Tafuta

Vatican News
2019.10.28 Askofu  Mkuu Vincenzo Paglia 2019.10.28 Askofu Mkuu Vincenzo Paglia  

Ask.Mkuu Paglia:unatakiwa uongofu wa maadili ili kushinda janga la kiafya!

Rais wa Taasisi ya Kipapa ya Maisha (PAV),Askofu Mkuu Vincenzo Paglia,katika kuwakilisha hati mpya iliyotolewa na Taasisi hiyo anasisitizia kuhusu mantiki tofauti zilizomo kwenye Hati hiyo iliyopewa jina:‘Humana Communitas’ na ambayo ni hati ya pili ya Taasisi hiyo inayojikita katika masuala ya matokeo ya mgogoro wa kiafya ulimwenguni na tafsiri yake ya kina.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican.

Kitu kinachotuunganisha na kile kinachotengenisha kama binadamu ambao kwa sasa tunajikuta tunashirikishana uzoefu mmoja na matokeo ya janga, ni kujiuliza ni wapi tupate ujasiri wa kuanzia. Ndiyo anafafanua Askofu Mkuu Vincenzo Paglia, Rais wa Taasisi ya Kipapa ya Maisha, katika mahojiano yake kuhusiana na Hati mpya ya Baraza hilo (PAV) baada ya Covid-19  iliyotangazwa tarehe 22 Julai 2020. Katika mahojiano hayo ameanza na kauli mbiu inayoongoza Hati hiyo hadi kufikia changamoto kwa jumuiya ya kikristo katika wakati huu mgumu. Akianza kueleza kichwa cha Hati kiitwacho “Humanae Communitas’ katika wakati janga, anasema hiki ni  kichwa cha barua ya Papa Francisko aliyowaelekeza Taasisi hiyo  kunako tarehe  6 Januari 2019, wakati wanaadhimisha miaka 25 tangu kuanzishwa kwa Taasisi hiyo. Papa alikuwa anawaomba watafakari kuhusu uhusiano unaounganisha jumuiya ya binadamu na ambayo inazaa thamani, maelewano, na ushirikishano wa pamoja.

Na janga hili linafanya kuwa na utambuzi mara mbili, kwa upande mmoja ni kuona kuwa sisi sote tunategemeana. Kile ambacho kinatokea sehemu mmoja katika upande mwingine wa nchi kinaunganishwa  hata ulimwengu mzima. Na kwa upande mwingine ni kuonesha kutokuwepo na usawa kwani anasisitìza “tumo ndani ya dhoruba inayofanana lakini siyo katika mtumbwi mmoja. Aliyemo kwenye mtumbwi mdhaifu, anazama kwa urahisi zaidi”. Kwa maana hiyo maadili ya maisha yanageuka kuwa ya ulimwenguni mzima. Swali :Tutajaribu kujiokoa wakati tunakwenda mbali na wengine zaidi, au udhaifu unaotuunganisha, utatufanya sisi tuwe wanadamu zaidi? Lazima tujibu swali hili na lazima tulifanye sasa. Je kuwa binadamu bado ni jukumu la pamoja? Ni maswali ya Askofu Mkuu Paglia. Na sehemu ya kichwa cha   Hati hiyo  inatoa tafakari  kuwa isiyo ya kawaida yaani ya kuzaliwa maisha kwa upya na kwa maana hiyo amebainisha Askofu Mkuu Paglia kuwa  ni ufunguo ambao unatokana na utamaduni wa kifalsafa. Hapa ni kutaka kutoa chachu zaidi ili kuelekeza juu ya dharura katika kutafuta mawazo mapya ya jumuiya ambayo utafikiri siyo jambo la kisasa. Katika wakati ambao maisha utafikiri yamesisimama na kukumbwa na vifo vya watu wapendwa waliokuwa ni kama  viongozi katika  jamii, Askofu Mkuu amesisitiza “hatuwezi kubaki katika kujadili kibarakoa au kurudia rudia juu ya ufunguzi wa mashule, huu sio wakati wake! Lakini zaidi ni kutafuta zile nafasi za kuwa na ujasiri wa kujadili hali halisi iliyo bora na kuelekeza katika masoko na elimu na ndiyo maana ya neno isiyo ya kawaida”, amebainisha.

Askofu Mkuu Paglia akijibu kuhusu hali halisi juu ya Janga ambalo limeonesha udhaifu kutoka Kaskazini hadi kusini mwa dunia na wakati huo huo wanasayansi bado hawana jibu la uhakika, yeye anabainisha kwamba mapya hayaonekana  katika kuzuka kwa virusi visivyo julikana. Kiukweli, ilikuwa inawezekana hata kuzungukwa na kushindwa kwa kubaki ndani ya nchi na kuzuia uharibifu mkubwa bila kutoka nje. Lakini tatizo ambalo halijawahi  kutokea  ni kile kitendo la ukasi na upana wa usambaaji  kupitia mtandao wa mahusiano na usafirishaji. Kwa upande mwingi ni suala jipya lakini wakati huo  ni jukumu la vyombo vya habari, ambavyo waliamua ni jinsi  gani ya kutoa habari juu ya  shida  na katika kuzuia kuenea kwa janga la virusi  na  habari za kugushi  kuhusu janga hili zilitokea. Kwa maaana hiyo kumekuwapo na mchanganyo wa uelewa hasa katika enzi ya janga katika jamii. Hata hivyo bado udhaifu  upo katika jamuiya, na  ambayo ilipaswa kutupatia uhakikisho wa msaada na ulinzi katika hatari, badala yake imetuacha  tubaki  kutokuwa na uhakika na udhaifu wetu.

Askofu Mkuu Paglia kadhalika amesema propaganda za kisiasa nazo zinachangia na ni makini katika halisi ya nchi fulani na ni changamoto ambayo ilitukumba bila kujiandaa katika mifumo ya kiafya.  Kwa maana hiyo hali halisi inaruhusu kuboresha ustadi na rasilimali, katika njia ya kutathmini na ambayo ni muhimu na uwezo wa kuendelea kuguswa kwa dhati. Vile vile amebainisha Askofu Mkuu kwamba ustadi wetu wa ufundi na uingiliaji wa usimamizi ulidanganyika kwamba tunaweza kuweka kila kitu chini ya udhibiti. Badala yake hata katika jamuiya zilizo tajiri zaidi kiuchumi, janga hili limezidi uwezo wao wa vifaa vya huduma za afya na maabara. Ilikuwa ngumu kufahamu hili la kutofaulu kwetu na kutambua vile vizingiti vyetu tulivyo navyo. Askofu Mkuu kadhalika amezungumzia juu ya kile ambacho tumejifunza kuhusiana na suala la  afya ya umma kwamba ni muhimu kuwekeza vizuri rasilimali katika kuzuia magonjwa ya kuambukizwa  na katika matibabu. Hii inamaanisha kuzingatia na wala siyo tu katika hospitali, bali kwenye mitandao yote ya ndani ya nchi ili iweze kuwpata  msaada na kwa elimu ya afya. Kwa kuongezea, amesema, tumejifunza kuwa afya ya kila mtu inahusiana sana na afya ya wote. Kwa maana hiyo inahitaji kuwa na tabia ya uwajibikaji na siyo  tu kulinda ustawi wa mtu binafsi lakini pia kwa ajili ya wengine.

Suala jingine muhimu katika mahojiano hayo ni kuhusu soko la chanjo hasa katika kuepuka ukosefu wa usawa wa kiafya kwa wale ambao wanaishi katika nchi matajiri na maskini. Kwa mujibu wa Askofu Mkuu Paglia amesema inahitaji utafiti udhibitiwe ili kwamba usiwe ni kwa ajili ya maslahi ya kisiasa na kiuchumi(kwa wachache), bali iweze kufanyika kwa uhuru na uwajibikaji. Kwa sababu hii,ufadhili lazima uwe wazi na ushirikishwe, ili faida pia ziweze kusambazwa kwa usawa. Hata hivyo kwa mujibu wa Askofu Mkuu  Paglia amesema  janga hilo limeonyesha kuwa hakuna nchi inayoweza kuendelea kwa  kujitegemea yenyewe bila wengine na siyo tu kwa sababu za kiafya, bali hata  kwa sababu za kiuchumi. Kwa maana hiyo Shirika  linaloratibu shughuli za kiafya linapaswa kuungwa mkono na wote na katika hatua mbali mbali za ufuatiliaji, kutayarisha na matibabu ya magonjwa na ambayo linaruhusu mzunguko wa habari ambazo ni muhimu. Shirika la Afya Ulimwenguni WHO limeonekana kuwa muhimu sana, hata kama limepata udhaifu kidogo, lakini lazima tujifunze kutokana na  makosa na kuboresha utendaji wake. Ni kwa njia hii tu tunaweza kufanya  sheria iwe moja ya haki ulimwengini na kwa ngazi ya juu katika kutunza afya kama kielelezo cha kulinda  maisha na hadhi ya kila mwanadamu.

Kwa mujibu wa Askofu Mkuu Paglia amesema kuwa jumuiya ya wakristo inaweza kusaidia kutafsiri mgogoro, na siyo tu  kwamba  shirika ndilo ambalo linatuwezesha kuondokana na kuboresha ufanisi. Hili ni suala la kuelewa kwa undani zaidi na kwamba kutokuwa na hakika na udhaifu ni sehemu ya hali halisi ya mwanadamu. Kizingiti hiki lazima kiheshimiwe na kukumbukwa katika kila mpango wa maendeleo, katika utunzaji kwa walio hatarini na kwa sababu tumekabidhiwa sisi wenyewe kila mmoja mwingine! Inahitaji uongofu wa kweli ambao unataka  sisi pamoja kwa  kufafanua asili yetu na  jumuiya yenye uzoefu wa kupoteza. Lakini ni  kuanzia na utambuzi huo inawezekana kuhusisha dhamiri na mabadiliko ambayo yanatufanya tuwe thabiti katika udugu wa ulimwengu, amesisitiza Askofu Mkuu.

22 July 2020, 14:04