Tafuta

Vatican News
Padre Cantalamessa mhubiri mkuu wa nyumba ya kipapa atimiza miaka 40 tangu kuchaguliwa kwake ( 23.06.1980-23.6.2020) Padre Cantalamessa mhubiri mkuu wa nyumba ya kipapa atimiza miaka 40 tangu kuchaguliwa kwake ( 23.06.1980-23.6.2020) 

Padre Cantalamessa atimiza miaka 40 kama mhubiri wa nyumba ya Kipapa!

Ni miaka 40 iliyopita ambapo tarehe 23 Juni 1980 Mtakatifu Yohane Paulo II alimteua Padre Raniero Cantalamessa(OFMcap)kuwa mhubiri mkuu katika nyumba ya Kipapa,ofisi ambayo kiutamaduni tangu mwaka 1743 ilikuwa imekabidhiwa na mmoja wa mtaalimungu wa Shirika la wahubiri wajulikanao kama wadomenikani.Tangu mwaka huo hadi sasa amehubiri katika vipindi vikuu vya Kanisa yaani katika Majilio na Kwaresima.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Ni kumbu kumbu nzuri tangu mwaka 1980 ambapo amefanya utume huo bila kuacha hadi leo katika kutoa tafakari za sala katika vipindi vikuu vya kiliturujia kama vile ya Majilio na Kwaresima kwa kwa ushiriki wa mapapa wote watatu, kuanzia Yohane Paulo II, Benedikto XVI na sasa Papa Francisko, na Sekretarieti  nzima ya Roma. Kwa maana hiyo nafasi hiyo imeweza kuthibitishwa kuanzia na Mtakatifu Yohane Paulo II kunako mwaka 2005 na Ratzinger, Papa Mstaafu Benedikto XVI  na kunako 2013 na ( Bergoglio) Papa Francisko.  Huyo ni Mfansiskani Mkapuchini Padre Raniero Cantalamessa ambaye tarehe 23 Juni 1980, Mtakatifu Yohane Paulo II alimteua kama mhubiri mkuu katika nyumba ya ofisi ambayo kiutamaduni tangu mwaka 1743 ilikuwa imekabidhiwa na mmoja wa mtaalimungu wa Shirika la wahubiri waojulikanao kama wadomenikani. Katika mahojiano na Gazeti la Baraza la Maaskofu Italia la ‘Avvenire’ Padre Cantalamessa anazungumza kuhusu mshangao mkubwa alioupata wa kuchaguliwa katika ofisi hiyo.

Utambuzi wa nafasi yake kama mhubiri wa nyumba ya kipapa

Kumbukumbu ya mhubiri wa nyumba ya Kipapa inamfanya afurahie Padre mwenye umri wa miaka 85 ambaye amepitia kipindi chote che janga la virusi akiwa mbali na vyombo vya habari kwenye nyumba ya upendo wa huruma huko Rieti katika milango ya Roma akiwa na baadhi ya watawa wa ndani ambapo anathibitisha kuwa itakuwa vigumu kusahau. Hata hivyo amekumbusha kuwa mtangulizi wake katika nafasi kama hiyo ndani ya familia ya Kipapa alikuwa ni  Padre Irario wa Milano Italia ambaye  alikaa kwa muda wa miaka 20 akihubiri kwa mapapa wanne ambao ni Roncalli, Papa Giovanni XXIII, Montini yaani  Papa Paulo VI,  Luciani yaani  Papa Paulo I  na  Wojtyla ambaye ni  Papa Yohane Paulo II. Padre Raniero amesema “mimi ninalo la kuelezea binafsi katika kudumu kwa muda wote kwenye nafasi hiyo na siyo kwamba ni mchezo tu, awe Wojtyla, Ratzinger na Bergoglio yaani mapapa watatu wa hekima walitambua kuwa nafasi hiyo ilikuwa inastahili mimi Padre Cantalamessa ambaye sisitahili kuwapo katika  Kanisa na kwa maana hiyo wameniacha katika ofisi hiyo”. Padre Cantalamesa amekuwa maarufu sana hasa kwa miaka 15 ya kuendesha kipindi katika Luninga ya Taifa Italia kiitwacho “sua immagine”, ambalo kila Jumamosi alikuwa akitafari Neno la Mungu la maandalizi ya masomo ya Jumapili.

Nilitafuta sababu za kukataa zikakosa

Hata kama tarehe  23 Juni inakumbukwa siku rasmi aliyochaguliwa  kuwa mhubiri wa Nyumba ya Kipapa , lakini katika mahohiano  amebainisha  huo haukuwa mwanzo. Kiukweli mwanzo wake mwaka 1980, alianza miezi mitatu kabla. Hii ni kwamba Mtakatifu Yohane Paulo II alimwita na kufanya mazoezi kabla ya kumkabidhi nafasi hiyo rasmi. Anakumbuka alivyopigiwa simu na Mkuu wa shirika lao la Kikapuchini wakati huo akiwa Padre Pasquale Rywalski  na kumwambia Baba Mtakatifu Yohane Paulo II amekuchagua kama mhubiri Mkuu wa Nyumba ya Kipapa. Unazo sababu za kukataa? “Nilitafuta sababu mihimu lakini sikupata hata moja zaidi kuwa na ufahamu wa mshangao na mtetemeko mkubwa. Padre Cantalamessa akijibu juu ya nini maana ya ndugu ndogo kama yeye kuhubiri kwa mapapa amesema, kiukweli nafasi kama hiyo ni kama kubadilisha. Hiyo ni kutokana na kwamba ni Papa anayehubiri kwa mhubiri na mengineyo ya Kanisa. “Wakati mwingine Mtakatifu Yohane Paulo II alipokuwa ananishukuru baada ya kuhubiri , nilimjibu kuwa mahubiri ya kweli yalikuwa ambayo Yeye alikuwa anafanya kwake na kwa Kanisa zima”, Padre Cantalamessa aidha ameongeza , Papa ambaye kila Ijumaa asubuhi saa 3.00 kamili wakati wa kipindi cha Majilio na  Kwaresima anapata muda wa kusikiliza mahubiri ya mtu rahisi, Padre  wa Kanisa!

Kumbu kumbu hai ya Mtakatifu Yohane Paulo II

Akifafanua juu ya  kumbu kumbu yake aliyo nayo ya Mtakatifu Yohane Paulo II ni ile ya kuweza kumjua kwa karibu sana kwa miaka 25 ya kuhubiri na 27 ya upapa wake ambayo amethibitisha imekuwa ni fursa kubwa ambayo hadi sasa inakuwa vigumu kusahau . Kwa mujibu wake Papa wajtyla ni mtu aliyeishi maisha yake yote kwa mpango wa Mungu na kwa ajili ya ulimwengu. Kumbu kumbu hai kabisa ni ile aliyobaki nayo wakati wa kuhitimisha tafakari ya mafungo  ya kwaresima ya mwisho wiki mbili kabla ya kifo chake. Yeye alikuwa amefuatilia mahubiri ya Padre Cantalamessa akiwa katika chumba chake. Alikuwa amekaa katika kiti chake na mateso yake lakini akiwa anasikiliza na aliweza kuzungumza kwa njia ya mtazamo wake zaidi ya maneno. Na ndiyo ilikuwa buriani yake ya mwisho amesema Padre Cantalamessa.

Kumbukizi la Kardinali Ratzinger akiwa rais wa Tume ya Kitaalimu Kimataifa

Kwa upande wa Papa mstaafu Benedikto XVI, Padre Cantalamessa amesema ameanza  kumfahamu akiwa Kardinali wakati yeye alipokuwa Rais wa Tume ya Kitaalimungu Kimataifa (cti) na yeye padre  akiwa mmoja wa wajumbe 30 kuanzia mwaka 1975 hadi 1981. Kwa upande wake daima alishangazwa na uwezo wake wa kutambua kuongoza mijadala na ujuzi wake kamili wa  lugha ya kilatino. Akiwa Kardinali Josefu Ratzinger  hakukosa kamwe katika mahubiri yake. Miaka 8 akiwa Papa Benedikto XVI, imekuwa ya maana sana kwake katika kuhamasisha ukuu wa mafundisho na taalimungu katika utamaduni wa wakati mamboleo. Aidha Padre Cantalamessa amesema katika muktadha wake wa kung'atuka kwake katika kiti cha mtume Petro  kwa mara ya kwanza katika historia ambamo ni kwa uhuru wake kwa ujumla bila ushawishi kutoka  nje umeweza kuleta mambo kadhaa chanya ya kihistoria kuhusu wakati ujao wa nafasi ya Papa wa Roma kwa kumfanya awe katika kipimo cha mtu.

Mtazamo wa uchaguzi wa jina la maskoni wa Assisi

Na mtazamo wake kuhusiana na Papa aliyeamua kuchagua jina la maskini wa Assisi na kama vile kurudi kwa uhamasishaji wa dhana hiyo, ametubitisha kuwa na ufahamu wake na Papa Francisko kunzia mbali akiwa Kardinali na Askofu Mkuu wa Buonos Aires nchini Argentina, mwanaume mwenye msimamo. Alipata fursa ya kuhubiri katika mafungo mawili ya makleri wa jimbo kuu lake miezi michache kabla ya kuchaguliwa kuwa Papa. Aliposikia kupitia televisheni jina ambalo alikuwa amechagua na kumwona tayari anachungulia  katika lango juu ya Kanisa kuu la Mtakatifu Petro na kusalimia waamini waliokusanyika  kwa salam rahisi ‘habari za jioni’ na  baaye kuomba abarikiwe na watu  alimwambia aliyekuwa karibu naye kuwa ‘ haigizi jambo lolote kwa ajili ya faida ya vyombo vya habari. Yeye ndivyo alivyo na katika mwaka hii saba ya kiti cha Mtakatifu Petro, Padre Cantalamessa anapngenza kwa  shukrani na ukomavu zaidi.

Kuhubiri katika Sinodi ya Kianglikani huko Westminster

Jambo jingine katika maisha yake ya utume wa kuhubiri licha ya Nyumba ya kipapa lakini pia hata aliweza kuhubiri katika Sinodi ya kiangliakani kwa uwepo wa Malkia Elizabeth  mwaka 2015   ambapo anakumbuka kipindi hicho kikiwa na maana sana katika utume wake wa kiekuemeni  katika kuhubiri. Mara nyingi katika miaka hii amealikwa kwenda kuzungumza na wachungaji wa makanisa mengine ya kikristo, kuanzia kwa walutheri hadi makanisa ya kipentekoste. Kuhusiana na mwaliko wa kiongozi mkuu wa kiangliakani Askofu Mkuu Justin Welby  alihubiri katika Abasia ya Westminster wakati wa  uzinduzi wa Sinodi yao. Malkia alijulishwa suala hili jipya. Na kusema kuwa “Ikiwa padre Mkatoliki amealikwa kuhubiri huko Westminster ina maana kuwa kwamba kuna jambo  ambalo limebadilika kati ya wakristo”.

Uzoefu wa upyaisho wa wakarismatiki katoliki

Ikumbukwe Padre Kantalamessa katika uzoefu wake ameshiriki mikutano mingi ya Karisimatiki ambacho kwa sasa kinaitwa “Upyaisho wa Wakaristimatiki Katoliki” (CHARIS). Kunako mwaka 1977 baada ya vizingiti vingi anasema alikubali kubaki huko Marekani na kupokea kile ambacho katika maneno ya Yesu kutoka Matendo ya mitume anasema ya kwamba “Yohana alibatiza kwa maji, bali ninyi mtabatizwa katika Roho Mtakatifu baada ya siku hizi chache” ( Mdo  1,5)  ndiyo kuitwa ubatizo katika roho Mtakatifu . Ilikuwa ni neema kubwa  zaidi katika maisha yake baada ya ubatizo, kufunga nadhiri za kidini  na kupata daraja la kikuhani, amesisitiza Padre. Neema ambayo ilipyaisha na kuimarisha zaidi neema ambazo alikuwa tayari anazo na ambazo amependelea kuwashauri wote kufanya kila mmoja katika mtindo wake na  kwa mujibu wa fursa ambayo Roho Mtakatifu anavyomjalia. Kwa kuongezea amesema Papa Francisko haachi kutoa fursa ya kutukumbusha kuwa “upyaisho wa kweli wa maisha ya kikristo na Kanisa hauwezi kuja kama si kwa njia ya roho Mtakatifu na umoja huo wa wakristo ni kazi ya Roho Mtakatifu”.

Mbingu na nchi zitapita lakini maneno yangu hayatapita kamwe

Kwa kuhitimisha mahojiano yake Padre Cantalamessa anaota ndoto ya kuona Kanisa na  kila mkristo na jamii kwamba licha ya ufundi wa kiteknoloja lakini bado tunahitaji unabii mkubwa wa kuweza kuinjilisha kwa maana “Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe” (Mt 24 35) na kwa kizazi kipya amependa kuwaachia maneno ya mtume: “Yesu Kristo ni yeye yule, jana na leo na hata milele” (Ebr 13,8.

23 June 2020, 13:14