Tafuta

Vatican News
Ni miaka 70 ya huduma ya matangazo ya kiingereza Afrika kwa ajili ya Radio Vatican Ni miaka 70 ya huduma ya matangazo ya kiingereza Afrika kwa ajili ya Radio Vatican  

Huduma ya Kiingereza Afrika ya Radio Vatican 1950-2020!

Ni miaka 89 tangu kuzinduliwa kwa Matangazo ya Radio Vatican.Ujumbe wa kwanza kutangazwa katika radio ulikuwa kwa lugha ya kilatino na Papa Pius XI,tarehe 12 Februari 1931.Na matangazo kwa lugha ya kiingereza kwa Afrika yakazinduliwa kunako mwaka 1950 kwa maana hiyo ni miaka 70 ya huduma ya kiingereza Afrika.Ni chereko chereko na vifijo.

Festus Tarawalie- Vatican na Sr.Angela Rwezaula- Vatican

Mwaka 2020 Radio Vatican imefikisha miaka 89 tangu ilipozinduliwa na Papa Pius XI kwa kutangaza ujumbe wa kwanza kwa kugha ya kilatino tarehe 12 Februari 1931. Program ya Kiingereza ilizinduliwa miaka sita baadaye kunako mwaka 1937 na matangazo ya lugha ya Kiingereza kwa Afrika yalianza kunako mwaka 1950, japokuwa ni mwaka 1979 ndipo huduma ya Kiingereza kwa Afrika ilianza kuitwa kama tunaitambua leo hii kwa maana  ya kuundwa ndani ya Program ya Kingereza kwa ujumla ili kutaka kujibu mabadiliko ya mchakato wa safari ya Bara.

Miaka 70 ya Idhaa ya Kiingereza kwa Afrika

Habari za jioni kwenye masafa mafupi

Huduma ya Kiingereza kwa ajili ya Afrika ilianza kama matangazo ya jioni kwenye masafa mafupi kwa wasikilizaji katika nchi zinazozungumza Kingereza na kusikiliza habari zinazotoka Vatican na Kanisa katika nchi za magharibi. Vile vile katika hatua za kwanza za vipindi vilijumuishwa masomo ya Katekisimu, maisha ya watakatifu na methali za Kiafrika. Vipindi hivyo vilitangazwa katika masafa mafupi kupitia njia ya kupokezana katika kituo cha matangazo cha Mtakatifu  Maria wa Galeria nje kidogo ya mji wa Roma. Matangazo ya FM kwa diaspora ya Italia badala yake yalipitia katika antenna iliyokuwa  juu ya Jumba la Makumbusho ya Redio Vatican ndani ya Jiji la Vatican.

Kanda kwa ajili ya Afrika

Kwa mujibu wa mwanahabari Sean Lovett, aliyekuwa mkuu wa zamani wa vipindi vya matangazo kwa  lugha ya Kiingereza na mjumbe wa kamati iliyoanzisha Huduma ya Kingereza Afrika,  anasema mpango wa awali ulikuwa sawa  sawa na ule wa Ulaya, Amerika ya Kaskazini na Austalia, lakini kuwa na mabadiliko kidogo tu kuendana na wasikilizaji barani Afrika. Kulikuwa  pia na vipindi  vilivyokuwa vinarekodiwa na kutumwa moja kwa moja kwa waamini kwenye bara kwa kutumia  kinachojulikana kama kanda kwa ajili ya Afrika.

Huduma ya Kiingereza Afrika na maono mapya

Kwa mujibu wa Lovett anasema walizingatia sana yafuatayo kabla ya kuanzisha huduma hiyo: “Kwanza, kuelewa ni mambo gani halisi ambayo yalikuwa yanahusiana na watu wa Afrika. Kwa maana hiyo, ili kubaini maswali kama vile huduma ya afya, haki, amani; Masuala ambayo yalikuwa yanawahusu watu ambao walikuwa wakisikiliza huko barani Afrika. Changamoto ya pili ilikuwa ni kutaka kumwangamiza yule mkoloni, wa maono ya Ulaya kama kwamba mambo yote  mabaya tu yanatoka  barani Afrika na kujaribu kuunda maono mapya ya Afrika, maono chanya ya Afrika kama mahali ambapo panaweza kutumika  kama mfano kwa wengine wote Ulimwenguni katika vitu vingi, amesisitiza Lovett.

Usomaji wa Injili ya Kiswahili katika Huduma ya Kiingereza Afrika (1993)

Ilikuwa ni mwaka 1993 ambapo  Huduma ya Kiingereza Afrika ilianza hata matangazo ya kila siku ya usomaji wa Injili ya Kiswahili, ambayo ni lugha ya kibantu na lugha itumikayo  Afrika Mashariki. Mwaka mmoja baadaye, ikawa idhaa ya lugha Kiswahili ya Radio Vatican ikiwa chini ya Huduma ya Kiingereza Afrika. Kiswahili kinazungumzwa sana nchini Tanzania na Kenya na katika baadhi ya maeneo ya Uganda, Burundi, Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Msumbiji. Inakadiriwa watu milioni 120, au zaidi wanaozungumza au kuelewa Kiswahili.

Huduma ya kiHausa kwa  muda mfupi

Tukio lingine muhimu katika historia ya Huduma ya Kiingereza Afrika ya Radio Vatican, ingawa ilikuwa ya muda mfupi ni uundaji wa matangazo ya kila siku katika lugha ya kiHausa, kunako mwaka 2002 ambayo ni lugha ya Kiafrika inayozungumzwa na watu wapatao milioni 100 hadi 150. Katika kihistoria, inachukuliwa kama lugha nyepesi na pana katika sehemu kubwa ya Afrika Magharibi. Kipindi hicho cha  dakika 15 kililenga malezi ya Kikristo na kilitangazwa saa 3.00 asubuhi, Roma, mara tu ilipokuwa inamalizika kipindi cha kawaida  cha Huduma ya Kiingereza Afrika. Kipindi katika lugha hiyo ya  kihausa kilikuwa kinaongozwa na  Wafanyakazi wa Radio Vatican kwa kushirikiana na Kituo cha Mawasiliano ya  Jamii cha Kaduna nchini Nigeria.

Sinodi ya kwanza ya Afrika na muundo mpya

Matangazo ya sasa ya nusu saa kila siku ya Kiingereza Afrika yalichukua muundo wake. Muundo huo unashughulikia mada nyingi zilizopendekezwa katika Wosia wa Kitume wa mwaka 1995, mwaka mmoja baada ya Sinodi ya kwanza ya Afrika: ‘Ecclesia in Africa’ yaani ‘Kanisa la Afrika’ wa Mtakatifu Yohane Paulo II.  Vipengere zaidi vilianzishwa baada ya kuchapishwa kwa Wosia wa ‘Africae Munus’ yaani “Dhamana ya Afrika” wa Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI  baada ya Sinodi ya Pili ya Afrika 2009.

Sehemu za matangazo ya vipindi

Hata hivyo mbali na habari juu ya Baba Mtakatifu, shughuli za Vatican na Kanisa  la ulimwenguni,  vipindi vya kila siku vya Kiingereza Afrika bado vina sehemu za makala na sehemu zilizowekwa zinazohusu maisha ya Kanisa barani Afrika, na zaidi kuhusu masuala ya haki, amani, maridhiano, maendeleo, utamaduni na jukumu la vijana katika Kanisa na jamii, katika  yote hayo na mlengo na kujibu changamoto zinazokabili bara hilo. Kwa kuongezea na hayo kuna habari ya kila siku juu ya matukio ya kijamii na kisiasa barani Afrika ambayo tunayaita, “Afrika News Panorama”, yaani mtazamo mpana wa habari za Afrika.

Alfajiri ya enzi za digitali

Mnamo mwaka wa 2017, matangazo yetu ya kila siku kwa wasikilizaji wa  Roma yalibadilishwa kutoka katika jukwaa la FM hadi kuiingia katika  Digitali ya  Radio DAB +. Kwa kuongezea, matangazo yetu kwa njia ya masafa mafupi kwenda Afrika sasa yanaelekezwa kutoka kituo cha matangazo hadi kisiwani Madagaska.

Makala katika tovuti kuhusu Kanisa la Afrika

Sehemu ya mabadiliko katika vyombo vya habari vya utangazaji na muktadha wa mitandao ya kijamii ndiyo njia tunayopita na ambayo imeazimiwa kuhamia kwa namna  fulani katika kupanua uandishi. Yaani njia ya uandishi wa uunganishwaji. Kwa  njia hiyo, mbali na mikondo yetu ya kiutamaduni, sasa tunachapisha hata makala kwenye tovuti kutoka katika baadhi ya historia za Kanisa la sasa ili kueneza habari katika bara zima. Hii inakuza sauti na mitazamo ya Kanisa barani Afrika, vile vile imeleta maendeleo muhimu kwa sababu inafungua mchakato wa mawasiliano kama njia mbili kutoka katika Kanisa la ulimwengu na njia nyingine inayoizunguka.

Podcast ya kila siku

Vipindi vyetu vya kila siku vinaweza kupakuliwa na kusikilizwa wakati wowote wa siku kutoka katika sehemu ya podcast kwenye  tovuti yetu ya www.vaticannews.va, Tunayo pia kupitia ukurasa wa Facebook katika program ya Kiingereza.

Huduma ya Kiingereza Afrika inatangazwa tena kupitia Redio Katoliki za FM

Katika bara la Afrika wakati huo huo, karibia vituo 40 vya redio Katoliki, pamoja na vituo vya matangazo ya Radio Maria vinarudia kurusha vipindi vyetu kila siku kwa Kingereza. Hii inahakikisha kuwa tunawafikia mamilioni  ya wasikilizaji ambao hawana masafa mafupi au mahali ambapo ishara za masafa ni dhaifu. Vituo vingi vya redio Katoliki ambavyo vinarusha tena vipindi vyetu vinamilikiwa na majimbo  mbali mbali Katoliki barani Afrika, kwa mfano katika parokia, mashirika ya kidini na baadhi ya mitandao ya Radio Maria.  Na ombi la kutuma kipindi kupitia WhatsApp linazingatiwa.

Wafanyakazi

Wafanyakazi wa kitengo cha Huduma ya Kiingereza Afrika ni watu wanne, ambao ni kutoka Sierra Leone, Uganda na Zambia, pamoja na wengine wawili kutoka Tanzania katika idhaa ya lugha ya Kiswahili. Pamoja na hayo tunashirikiana na wahudumu kadhaa, waandishi, marafiki na wageni na Maaskofu binafsi wa mabaraza ambao wanatusasisha kila mara habari,  pia habari juu ya bara lai  la Afrika. Vile vile kuna wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya Kipapa mjini Roma hawa ni makuhani, watawa, waseminari, walei  ambao kwa kawaida hutoa huduma yao kutusaidia. Na kwa kila mwaka, tunapokea kwa wastani kati ya wanafunzi watatu hadi wanne au zaidi wanaokuja kwa kipindi  kujifunza katika  Huduma yetu ya Kiingereza Afrika au katika lugha yetu ya Kiswahili.

Mtandao wetu barani Afrika unakua

Tunapoangalia siku zijazo, changamoto kubwa ya  Huduma ya Afrika, kwa ujumla ni jinsi gani ya  kuunda mtandao wa vituo vyote  vya redio na majimbo barani Afrika, kwa maoni na kubadilishana zaidi habari juu ya shughuli za Kanisa, tunakubali kusikiliza maoni, kwa kutumia barua pepe hizi: inglese.africa@spc au paul.samasumo@spc.va.

Laudetur Iesus Christus, Tumsifu Yesu Kristo, Praised be Jesus Christ!

15 July 2020, 16:30