Tafuta

2020.07.23 Makataba ya Kitume Vatican 2020.07.23 Makataba ya Kitume Vatican 

Tovuti mpya ya Maktaba ya Kitume,Vatican tayari iko mtandaoni!

Tangu tarehe 16 Julai 2020,Tovuti mpya ya Maktaba ya Kitume Vatican iko tayari inafanya kazi katika mtandao.Taratibu zote zimerahisishwa za kuomba nakala za maandishi na vifaa vingine.Kwa mujibu wa Mkuu wa Maktaba anasema kuwepo kimwili unakuwa mgumu zaidi kutokana na janga na tovuti hiyo inataka kuwa mahali pa kukaribisha,kushirikiana na uwazi.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Tangu tarehe 16 Julai 2020, Tovuti Mpya ya Maktaba ya Kitume Vatican iko kwenye mtandao tayari. Upyaisho wa kuingia kwenye maktaba ya Papa kupitia Mtandao ilikuwa inaandaliwa kwa kitambo na ambayo kwa sasa ina sifa ya muundo mpya wa picha na ufikiaji rahisi wa yote yaliyomo na huduma zote  ambazo zimeimarishwa na kutajirishwa. Taratibu za kuomba nakala za maandishi na vifaa vingine vilivyowekwa kwenye Maktaba vimefanywa kuwa na  urahisi wa kuweza kufikiwa na uwazi zaidi. Kwa mujibu wa Mweyekiti wa Maktaba ya Kitume Vatican, Monsinyo  Cesare Pasini “Maandishi (Graphics) hutoka kwa haraka sana katika aina hii ya mawasiliano ya kidigitali, kwa maana hiyo walikuwa na utambuzi kwa muda mrefu kuwa kitu kipya, cha busara zaidi na  angavu zaidi kilikuwa kinahitajika.

Njia mpya na vifaa vipya kuwezesha huduma ya wasomoji na watafiti

Kwa mujibu wa Mkuu wa Maktaba anasema, pia kulikuwa na njia mpya, vifaa vipya ambavyo vilikuwa vinahitaji kuongezwa na tovuti iliyosasishwa kutoa huduma hizi zenye nguvu zaidi. Kwa upande mmoja tovuti hii imetulia kwani  kuna maandiko ya kusoma na picha za kuangalia  lakini pia  kuna utafiti wa kufanywa na yote haya yalikuwa yanahitaji uvumbuzi na mabi ni upyaisho katika tovuti mpya ambayo wametengeneza katika Tovuti hii mpya iliyowakilishwa. Wale ambao wanaingia kwenye maktaba katika njia hii sasa wanataka kujua, kuona, kushauriana na labda kuzingatia zaidi. Kwa njia hii lazima huduma  hizi lazima ziwe vitu vya kwanza vizuri ambavyo vinaweza kutazamwa, na kuwapatia  na hamu ya kujua na kufanya utafiti. Kwa maana hiyo inawezakana kutazama juu ya medali, sarafu, picha za kuchora, magazeti, vitu vilivyochapishwa, maandishi ya mikono.

Kila mmoja anaweza kupata kile anachotaka au katika lugha na tamaduni nyingi

Mtafiti au msimo anajua kile anachoweza kupata katika maktaba au labda anapata kitu ambacho alikuwa akitafuta katika masomo yake, lakini bado pia anaweza kujiingiza zaidi katika elfu za tamaduni, elfu za lugha ambazo wanazo kwenye maktaba ya Kitume  katika hazina yao na  lugha za historia ya ulimwengu. Mtafiti, msomaji na msomo kadhali anaweza  kupata habari muhimu za zamani na habari tofauti  za sasa katika maktaba ya Kitume. Na mwisho kuna ukurasa wa tweet yao: Twitter @bibliovaticana, ambayo inatangaza ratiba zao na mipango kwa njia ya haraka na uwazi zaidi. Pia Monsinyo Cessare amezungumzia juu ya umuhimu wa Tovuti yao katika huduma ya Papa kwamba, wao  wako kwenye maktaba ya Papa kwa sababu maktaba ni yake na imefunguliwa kuwa wazi kwa mapenzi yake kwa karne nyingi.

Huduma ni ya kisasa na ya haraka kufikia kile kona

Katika hili basi kwa mujibu wa wakuu amesema, wanataka kuwa kweli katika huduma ya wageni wao, kifaa cha kisasa cha haraka kufikiwa ambacho hutoa mara moja kile ambacho mtu anatafuta. Pamoja na wadau wengine, pia wanataka kujitambulisha kuwa wao ni wakina nani na kwa nini wanatoa huduma hiyo hasa ambayo inataka kufikia mipaka ya ulimwengu. Papa Francisko mara nyingi amezungumzia juu ya ukweli kwamba lazima tutoke nje na tufikie mipaka ya mbali na kwa maana hiyo,  Monsinyo Cessare anaamini kuwa hakuna kitu kama tovuti sasa iliyopo kwenye mtandao ambayo inaruhusu kufikia mipaka yote na nchi zote za ulimwengu, walio karibu na wa mbali. Ikumbukwe kwamba mara baaada ya Karantini, kunako tarehe Mosi Juni,2020,  Maktaba ya Kitume ilifunguliwa tena kwa watafiti na wasomi. Na kila hatua zimetangazwa katika Tovovuti hiyo mpya!

23 July 2020, 15:12