Tafuta

Vatican News
2019.01.08 wanawake, watoto na vijana na hata wa kiume wako hatarini katika mtego wa biashara mbaya ya binadamu 2019.01.08 wanawake, watoto na vijana na hata wa kiume wako hatarini katika mtego wa biashara mbaya ya binadamu 

Vatican:inahitajika mfumo wa kisheria unaolenga haki na uhuru

Kwa mujibu wa Monsinyo Joseph Grech Mwakilishi wa utume wa Kudumu wa Vatican katika Mashirika ya Kimataifa huko Vienna wakati wa hotuba yake kwenye Mkutano wa 20 wa Ushirikiano dhidi ya Biashara ya usafirishaji wa Watu, amesema kuwa inahitajika mfumo wa kisheria unaolenga haki na uhuru msingi wa waathiriwa dhidi ya biashara ya binadamu.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Vatican imesema kuwa inahitajika mfumo wa kisheria unaolenga haki na uhuru msingi wa waathiriwa dhidi ya biashara ya binadamu. Amesema hayo Monsinyo Joseph Grech Mwakilishi wa utume wa  Kudumu wa Vatican katika Mashirika ya Kimataifa huko Vienna wakati wa hotuba yake kwenye Mkutano wa 20 wa  Ushirikiano dhidi ya Biashara ya usafirishaji wa  Watu, Mkutano  ulioandaliwa katika mji mkuu wa Austria  kwa kushirikiana na Shirika la Usalama na Ushirikiano Ulaya(OSCE),kuanzia tarehe 20/22 Julai 2020.

Ni moja ya shughuli haramu zenye faida zaidi ulimwenguni, lakini pia ni moja ambayo kiwango cha ukosefu wa sheria bado ni kubwa sana. Usafirishaji wa watu leo ​​unawaathri watu  wapatao milioni 40. Na walio wengi ni wanawake, lakini pia wanaume, vijana watoto  na wasichana zaidi , wanaofikiriwa na mitandao ya uhalifu kama kifaa cha kubadilishana  na kupunguzwa katika  hali ya utumwa, unyanyasaji wa kijinsia na kazi za suruba, bado pia ndoa za utotoni kuuza watoto kiharamu hadi kufikia kuuza viungo na usafirishaji wa viungo. Hizi ni shughuli ambazo mara nyingi zinabaki bila kupata adhabu kali. Kila waathiriwa 2154 , leo hii ni mtu mmoja kati ya wafanya biashara haramu anahukumua, licha ya ongezeka la jitihada za taaasisi za kitaifa na kimataifa au mashirika yasiyo ya kiserikali kupambana na matukio haya.

Utaftaji njia mpya na  juhudi ili kumaliza mgogoro huu wa  kutokujali na kuhakikisha haki kwa wahathiriwa huku wakiwalinda, kuhakikisha heshima inayofaa kwa haki zao za msingi za binadamu ndiyo wito mkuu ambao umetolewa katika Mkutano huu wa “Ushirikiano dhidi ya Biashara ya watu”, Jukwaa ambalo ni la utetezi na kupambana dhidi ya biashara ya binadamu na ambalo linaleta pamoja mashirika ya kimataifa na asasi za kiraia. Tukio la mkutano huo limeongzwa na mada ya “Kukomesha kutokujali: kutekeleza haki kwa kushtaki wafanya biashara ya binadamu”.

Kwa mujibu wa Mosninyo Joseph Grech, ambaye alizungumza kwa niaba ya Utume wa Kudumu wa Vatican, katika Mashirika ya Kimataifa huko Vienna amesema, licha ya juhudi za jumuiya ya kimataifa, rasilimali ni chache, hasa kwa sababu ya mzozo unaoendelea wa kiuchumi na kukosekana kwa utulivu wa kisiasa katika mataifa mengi. Zaida ameongeza ufadhili usiofaa wa mifumo ya kitaifa ya mahakama inahimiza kuzingatia matokeo ya haraka, badala ya kukamatwa na kuhukumiwa kwa wahalifu wakumbwa na kwa maana hiyo rasilimali zaidi zinahitajika, lakini ambazo zinaweza kuleta tofauti ya kweli katika mapambano ya janga hili  hili. Matokeo yake amesema   ni kwamba kwa njia hii ya  kutokujali kwa wafanyabiashara wa binadamu basi wanapata mpenyo zaidi wa kunatekeleza uhalifu wao.

Kupata haki yaki yao waathiriwa isiwe ndiyo kusudi la mchakato wa kesi za kisheria dhidi ya wale wanaohusika, kwa mujibu wa mwakilishi wa Vatican katika hotuba yake ya tatu. Kinachotakiwa katika ni haki zao za kibinadamu  na ambazo lazima zihakikishwe kabla, kwa  wakati na baada ya mchakato. Hii ikiwa na maana ya  kuwaweka katika hali ya  kutoa ushuhuda dhidi ya wanyanyasaji wao kwa usalama, pamoja na mahojiano yaliyowekwa kumbukumbu au kwa kuwakilishwa na watu wawakili au wa tatu,  hakikisha fidia ya kutosha na wanatoa fursa kwa kujumuishwa tena kwa jamii.

23 July 2020, 15:53