Tafuta

Familia ni ishara ya upendo mahali ambamo fadhila nyingi hukuzwa ndani mwake. Familia ni ishara ya upendo mahali ambamo fadhila nyingi hukuzwa ndani mwake. 

Bi Gambino:Ni katika mtindo upi familia inakuwa taasisi msingi!

Ni katika mtindo gani familia inakuwa ni taasisi ya lazima na msingi wa kufikia wema wa pamoja?Ni swali hili na pia kujibu kwa kirefu katika ujumbe wa Bi Gambino,Katibu Msaidizi wa Baraza la Kipapa la Walei Familia na Maisha alioutoa kwa njia ya video kwa washiriki wa Mkutano kuhusu siasa kwa ajili ya furaha ambo umeandaliwa katika harakati za tuki la mkutano ujao wa Uchumi wa Fancis.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican.

Katika ujumbe wa Katibu Msaidizi wa Baraza la Kipapa la Walei Familia na Maisha,  Bi Gambino anakazia juu ya injini ya kweli ya kuamsha kwa upya uchumi huku akiungana na Washiriki wa mkutano uitwao Kijiji  katika “siasa kwa ajili ya furaha”  na mbao umeandaliwa katika harakati za tukio la mkutano wa siku  zijazo kuhusu “Economy of Francis” yaani  “Uchumi wa Francis”. Mkutano huo ulifanyika kwa njia ya mtandao hivi karibuni kwa ushiriki wa vijana ulimwenguni kote. Katika ujumbe huu kwa njia ya video, Bi Gambino anasema “Hakuna muda wa sintofahamu kama alivyotueleza kwa nguvu Papa Francisko mbele ya madhara ya janga la corona. “Wale wote wenye kuhusika na sera za kisiasa, wajikite kwa ari zote kwa ajili ya wema na ustawi wa wote, huku wakitoa zana na vifaa vya lazima kuelekeza kwenye maisha yenye hadhi” (Ujumbe wa Pasaka 12.04.2020).

Upamoja katika hali ya maisha kijamii

Wema wa pamoja ina maana ya kuwa na “upamoja wa hali ya maisha ya kijamii ambao unawezesha kwa kiasi kikubwa  yale makundi pamoja na wajumbe binafsi  ili kufikia ukamilifu mpana zaidi na wa kasi (Gaudium et spes n. 26).  Wema huo hautokani kiurahisi na kuwa na idada ya vitu maalum vya kila mtu. Ustawi  wa pamoja ni kwa ajili ya  watu wote na kila mmoja yumo ndani mwake, kama jinsi alivyo na hasiyegawanyika na ni kwa njia ya upamoja tu, inawezekana kuufikia, kuutambua na kuulinda.  Mantiki yake ni ule mfumo ambao sisi sote tunatakiwa kuufuata, yaani kuanzia sisi binafsi, familia, makampuni na serikali. Hii inatakiwa kutafuta maana na wema katika mitindo mbali mbali ya maisha ya kijamii iliyopo ili kuhakikisha kwa wote ule usawa wa ugawaji wa mali.

Ni katika mtindo upi familia inakuwa taasisi msingi?

Bi Gambino akiendelea katika ujumbe wake aidha amesema kuwa hata hivyo lakini wema wa pamoja hauishii hapo peke yake kwa sababu unahitaji kufikia hatima ya mwisho ya binadamu ili kila mmoja aweza kujikamilisha. Kwa maana hiyo haiwezekani kupunguzwa katika ustawi wa jamii kiuchumi tu. Ni katika mtindo gani familia inakuwa ni taasisi ya lazima na msingi wa kufikia wema wa pamoja? Anauliza swali, Bi Gambino na kulijibu kuwa Familia ambayo inazaliwa kutokana na muungano wa kina wa maisha na upendo wa wenzi wenye msingi kati ya mwanaume na mwanamke, inamiliki asili yake ya ukuu kijamii na kama mahali msingi pa uhusiano binafsi na ikiwa ni mahala pa  kwanza na maisha ya kiungo cha kijamii. (Apostolicam actuositatem n. 11).   Familia ni mahali pa kwanza kwa ubinadamu wa mtu na jamii na utunzaji wa maisha na upendo. Familia ni kiini msingi cha mtu. Katika msingi huo wa kwanza na msingi wa muundo huo unaosaidia maendeleo safi ya ekolojia ya binadamu ni familia. (Centesimus annus n. 39).

Wenzi wa familia husaidia nguvu ya serikali kuendeleza ubinadamu

Wenzi wa familia katika msimamo na uhakika wa wajumbe wanatakiwa katika sababu hizi kusaidia nguvu ya Serikali na kwa hali yoyote ikiwa na msingi wa kila uwezekano wa kuendelea kukuza utu kibinadamu na ukuu wake kijamii. Uhusiano kati ya familia, ustawi wa pamoja na maisha ya uchumi ni yenye nguvu sana. Katika uhusiano ambao unatabia ya familia, unao uwezo wa kuzaa tabia za fadhila ndani ya soko na kama vile kushirikishana na mshikamano katika vizazina  kuvifanya viweze kuzalisha huduma. Familia inazaa rasilimali za kibinadamu na kufanya uwepo wa mzunguko wa uchumi kuanzia na mahitaji muhimu na uzalisha huduma. Hii ina nguvu ya mvutano wa mfumo wa kiuchumi. Na uzoefu wa janga hili la corona umeonesha wazi. Familia umeonesha kuguswa sana na kubeba madhara ya kibinadamu na kiuchumi yenye uzito mkubwa sana wa mgogoro. Ikiwa tunaweza kutumia ongezeko la kipato kwa ajili ya kununua mahitaji ya mali na sio vitu visivyostahili na kutumia muda mwingi kwa waleambao tunawapenda, ni wazi kwamba kila kitu kinaweza kubadilika, amesisita Bi Gambino.

Lazima kuachana na dhana ya ubinafsi na kutoa kipaumbele cha kijamii

Bi Gambino ametaja mambo kadhaa amabyo yanaweza kusaidia na kwamba ili kujikwamua ina maana na kuachana na dhana ya mtu   kibinafsi; kutambua watu na  kutoa kipaumbele cha kijamii katika familia kama msingi wa uzuri wa kawaida wa pamoja; Aidha inatakiwa kukuza hali ya kazi na utaratibu wa ugawaji sawa  kati ya majukumu ya utunzaji na majukumu ya kitaalam katika soko la kazi ili wanaume na wanawake wasilazimike kuachana na familia hasa katika mpango wa familia;  Vile vile amesema  kuwa wazi katika uchumi sio lengo la utimilifu wa wanadamu na uadilifu mzuri wa kibinadamu tu , lakini  pia ni jukumu la sehemu. Halli kadhalika inahitajika upyaisho wa mifano ya uchumi msingi inayokita juu ya uongofu wetu kibinafsi na ukarimu kwa wahitaji zaidi ... “Lazima tufanye kazi ili kushirikiana, mshikamano na ushiriki wa  kuwa na kanuni za soko kama nafasi ya mkutano kati ya watu, inayotawaliwa na uaminifu na uwazi”.

17 August 2020, 13:41