Tafuta

Vatican News
2020.07.10 Papa na Profesa Mario Draghi. 2020.07.10 Papa na Profesa Mario Draghi. 

Papa amefanya uteuzi wa Wajumbe wa Taasisi ya kipapa ya Elimu ya Sayansi jamii!

Papa Francisko amewateua wajumbe watatu katika Taasisi ya Elimu ya Sayansi Jamii ambao ni Profesa Mario Draghi,Profesa Kokunre Adetokunbo Agbontaen Eghafona,na Profesa Pedro Morandè Court.

VATICAN

Tarehe 10 Julai 2020 Papa Francisko amewateuwa wajumbe wa Taasisi ya Kipapa ya Elimu na Sayansi  jamii, wawili ni Profesa wa vyuo vikuu: Kokunre Adetokunbo Agbontaen Eghafona wa Nigeria, Profesa Pedro Morandè Court wa Chile  na Profesa Mario Draghi, ambaye aliwahi kuwa Rais wa Benki Kuu ya Ulaya.

Mario Draghi

Professa Mario Draghi alizaliwa Roma mnamo tarehe 13 Septemba, 1947. Alihitimu shahada katika sera ya siasa za Uchumi katika Chuo Kikuu cha  "La Sapienza" na kupata udaktari  wake katika Uchumi kwenye Taasisi ya Teknolojia ya Massachusetts. Kunako mwaka  1981 alikuwa Profesa wa kawaida wa Uchumi na Sera ya Fedha katika Kitivo cha “Cesare Alfieri” cha Chuo Kikuu cha Firenze, Italia. Amewahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia na baadaye, Meneja Mkuu wa Hazina ya Serikali ya Italia. Alikuwa Gavana wa Benki ya Italia tangu 2005 hadi 2011 na Rais wa Bodi ya Usimamizi wa Fedha tangu 2006 hadi 2011, alipochaguliwa kuwa Rais wa Benki Kuu ya Ulaya hadi 2019.  Yeye ni mwanachama wa Bodi ya Wakurugenzi wa Taasisi ya Mafunzo ya Juu (IAS) na Kikundi cha wataalam thelathini (G30). Yeye pia  ni mwandishi wa machapisho mengi,na michango ambayo inatazama uchumi mdogo hadi uchumi wa kimataifa na sera za fedha.

Pedro Morandé Court

Huyu ni Profesa mstaafu wa elimu jamii katika Chuo Kikuu Katoliki cha Kipapa nchini Chile. Profesa Pedro Morandé alizaliwa Santiago ya Chile, tarehe  3 Agosti 1948. Anayo shahada ya Elimu Jamii kutoka Chuo Kikuu Katoliki cha kipapa cha Chile (UC) na Udaktari wa Elimu Jamii katika Chuo Kikuu cha Friedrich-Alexander cha Erlangen-Nuremberg (Ujerumani).

Kokunre Adetokunbo Agbontaen Eghafona

Profesa Eghafona alizaliwa tarehe 1 Oktoba 1959 huko London. Mafunzo yake ya juu katika Chuo Kikuu cha Benin,kwenye mji wa Benin nchini Nigeria. Alipata digrii katika Historia na baadaye Mwalimu wa Sanaa.  Shahada ya Sayansi katika sanaa Chuo Kikuu cha Ibadan, nchini Nigeria. Amekuwa Profesa  wa Chuo Kikuu cha Benin katika Idara ya Sayansi,  tangu 1992; Baadaye Mkuu wa chuo mwandamizi 1996. Ameshika nyazifa mbalimbali za kiutawala, pamoja na kuwa Mkuu wa Idara ya Saikolojia na Anthropolojia, tangu 2009 hadi 2013 na Mkurugenzi wa mipango ya muda 2016. Amekuwa na jukumu la maendeleo endelevu ndani ya Mtandao wa suluhisho endelevu la Umoja wa Mataifa kuanzia 2012 hadi 2017.  Yeye ni mwandishi wa machapisho mengi ya kitaaluma. Licha ya shughuli zake za kisayansi ni pamoja na hatua za kupambana na biashara mbaya ya binadamu nchini Nigeria.

10 July 2020, 14:55