Tafuta

Vatican News
Askofu  Mario Grech ateuliwa na Papa Francisko kuwa Katibu mkuu wa Sinodi za Maaskofu. Askofu Mario Grech ateuliwa na Papa Francisko kuwa Katibu mkuu wa Sinodi za Maaskofu. 

Askofu Mario Grech: Katibu Mkuu wa Sinodi za Maaskofu!

Askofu Mario Grech alizaliwa mwaka 1957 huko Malta. Tarehe 22 Mei 1984 akapewa Daraja takatifu ya Upadre. Tarehe 26 Novemba 2005 akateuliwa na Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Gozo na kuwekwa wakfu tarehe 22 Januari 2006. Tarehe 2 Oktoba 2019 akateuliwa na Papa Francisko kuwa Katibu mwandamizi wa Sinodi za Maaskofu mjini Vatican.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko tarehe 15 Septemba 2020 ameridhia ombi lililowasilishwa kwake na Kardinali Lorenzo Baldisseri, Katibu mkuu wa Sinodi za Maaskofu la kutaka kung’atuka madarakani. Wakati huo huo, Baba Mtakatifu amemteuwa Askofu mstaafu Mario Grech wa Jimbo la Gozo lililoko nchini Malta kuwa ni Katibu mkuu wa sinodi za Maaskofu. Kabla ya uteuzi huu, Askofu Mario Grech alikuwa ni Katibu mkuu mwandamizi wa Sinodi za Maaskofu.

Itakumbukwa kwamba, Askofu Mario Grech alizaliwa tarehe 20 Februari 1957 huko Qala, Jimbo Katoliki la Gozo nchini Malta. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 22 Mei 1984 akapewa Daraja takatifu ya Upadre. Tarehe 26 Novemba 2005 akateuliwa na Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Gozo na kuwekwa wakfu tarehe 22 Januari 2006. Tarehe 2 Oktoba 2019 akateuliwa na Baba Mtakatifu Francisko kuwa Katibu mwandamizi wa Sinodi za Maaskofu mjini Vatican, akiwa na haki ya kurithi ofisi ya Katibu mkuu wa Sinodi za Maaskofu.

Katibu Mkuu Sinodi
16 September 2020, 16:16