Tafuta

2018-04-11 Baraka ya Papa kwa kiumbe katika umbu la mama 2018-04-11 Baraka ya Papa kwa kiumbe katika umbu la mama 

Papa Francisko:Tukumbuke mwanamke analinda maisha!

Tukumbuke kuwa mwanamke anasimamia na kulinda maisha,kuwa na muungano na kila kitu na akitunza kila kitu.Kadiri tunavyoheshimu mwili wa mwanamke,ndivyo tunatambua kiwango chetu cha ubinadamu.Ndivyo ulivyoandikwa ujumbe wa Papa Francisko katika mitandao ya kijamii katika fursa ya Siku ya Kutokomeza Ukatili wa kijinsia katika sehemu za migogoro.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Yalikuwa maneno ya nguvu yanayogusa sana ya Papa Francsiko ambayo aliandika katika Tweet kwenye fursa ya “Siku ya Kimataifa ya Kutokomeza Ukatili wa kijinsia katika sehemu zenye migogoro” hivi karibuni. Papa anaandika katika mtandao wa pontifex: “Tukumbuke kuwa mwanamke anasimamia na kulinda maisha, kuwa na muungano na kila kitu na akitunza kila kitu. Kadiri tunavyoheshimu mwili wa mwanamke, ndivyo tunatambua kiwango chetu cha ubinadamu”.  Mawazo ya Papa yanatoa maana ya kina katika fursa ya siku hii  iliyoundwa kunako tarehe 19 Juni 1995 na Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa, mbele ya hatari hizi zisizo za kibinadamu ambazo hadi leo hii zinaona mamia elfu ya waathirika wa kijinsia  hasa katika maeneo mengi yenye kutumia silaha na migogoro.

Haki ya jinai ya kimataifa inaorodhesha aina hii ya uhalifu, kwamba siyo tu katika ubakaji, lakini pia kuna makosa mengine mengi  ya kutumia maneno ya kijinsia, utumwa wa kijinsia, ukahaba wa kulazimishwa na aina nyingine yoyote ya unyanyasaji wa kijinsia kwenye maeneo mengi yenye mizozo. Hii inachukuliwa kuwa ni sawa na mauaji ya kimbari. Lakini nyuma ya tabia hii chafu kuna nia kubwa ya  kukomesha  ugumu zaidi wa adui huyo, kwani kama mwanamke ndiye anayetoa uhai na anahakikishia urithishaji  asili wa jumuiya. Na kwa mujibu wa   maoni ya Sister  Eugenia Bonetti, mmisionari wa Consolata na rais wa Chama cha “Hakuna zaidi Watumwa”, cha Mashirika ya Kitawa,  amebainisha kwamba wanawake siyo waathiriwa peke yake katika maeneo ya  vita, bali pia hata katika jamii zetu. “Tunaona kila siku, katika barabara zetu, mitaa yetu, katika familia zetu, na  hata mahali pa kazi”amethibitisha.

Sister Eugenia Bonetti katika mahojiano pia amebainisha kuwa kwa nguvu ya mwanamke alichaguliwa na Bwana ili kujifanya mtu na atupatie zawadi ya Ukombozi. Uwezo wake wa kike wa kujitoa kwa wengine ni mithali. Aidha Sister huyo, amesema mmisionari ni mama na kwa sababu hii, ni kiongozi wa upendo kwa watoto wake wakati wa shida na hatari yoyote. Kumlinda mwanamke kutokana na vurugu yoyote ile, kwa njia hii  inamaanisha kujitetea sisi binafsi na pia muumbaji mwenyewe. Sr. Bonetti anakumbuka sana wanawake wengi wa dini  waliouawa na kubakwa wakati wa migogoro, walipigwa, kama wanawake na kama mashuhuda wa imani. Na hatimaye mtawa huyo anashukuru Papa Francisko kuwa mshikiriki wa kusimamia na kutetea wanawake.

26 June 2020, 13:38