Tafuta

Vatican News
Maandamano ya kila Ijumaa kwa ajili ya wakati endelevu huko  Duesseldorf Maandamano ya kila Ijumaa kwa ajili ya wakati endelevu huko Duesseldorf  (ANSA)

Vatican-Ask.Mkuu Jurkovič mabadiliko ya tabianchi ni tatizo kuu!

Mabadiliko ya tabianchi ni matatizo ya ulimwengu ambayo ni magumu katika mazingira,kijamii,kiuchumi,ugawaji sawa na kisiasa.Ni changamoto msingi za sasa kwa ajili ya binadamu.Kuishi ndani mwake,kuna lazimisha kufikiria sayari moja ya kuwa na mpango wa pamoja.Kwa Askofu Mkuu Jurkovič, Mwakilishi wa Kudumu katika ofisi za Umoja wa Mataifa, Geneva katika hotuba kwenye kikao cha Baraza la haki za binadamu.

Na Sr. Angela Rwezaula;-Vatican.

Mabadiliko ya tabia nchi ni matatizo ya Dunia na ili kukubiliana nayo mipango ya pamoja inahitajika, kwa mujibu wa Askofu Mkuu Ivan Jurkovič, Mwakilishi wa kudumu wa Vaticana katika Ofisi za Umoja wa Mataifa na mashirika mengine ya Kimataifa huko Geneva Uswiss wakati wa hotuba yake tarehe 9 Julai 2020 kwenye kikao cha 44 cha Baraza kwa ajili ya haki za binadamu. Mbele ya mateso ya maskini na unyonyaji wa nyumba yetu ya pamoja familia ya kibinadamu haiwezi kukaa ikitazama na kuwa na sintofahamu, amesema Askofu Mkuu Jurkovič. Kwa kunukuu Wosia wa Kipapa wa Papa Francisko wa Laudato si, kuhusu utunzaji wa nyumba yetu ya pamoja, kiongozi huyo ameongeza kusema “hali ya tabia nchi ni faida ya pamoja, ya wote na kwa ajili ya wote. Hali hiyo kwa ngazi ya kidunia ni yenye mfumo mgumu katika uhusiano wa hali nyingi za maisha ya binadamu (…) Mabadiliko ya tabia nchi ni matatizo ya ulimwengu ambayo ni magumu katika mazingira, kijamii, kiuchumi, ugawaji sawa na kisiasa na ambayo yunaunda kwa hakika changamoto msingi za sasa kwa ajili ya binadamu (…) Kuishi ndani mwake, kunatulazimisha kufikiria tena katika sayari moja kuwa na mpango mmoja wa pamoja.” 

Katika kipindi cha janga ni lazima kusaidiana kulinda nyumba ya pamoja

Serikali yoyote mdau yeyote binafsi, shirika lolote la kimataifa, amesisitiza askofu Mkuu, haviwezi kuwa na mafanikio kwa kutenda peke yake tu, kwa sababu ushirikisno na jitihada za wote ndizo msingi”. Aidha amekumbuka kuwa “katika kipindi hiki kigumu, kilichosababishwa na janga la Covid-19, tunaalikwa kusaidiana mmoja na mwingine na siyo kujibagua katika ubinafsi badala yake kuhamasisha na kulinda maisha ya binadamu kwa kutoa msaada  kwa wote wa kutosha katika matibabu, na  kuongezea mshikamano na kwa ajili ya kupambana na utamaduni wa ubaguzi”.

Mshikamano zaidi mpya ulimwenguni unahitajika

Kutokana na hilo ndipo mwakilishi wa kudumu ametoa wito wa “kuwa na mshikamano mpya wa ulimwengu” ili watu wote waweze kushirikiana kama chombo cha Mungu kwa ajili ya kutunza kazi ya uumbaji, kila mmoja katika utamaduni wake na uzoefu, mipango mipya na uwezo kwa ajili ya kulinda nyumba yetu ya pamoja. Ili kuweza kufanya hivyo misingi mitatu anasema  inahitajikna ambayo inatakiwa sasa ushirikiano wa kimataifa kwa ajili ya kulinda mazingira kwa ngazi ya ulimwengu. Msingi wa kwanza uliolekezwa na Askofu Mkuu Jurkovič  ni utambuzi kwamba mabadiliko ya tabia nchi yanaleta wasi wasi wa pamoja wa ubinadamu wote na kwa njia hiyo tunahitaji ushirikiano mkubwa kwa ajili ya familia ya kizazi kilichopo na kile kijacho.”

Inapotokea kukabiliana na masuala ya ulimwengu lazima kusahau mipaka na vizingiti

Msingi wa pili alioulekeza unatazama Mataifa kwa  uwajibikaji wa pamoja lakini kwa mujibu wa uwezo wao walio nao. Na msingi wa tatu hatimaye ni kuongeza nguvu ya kuamini kwamba “sisi sote ni familia moja ya kibinadamu”. Inapoteka kukabiliana na masuala ya ulimwengu, ameeleza, hapatakiwi kuwepo na mipaka au vizingiti, siasa au kijamii, au kwamba tunajificha   nyuma yake kile kisemwacho daima kuwa ni nafasi ya utandawazi wa sintofahamu. Kwa maana hiyo Askofu Mkuu Jurkovič anasema “mbele ya changamoto ya ustaarabu ambao unapendelea wema wa pamoja sisi tunahitaji mabadiliko chanya kwa maana hakuna uchaguzi zaidi ya kujali masuala msingi ya haki.

11 July 2020, 14:48