilifungwa kiunoni linaelekeza kazi ilitolewa na safari. Hii inaelezewa vizuri katika katika Kitabu cha Kutona kwa ajili ya karamu Pasaka, kabla ya kuanza safari ya kwenda Misiari kukabiliana na usiku( Taz12,11).  Inakumbusha kuwa ili kuandaa vema safari ya maisha, ikielekeza kutoka kuekekea Nchi ya kweli  ya ahadi, hakuna haja ya kunaswa na ulimwengu, haijalishi kuonekana mzuri, lakini tu kujivika nguo ya huduma

Kusubiri Bwana katika roho ya huduma utafikiri katika maandiko ya Injili ndiyo kweli kinachohesabika. Vitu vingine vingi vinaonekana kuwa muhimu kwetu, ambavyo vinachukua umakini na hisia za hali. Lakini yote haya ni bure, Yesu anatuonya, na hata tujitahidi vipi kuwa mtu na kujua mambo zaidi, hatutaweza kuona muhimu, kukutana naye. Kiukweli, maandishi yanasema, katika saa msiyodhania (aya ya 40). Mungu anashangaza, Baba Mtakatifu anapenda kurudia maneno haya. Katika suala hili, Yesu, akiongea juu ya ziara yake kwetu, anaorodhesha tu wakati usiofaa kwa mfano katikati ya usiku au kabla ya alfajiri" (Taz haya 38). Wamebarikiwa, Yesu anarudia neno hili mara mbili katika mistari michache wale ambao hawaishi kwa kutarajia kitu kwao wenyewe, lakini kwa kumtarajia Yeye, kwa sababu anatosha. Heri wale wanaomngojea katika masaa yasiyowezekana, au wale ambao, kukaa macho, daima hubaki katika huduma daima

Akiendelea kukumbuka marehemu amesema, Askofu Mkuu Chennoth, mwaka jana, katika tukio la  kuadhimisha miaka 50 ya ukuhani, aliandika kumbukumbu kadhaa za tawasifu, ambazo, sio kwa bahati mbaya , alitaka kuipa jina “Daima na Mungu wangu mpendwa” (Always with my beloved God). Mwanzoni daima ni dalili ya nia yake ya maisha. Mnamo tarehe 22  Februari  mwaka huu, na baadaye katika sikukuu ya Ukulu wa Mtakatifu Petro, kwa aina fulani ya agano la kiroho alichagua maneno kadhaa ya kumshukuru Mungu, kwa jamaa zake na kwa wale wote ambao, aliandika, “wamenikabidhi utume katika Kanisa”. Aliendelea hivi “Ninakabidhi ya zamani yangu kwa huruma ya Kimungu na maisha yangu ya baadaye kwa maji mwenyezi Mungu, nikitamani kutembea mbele za Bwana hadi mwisho wa maisha yangu. Imekuwa ni bahati kwangu kuhudumia Mapapa, Kanisa la Ulimwenguni na Makanisa yote mahalia. Yaliyopita kwa huruma ya baadaye ni neema na ya sasa, tunaweza kusema, kwa Neema. Kutoka katika hili inaibuka hamu yake ya kuwa mbele za Bwana kila wakati, kusoma katika mpangilio wa maisha yake mwisho wa maisha  ( kairology" mahali halisi, ambapo Uratibu wa muda huamuliwa na Bwana na uratibu wa anga huamuliwa na huduma kwa Kanisa lake.

Joseph Chennoth, kabla ya kuondoka Chuo cha Kipapa cha Kikanisa, alisaini kwa maana hii tamko, kwa wakati ule, kukubali kwa uhuru kamili na roho ya utumishi nafasi zilizokuwa zikimsubiri, kujitoa mwenyewe. Kardinali maenukuu “kukubali marudio yoyote ambayo nitapewa dhamana, kulingana na mahitaji ya kazi, katika nchi yoyote na katika hali yoyote ya hewa, bila kuweka masharti yoyote au mapungufu katika siku zijazo”. Maisha yake, ambayo sasa ninaelezea kwa kifupi, kiukweli yametimika na nguo zilizobana kwenye kiuno, akiwa katika huduma na njiani, kila wakati kwa kuhifadhi  utulivu wa akili ambao uliambatana na raha ya kufurahi na isiyoingilia kamwe.

24 September 2020, 17:29