Tafuta

Vatican News
Mama Maria mpalizwa mbiguni Mama Maria mpalizwa mbiguni 

Kard.Piacenza:Mama Maria hajawahi kwenda mbali nasi

Kupalizwa Mbinguni mwili na roho ya Mama Maria kunadhirihirisha na kutupatia udhibiti wa matumaini yetu kwa ajili ya wakati ujao ambao tunausubiri mara baada ya kifo na kwa ajili ya matatizo na mahangaiko yetu ya wakati, amesema hayo Kardinali Mauro Piacenza,Mhudumu Mkuu wa Toba ya Kitume.

Na Sr. Angela Rwezaula -Vatican.

Katika hali hali halisi ya Kupalizwa Mbinguni mwili na roho ya Mama Maria kunadhihirisha wazi na kutupatia udhibiti wa matumaini yetu kwa ajili ya wakati ujao ambao tunausubiri mara baada ya kifo na kwa ajili ya matatizo na mahangaiko yetu ya wakati. Amesema hayo Kardinali Mauro Piacenza, Mhudumu Mkuu wa Toba ya Kitume wakati wa mahubiri yake kwenye mkesha katika Groto ya Bikira Maria wa Maonesho mjini Roma ikiwa ni katika fursa ya kuhitimisha Novena ya Siku Kuu ya Kupalizwa Mbinguni Bikira Maria.

Kupalizwa mama ni msaada wa imani

Kupalizwa kwa mama Maria ni msaada wa imani yetu katika maisha ya wakati ujao kwa sababu yeye ni mwakilishi  wa kwanza na  wa dhati wa ufufuko wa miili yetu.  Mama Maria ni mmoja wetu na ikiwa ni mmoja wetu ambao tuko nyuma ya Yesu, Yeye ameingia katika ufalme wa Mbingu na kufungamanishwa utu wake ina maana kuwa, ukombozi wa miili yetu uko tayari umeanza, amekazia Kardinali Piacenza.

Mpalizwa mbinguni hajawahi kukaa mbali nasi

Pamoja na  kutukuzwa kwa namna ya pekee Mama Mpalizwa lakini hajawahi kwenda mbali na sisi. Mbingu ni dunia isiyoonekana na ya kweli zaidi mahali ambamo anaishi Mungu, Malaika na watakatifu, Kardinali Piacenza amesisitiza. “Mungu yuko karibu sana na sisi kwa sababu Muumbaji hajawahi kwenda mbali na viumbe wake”.

Katika janga linaloendelea watu wawe na mwanga na kuongoka

Kardinali Piacenza kwa kuhitimisha mahubiri yake amesali kwa sababu ya janga kubwa hili linaloendelea kutesa ubinadamu, ili watu wote waweze kuwa na mwanga wa tafakari na ulazima wa kuongoka katika jitihada zao wote za kusali na kuwa na mshikamano wa kikristo.

17 August 2020, 13:36