Tafuta

Vatican News
2020.07.05 KARDINALI PIETRO PAROLIN KATIBU WA VATICAN 2020.07.05 KARDINALI PIETRO PAROLIN KATIBU WA VATICAN 

Vatican:Uteuzi wa mratibu wa Kamati ya kisayansi ya Mfuko wa Yohane Paulo I!

Kardinali Petro Parolini Katibu wa Vatican amemteua Mratibu wa Kamati ya kikundi cha wataalam kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli za utafiti na mafunzo ya kina juu ya wazo na mafundisho ya Papa Luciani baada ya miaka 42 tangu kuchaguliwa kwake kuwa Papa.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Katika siku ya kumbu kumbu ya mwaka wa 42 tangu alipochaguliwa Papa Yohane Paulo I, yaani kunako tarehe 26 Agosti 1978 akiwa ni mfuasi 263 wa Mtakatifu Petro, Rais wa Baraza la Mfuko wa Vatican wa Papa Yohane Paulo I Kardinali Pietro Paloni, Katibu wa Vatican amefanya uteuzi wa mratibu  wa Kamati ya kisayansi ya mfuko huo kwa watu wenye uwezo na uzoefu. Atakaye shika nafasi hiyo ya uratibu wa mfuko huo ni Dk. Stefania Falasca, Makamu Rais wa Mfuko huo. Ilikuwa tarehe 3 Julai 2020 walipotangaza Kamati ya mfuko  huo na tangu kuanza kwake, kwa utashi wa Papa Francisko ukiambatana na barua yake  (Rescriptum ex audentia) iliyotangazwa mnamo tarehe 17 Februari 2020, Mfuko huo kwa mujibu wa taarifa unafanya kazi kwa bidii ili kuimarisha muundo wake na kuandaa shughuli zinazochangia kuonyesha zaidi kazi ya Papa Yohane  Paul I kwa mujibu wa taarifa.

Kamati hii imeundwa na wajumbe kutoka vitengo mbali mbali

Kamati hii ambayo wajumbe wake wamechaguliwa kwa miaka mitano, wanajumishwa kutoka sehemu mbali mbali za viengo kama vile: Profesa Carlo Ossola, profesa wa philologist katika chuo cha Ufaransa huko (Collège de France) huko Paris; Profesa Dario Vitali, wa  mafundisho ya kikanisa na mkurugenzi wa Idara ya Taalimungu katika Chuo Kikuu cha kipapa cha Gregoriana; Monsinyo Gilfredo Marengo, profesa wa Elimu ya binadamu ya kitaalimungu na Makamu wa  Taasisi ya Kipapa ya Kitaalimungu ya Yohane Paulo  II kwa ajili ya  Sayansi ya Ndoa na Familia  katika Chuo Kikuu cha kipapa cha Laterano; Profesa Mauro Velati, mshiriki wa Mfuko kwa ajili ya Sayansi ya Kidini ya Yohane XXIII na katika shughuli za mchakato wa kutangazwa mtakatifu kwa Papa Yohane Paulo I na ambaye  tayari amekwisha andika  sehemu inayohusiana na miaka aliyokuwa huko Venezia  katika hati ya wasifu wake; Padre  Diego Sartorelli, mkurugenzi wa Maktaba na hifadhi ya majalida ya  Kihistoria ya Upatriaki wa Venezia na Loris Serafini, mtunza kumbukumbu, na mkurugenzi wa Jumba la Makumbusho la  Albino Luciani yaani (Papa Yohane Paulo I) huko Kanale  ya Agordo. Aidha Bodi ya Wakurugenzi imeamua kwamba katika awamu hii ya kwanza ya shughuli za mfuko, watashiriki kazi ya Kamati ya Kisayansi,  Rais wa Pango la hifadhi za Nyaraka za Kitume, Vatican Askofu Sergio Pagano na  Rais wa Maktaba ya Kitume ya Vatican Monsinyo Cesare Pasini.

27 August 2020, 15:03