Tafuta

Vatican News
Mapacha waliotengenishwa vichwa vyao katika Hospitali  ya bambino' Gesu' Mapacha waliotengenishwa vichwa vyao katika Hospitali ya bambino' Gesu'  (ANSA)

Italia:Tukio la kihistoria la kutengenisha vichwa vya mapacha vilivyoungana!

Ni tukio la kwanza la namna yake kutokea nchini Italia na labda dunia nzima maana hakuna sehemu ambayo tukio kama hili limeandikwa ambapo katika Hospitali ya Kipapa ya Bambino Gesu',madaktari wake wameweza kuwatengenisha watoto mapacha waliokuwa wameunganika vichwa vyao tangu kuzaliwa.

Na Sr. Angela Rwezaula-Vaticn

Watoto mapacha wa kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati ambao walikuwa wameunganika vichwa kabisa sehemu ya nyuma ya fuvu na mfumo wa Vena sasa wapo salama baada ya kufanyiwa upasuaji katika hospitali ya Bambino Gesù mjini Roma.

Ni tukio la kwanza la namna hii kutokea nchini Italia, na labda dunia nzima maana hakuna sehemu ambayo tukio kama hili limeandikwa. Katika kufanikisha kukamilisha upasuaji huo mpaka mwisho,  tukio hilo limekuwa likifanyiwa utafiti kwa miezi 12 na upasuaji umefanyika mara tatu ambapo mara ya mwisho umefanyika tarehe 5 Juni 2020.

Katika mkutano wa Madaktari, wameridhia na ufanikishaji wa tukio hili na taarifa itasambazwa dunia nzima. Rais wa hospitali ya Bambino Gesù amekumbuka maneno ambayo waliyasema katika mkutano na mapacha huko Bangui, ambapo mapacha walikuwa hawana matumaini ya kuishi siku nyingi. Lakini leo, kiukweli maisha yao yanaokolewa!

08 July 2020, 10:59