Tafuta

Vatican News
2020.07.11 Mwenyeheri Maria Antonia Samà 2020.07.11 Mwenyeheri Maria Antonia Samà 

Maria Antonia Samà mlei wa Calabria atatangazwa kuwa mwenyeheri

Aliishi zaidi ya miaka 60 akiwa kitandani amepooza na huku akiwaalika kila mtu kuwa na imani kwa Mungu na katika kila hali.Atatangazwa kuwa mwenyeheri na watumishi wengine wa Mungu ambapo Papa Francisko ameridhia fadhila zao za kishujaa alipokutana na Rais wa Baraza la Kipapa la Kuwatangaza watakatifu.

Na Sr. Angela Rwezaula; -Vatican

Katika mkutano uliofanyika tarehe 10 Julai 2020 kati ya Papa na Rais wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya kuwatangaza watakatifu, Papa Francisko ameridhia baraza hilo kutangaza hati za utambuzi wa fadhila zao za kishujaa kwa wenye heri wapya zinazohusiana na Miujiza kwa maombezi ya watumishi wa Mungu kutoka Italia, Uhispania  na mexico.

Ijumaa tarehe 10 Julai 2020 Papa Francisko amekutana na Kardinali Angelo Becciu, Rais wa Baraza la Kipapa la kuwatangaza wenye heri wapya na watakatifu. Katika mkutano wao, Papa ameridhia baraza hilo kutangaza hati za wenye heri wapya zinazohusiana na muujiza kwa maombezi ya Mtumishi wa Mungu Maria Antonia Samà, Mlei. Alizaliwa tarehe 2 Machi 1875 huko Mtakatifu Andrea Jonio (Italia) na kifo chake tarehe 27 Mei 1953; Yeye aliishi zaidi ya miaka 60 akiwa kitandani amepooza na huku akiwaalika kila mtu kuwa na imani kwa Mungu na kwa kila hali.

Fadhila za kishujaa za Mtumishi wa Mungu Eusebio Francesco Chini, Padre wa wa Shirika ya Yesu; Alizaliwa tarehe 10 Agosti 1645 huko Segno (Italia) na kifo chake huko Magdalena (Messico) tarehe 15 Machi 1711; Fadhila za kishujaa za Mtumishi wa Mungu Mariano Giuseppe de Ibargüengoitia y Zuloaga, Padre wa Jimbo na mwanzilishi msaidizi wa Shirika la Watumishi wa Yesu; Alizaliwa tarehe 8 Septemba 1815 huko Bilbao (Uhispania) na kifo chake tarehe 31 Januari 1888;

Fadhila za kishujaa za Mtumishi wa Mungu Maria Félix Torres, Mwanzilishi wa Shirika la Chama cha Mwokozi; Alizaliwa tarehe 25 Agosti 1907 huko Albelda (Uhispania) na kifo chake huko Madrid tarehe 12 Januari 2001; Fadhila za Mtumishi wa Mungu Angiolino Bonetta, Mlei wa Chana cha Wafanyakazi kimya wa Msalaba; Alizaliwa tarehe 18 Septemba 1948 huko Cigole (Italia)  na kifo chake tarehe 28 Januari 1963.

11 July 2020, 14:38