Tafuta

Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Claudio Gugerotti kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Uingereza Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Claudio Gugerotti kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Uingereza 

Askofu mkuu Claudio Gugerotti, ateuliwa kuwa Balozi Uingereza!

Askofu mkuu Claudio Gugerotti alizaliwa tarehe 7 Oktoba 1955. Tarehe 29 Mei 1982 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Tarehe 7 Desemba 2001, Mtakatifu Yohane Paulo II akamteuwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Georgia na Armenia na kumpandisha hadhi kuwa Askofu mkuu. Mtakatifu Yohane Paulo II, tarehe 6 Januari 2002 akamweka wakfu kuwa Askofu mkuu. Sasa ni Balozi nchini Uingereza.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Claudio Gugerotti kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Uingereza. Kabla ya uteuzi huu Askofu mkuu Claudio Gugerotti alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini Ukraine. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu Claudio Gugerotti alizaliwa tarehe 7 Oktoba 1955 huko Verona, nchini Italia. Baada ya malezi na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 29 Mei 1982 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Tarehe 7 Desemba 2001, Mtakatifu Yohane Paulo II akamteuwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Georgia na Armenia na kumpandisha hadhi kuwa Askofu mkuu.

Tarehe 13 Desemba 2001 akateuliwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Azerbaijan. Mtakatifu Yohane Paulo II, tarehe 6 Januari 2002 akamweka wakfu kuwa Askofu mkuu.Tarehe 15 Julai 2011, Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI akamteuwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Belarus. Tarehe 13 Novemba 2015 Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Ukraine. Tarehe 4 Julai 2020, Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Uingereza.

Uingereza
04 July 2020, 13:34