Tafuta

Vatican News
Kikundi cha wakimbizi wa Bosina kutoka  Srebrenica, wakitembea karibu na kijji cha Potocari Kikundi cha wakimbizi wa Bosina kutoka Srebrenica, wakitembea karibu na kijji cha Potocari 

Ask.Mkuu Jurkovič:Suluhisho la kweli la kulinda maisha na hadhi ya binadamu linahitajika!

Jitihada za Vatican katika kushiriki na kila mdau anayehusika katika mazungumzo ya kujenga na ambayo yanalenga kupendekeza suluhisho kamili kwa uhamiaji wa wimbi la watu na harakati za wakimbizi.Ni dharura ya matumaini iliyoelezwa na Papa Francisko katika Ujumbe wa Siku ya Wahamiaji na Wakimbizi Duniani 2018.Haya yamesema na Askofu Mkuu na Ivan Jurkovič, Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika UN huko Geneva,Uswiss.

Na Sr. Angela Rwezaula;– VATICAN.

Kuhifadhi maisha na hadhi ya kibinadamu ya wakimbizi, kupunguza mateso yao na kuhamasisha maendeleo yao ya kweli na ya msingi ndiyo jitihada za Vatican zilizodhibitishwa na Askofu Mkuu Ivan Jurkovič, Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika Makao ya Umoja wa Mataifa  na mashirika mengine ya kimataifa huko  Geneva, Uswiss. Jumanne tarehe 7 Julai 2020 katika hotuba yake  kwenye Kamati ya Kudumu ya 78, kuhusu  mpango wa Kamati kuu ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Wakimbizi na ambapo amezungumizia  mada ya “michakato ya makazi na njia nyongeza”. Awali ya yoteAskofu Mkuu Jurkovič amesisitiza jitihada za Vatican za kufanya kazi na kila mdau anayehusika katika mazungumzo ya kujenga na ambayo yanalenga kupendekeza suluhisho kamili kwa uhamiaji wa watu wengi na harakati za wakimbizi. Kwa maana hiyo  amekumbusha kuwa ni dharura ya matumaini iliyoelezwa na Papa Francisko  katika Ujumbe wa Siku ya Wahamiaji na Wakimbizi Duniani 2018, au kwamba idadi kubwa ya Nchi zifungue mikondo ya kibinadamu, wakati akisisitiza hitaji la kutafuta mifumo inayoonekana ya kushiriki usawa wa kubeba mzigo huo na majukumu.

Nchi zinazokarimu wakimbizi zishirikishwe katika ugawaji sawa  

Mwakilishi wa  kudumu Aidha  amebainisha kuwa  Nchi zinazokaribisha wakimbizi pia zinashirikishwe  katika kugawana faida. Hii ni kwamba kiukweli, wakimbizi wengi wana ujuzi ambao lazima utambuliwe vizuri na kuthaminiwa na juhudi ya kuamua ili kukuza ujumuishaji wao wa kijamii na kitaalam ambao unapaswa kutiwa moyo na kumhakikishia kila mtu uwezekano wa ajira, elimu ya lugha na uraia hai.  Hata hivyo  katika hotuba yake ameonesha shukrani kwa  hatua za dharura zilizochukuliwa katika kuwahamisha wakimbizi kutoka Libya, ambao walikuwa katika hatari kubwa, kuelekea Niger na Rwanda. “Tunashukuru kuona kwamba  karibu watu 1,200 ya  wakimbizi hawa wamehifadhiwa tena kwa njia ya dharura.” amesema Jurkovič.

Suluhisho la kudumu la wakimbizi

Utambuzi na pongezi tena amezionesha kwa hatua zilizochukuliwa na Kamati Kuu na serikali nyingi za mwenyeji kutoa suluhisho la kudumu kwa wakimbizi, pia kupitia mipango ya makazi katika nchi za tatu na utoaji wa njia zingine zinazosaidia, hasa kwa wakimbizi walio katika hali ya hatari na ambao hawawezi kurudi salama katika nchi zao za asili au kuunganishwa katika maeneo ya hifadhi. Juhudi hizi za kitaifa, amesema mwakilishi wa Kudumu, mara nyingi huungwa mkono na mashirika ya kidini na mashirika mengine ya asasi za kijamii ili kuhakikisha ujumuishaji mzuri na ujumuishaji wa ndani ya jamuiya mahalia. Licha ya hayo yote lakini ameonesha malalamiko kwa idadi kubwa ya wakimbizi na familia ambao hukaa bila kujua kuhusu maisha yao ya baadaye na wanalazimishwa, bora kuishi bila kukosa kukidhi mahitaji yao ya kila siku au, mbaya zaidi, walioko kwenye vituo vya kuwashikilia kama wafungwa , ambapo wananyimwa fursa ya kupata elimu, huduma za afya na fursa nzuri za kazi, na wana hatari ya kukumbwa na uhalifu wa biashara ya wanadamu na utumwa wa kisasa. Kwa njia hiyo wito wa Askofu Mkuu Jurkovič ni kwamba inahitaji kushirikiana katika jukumu la kulinda maisha na hadhi ya  binadamu kwa wakimbizi.

09 July 2020, 13:13