Tafuta

Vatican News
Maaskofu Wasaidizi Jimbo kuu la Kinshasa, DRC: Jean Crispin Kimbeni Ki Kanda; Vincent Tshomba Shamba Kotsho na Charles Ndaka Salabisala Maaskofu Wasaidizi Jimbo kuu la Kinshasa, DRC: Jean Crispin Kimbeni Ki Kanda; Vincent Tshomba Shamba Kotsho na Charles Ndaka Salabisala 

Papa Francisko ateuwa Maaskofu Wasaidizi Watatu: Kinshasa, DRC.

Maaskofu wasaidizi wa Jimbo kuu la Kinshasa:Jean-Crispin alizaliwa tarehe 22 Oktoba 1969 na tarehe 30 Mei 1999 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Askofu mteule Vincent Tshomba S. Kotsho alizaliwa tarehe 22 Januari 1963. Tarehe 1 Agosti 1990 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Vincent Kotsho alizaliwa tarehe 22 Januari 1963. Tarehe 1 Agosti 1990 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amewateuwa wafuatao kuwa ni Maaskofu wasaidizi wa Jimbo kuu la Kinshasa, nchini DRC: Monsinyo Jean-Crispin Kimbeni Ki Kanda, Mheshimiwa Padre Vincent Tshomba Shamba Kotsho na Padre Charles Ndaka Salabisala. Itakumbukwa kwamba, Askofu mteule Jean-Crispin Kimbeni Ki Kanda, kabla ya uteuzi huu, alikuwa ni Afisa mwandamizi, Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa watu na msimamizi wa Parokia ya “Santa Maria Assunta in Cielo”, Jimbo Katoliki la Civilta Castellana, Italia. Alizaliwa tarehe 22 Oktoba 1969. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, kunako tarehe 30 Mei 1999 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Tangu wakati huo alitumwa na Jimbo kuu la Kinshasa, kujiendeleza zaidi katika masomo, kuanzia mwaka 1999 hadi mwaka 2001 na huko akajipatia Shahada ya uzamili katika masomo ya falsafa. Kati ya Mwaka 1992-2002 alipangiwa pia kufundisha kwenye nyumba ya malezi ya kwanza ya Kardinali Malula. Kati ya Mwaka 2001 hadi mwaka 2002, aliteuliwa kuwa Katibu mkuu wa Jimbo la Kinshasa na Gambera Msaidizi wa Madhabahu ya “Notre-Dame de la Paix de Fatima". Na mwaka 2002 akateuliwa kuwa Afisa kwenye Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa Watu mjini Roma. Na mwaka 2017 akateuliwa kuwa Msimamizi wa Parokia ya “Santa Maria Assunta in Cielo”, Jimbo Katoliki la Civilta Castellana, Italia.

Askofu mteule Vincent Tshomba Shamba Kotsho alizaliwa tarehe 22 Januari 1963. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 1 Agosti 1990 akapewa Daraja takatifu ya Upadre. Tangu wakati huo, amewahi kuwa Paroko-usu, na baadaye Paroko wa Parokia za: “Saint Augustin”; “Saint André”; Mama wa Bosawa; “Saint Frédéric; Saint Marc” na Dekano; Saint Augustin na Dekano wa Saint Gabriel. Kati ya Mwaka 2014-2018 akateuliwa kuwa Paroko wa “Saint Joseph” na Dekano. Tangu mwaka 2018 hadi kuteuliwa kwake kuwa Askofu msaidizi amekuwa ni Paroko wa “Saint Albert le Grand”, Mjumbe wa Tume ya Haki na Amani pamoja na kuteuliwa kuwa Mjumbe wa Halmashauri ya Wakleri, Jimbo kuu la Kinshasa, DRC.

Askofu mteule Charles Ndaka Salabisala alizaliwa tarehe 14 Januari 1973, huko Popokabaka. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 19 Septemba 2001 akapewa Daraja takatifu ya Upadre kwa ajili ya Jimbo Katoliki la Popokabaka. Tangu wakati huo amebahatika kuwa ni Paroko-usu na mlezi katika nyumba ya malezi ya Popokabaka, Katibu mkuu wa Jimbo na wakati huo huo, akiwa ni Katibu wa Askofu mahalia. Kati ya Mwaka 2010 hadi mwaka 2017 alitumwa na Jimbo Katoliki la Popokaba kwenda nchini Hispania ili kujiendeleza zaidi na huko akajipatia shahada ya Uzamivu katika Taalimungu na Shahada ya Uzamili katika masomo ya Kisaikolojia. Akiwa nchini Hispania, amebahatika kuhudumia Parokia mbali mbali kwenye Jimbo Katoliki la Calahorra y La Calzada-Logroño. Kunako mwaka 2017 akateuliwa kuwa Gambera wa Seminari kuu ya Kikwit na Dekano wa Kitivo cha Taalimungu, Chuo Kikuu cha Kikatoliki la Grand Bandundu.

Maaskofu Wasaidizi DRC
30 June 2020, 13:44