Tafuta

Vatican News
Askofu mkuu Giuseppe Pinto aliyekuwa Balozi wa Vatican nchini Croatia ameng'atuka kutoka madarakani tarehe 31 Julai 2020 Askofu mkuu Giuseppe Pinto aliyekuwa Balozi wa Vatican nchini Croatia ameng'atuka kutoka madarakani tarehe 31 Julai 2020  (ANSA)

Askofu Mkuu Giuseppe Pinto Ang'atuka Kutoka Madarakani

Askofu mkuu Giuseppe Pinto alizaliwa kunako tarehe 26 Mei 1952 nchini Italia. Tarehe 1 Aprili 1978 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Tarehe 4 Desemba 2001 akateuliwa na kuwekwa wakfu tarehe 6 Januari 2002. Taarifa zinaonesha kwamba, tangu wakati huo, ametekeleza dhamana na utume wake kama Balozi wa Vatican huko Senegal, Cape Verde, Mali, Guinea Bissau, Chile na Ufilippini.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko ameridhia ombi lililowasilishwa kwake na Askofu mkuu Giuseppe Pinto, Balozi wa Vatican nchini Croatia la kutaka kung’atuka kutoka madarakani. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu Giuseppe Pinto alizaliwa kunako tarehe 26 Mei 1952 huko Noci, nchini Italia. Baada ya masomo na majiundo yake ya kikasisi, kunako tarehe 1 Aprili 1978 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Tarehe 4 Desemba 2001 akateuliwa na Mtakatifu Yohane Paulo II kuwa Askofu mkuu na kuwekwa wakfu tarehe 6 Januari 2002.

Taarifa zinaonesha kwamba, tangu wakati huo, ametekeleza dhamana na utume wake kama Balozi wa Vatican huko: Senegal, Cape Verde, Mali, Guinea Bissau, Chile na Ufilippini. Tarehe 1 Julai 2017 akateuliwa na Baba Mtakatifu Francisko kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Croatia. Na ilipofika tarehe 31 Julai 2020, Baba Mtakatifu ameridhia kung’atuka kwa Askofu mkuu Giuseppe Pinto aliyekuwa Balozi wa Vatican nchini Croatia.

Askofu Mkuu Pinto

 

01 August 2020, 14:34