Tafuta

Vatican News
Mshikamano wa dhati unahitajika katika kipindi cha virusi vya corona. Mshikamano wa dhati unahitajika katika kipindi cha virusi vya corona.   (AFP or licensors)

Covid-19.PAV:maadili muhimu yanahitajika kulinda wadhaifu zaidi!

“Humana communitas” katika wakati wa janga.Tafakari la sasa kuhusu kuzaliwa upya maisha”:ndiyo hati mpya ya Taasisi ya Kipapa kwa ajili ya Maisha(Pav) kuhusu matokeo ya mgogoro wa kiafya uliosababishwa na virusi vya corona.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Covid imeukumba ulimwengu mzima na kufanya ulimwengu ubaki umetengwa. Tunaishi tayari katika kipindi hiki kwa muda mrefu. Ni uzoefu ambao bado haujamalizika na unaweza kudumu bado kwa muda mrefu. Lakini ni tafsiri gani ya tunaweza kuitoa? Kwa hakika tunaalikwa kukabiliana nayo kwa ujasiri. Utafutaji na maelezo ya kisayansi yanahakikisha jambo ambalo limesababaishwa na janga. Lakini tunaitwa kuwa na utambuzi zaidi wa kina. Ikiwa ndiyo hivyo hata kwa namna ya kuwa mbali zaidi lakini itazuia kuangukia kwenye mtego.  Lakini je! itatuzuia kutoka katika mtego wa hali ya kutojali, au mbaya zaidi, ya kulazimika kujiachia? Inawezekana kuchukua hatua ya kurudi nyuma na  ambayo haimaanishi kutotenda kazi, bali kuwa na wazo ambalo linaweza kugeuka kuwa shukrani kwa ajili ya  maisha tuliyopewa, kana kwamba ni njia ya kuelekea katika kuzaliwa upya kwa maisha? Ndiyo maswali yanavyoanza kwenye Hati mpya ya “Humana Comunitas” katika wakati wa janga. Tafakari la sasa kuhusu kuzaliwa upya maisha”: iliyotolewa na Taasisi ya Kipapa kwa ajili ya Maisha(PAV) kuhusu matokeo ya mgogoro wa kiafya uliosababishwa na virusi vya corona.

Utekelezaji wa mshikamano kimataifa 

Hati ya PAV iliyotolewa tarehe 22 Julai 2020 inafafanua hali halisi ya maisha ya sasa kwa kutaka kuzaliwa kwa upya maisha baada ya athari za janga lililosababishwa na virusi vya corona. Hati hii inafuata nyingine iliyotolewa kunako tarehe 30 Machi 2020 kwa jina la “Janga na Udugu ulimwengu.” Kiini cha Hati  hiyo kimejikita kwenye fafanuzi za misingi mitatu kwanza maendeleo ya maadili ya hatari, utekelezaji wa ushirikiano wa kimataifa na kuhamasisha mshikamano wenye dhamana.

Janga limetufanya kujua kuwa kila kitu kimeunganishwa 

Hati hii imefunguliwa kwa maswali kuhusiana na somo tulilojifunza. Jibu lake ni kuhusu funzo la udhaifu ambao umegusa wote zaidi waliolazwa hospitalini, wafungwa katika magereza, wakimbizi katika makambi ya wakimbizi. Lakini kuna hata fundisho jingine kuwa  na utambuzi wa maisha kwamba  ni tunu msingi.  Vile vi janga limetufanya tuelewa kuwa kila kitu kinaunganisha pamoja na kwamba Dunia iko kwenye mtego na uchaguzi wa kiuchumi kulingana na uchoyo na utumiaji mwingi ambao unaleta  athari kubwa katika  kuenea kwa virusi.

Umakini kwa watu walio katika mazingira magumu

Umakini mkubwa unapaswa kutolewa kutegemeana na wanadamu na mazingira magumu ya pamoja Hati inabainisha, kwa sababu wakati Nchi ambazo zimefunga mipaka yake na zadi wengine kuweka hata mchezo wa kutupiana lawama, kwa bahati mbaya wanasisitiza kwamba virusi havijuhi mipaka. Kwa maana hiyo ni wito wa Taasisi ya Kipapa ili kuwepo na makakati wa nguvu kwa ajili ya kushirikishana taarifa, kutoa msaada na hata rasilimali. Kwa namna ya pekee jitihada zinawekwe kwenye maendeleo ya tiba na chanjo. Katika muktadha huo, kiukweli ukosefu wa uratibu na ushirikiano ni kizingiti kikubwa cha kutibu na kudhibiti Covid-19.

Umuhimu wa maadili muhimu ya kuwajibika

Hati ya PAV katika kuuliza swali ni kitu gani cha kufanya, inasisitiza umuhimu wa kuwa na maadili muhimu  yenye uwajibikaji na maalum mbele ya watu ambao afya yao maisha na hadh zao  ziko hatarini zaidi. Na kwa upande wa pili Taasisi ya Kiapa ya Maisha inaalika kuwa na jitihada za ulimwengu na ushirikiano kimataifa ili kweli iwezekane kutambuliwa kama haki ya binadamu ulimwengu ya “upatikanaji wa huduma bora za afya na dawa muhimu”.  Na wakati huo huo, wakiwa na tumaini moja la utafiti wa kisayansi unaowajibika, au tusema fungamani na huru kutoka katika migogoro ya afya binafsi na ambayo imajikita katika kanuni za usawa, uhuru.

Uhamasishwaji wa mshikamano

Upeo kwa maisha ya umma kwenye utafiti hauwezi kutolewa sadaka juu ya faida binafsi, Taasisi ya Maisha inathibitisha, na ndiupo inasisitiza umuhimu wa Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO ) ili waweza kusaidia hasa mahitaji na wasiwasi katika Nchi ambazo hazijaendelea ili kukabiliana na  janga ambalo halijawahi kutokea. Na hatimaye katika Hati ya Taasisi ya Kipapa ya Maisha, ni tumaini la  uhamasishwaji wa  mshikamano  unaowajibika na ambao utambue kweli hadhi sawa ya kila mtu, kwa namna ya pekee anayeishi na uhitaji zaidi. Na kumalizia wanatoa  mwaliko wa kuwa na tabia za matumaini kwa maana “Ni wakati wa kufikiria na kutekeleza mpango  wa kuishi kwa binadamu unaoruhusu maisha bora ya wakati endelevu kwa wote”.

22 July 2020, 14:03