Tafuta

Vatican News
Yesu:"Haki yenu isipozidi hiyo haki ya waandishi na Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni(Mt 5,20) Yesu:"Haki yenu isipozidi hiyo haki ya waandishi na Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni(Mt 5,20) 

Maendeleo ya mafundisho ni uaminifu katika mapya

Baadhi ya ukosaji fulani wa mafundisho ya Papa wa sasa katika muktadha wa Mtaguso Vatican II,unaishia kusahau huduma ya Mtakatifu Yohane Paulo II na Papa Benedikto XVI.

Sergio Centofanti

Ukosoaji fulani wa mafundisho ya Papa wa sasa ni kuonyesha jinsi gani hatua kwa hatua unavyozidi kwenda mbali na Mtaguso wa Vatican II. Siyo kutokana na tafsiri fulani ya vifungu kadhaa, bali  kutoka katika maandishi yenyewe ya Mitaguso. Baadhi ya usomaji ambao unasisitiza kumpinga Papa Francisko kati ya watangulizi wake, huishia kukosoa hata hadharani pia Mtakatifu Yohane Paul II na Papa Mstaafu Benedikto XVI au kwa hali yoyote kupitisha kwa kimya mantiki msingi ya huduma yake ambayo inawakikishia maendeleo dhahiri ya Mtaguso wa mwisho. Makamu wa mhariri mkuu wa baraza la mwasiliano vatina

Unabii wa mjadiliano

Mfano wa kile ambacho kimeelezwa, ni kwamba  hivi karibuni ilikuwa maadhimisho ya miaka 25  tangu kutangazwa kwa Wosia wa “Ut Unum sint” mahali ambapo Papa Wojtyla anasema kwamba jitihada za kiekumene na mazungumzo na wasio Wakatoliki ni kipaumbele cha Kanisa. Maadhimisho hayo yameadharauliwa na wale ambao leo hii wanapendekeza tafsiri ya kupunguza Utamaduni, uliofungwa kwa “mazungumzo ya upendo”, zaidi ya yale ya mafundisho yaliyohamasishwa  na Papa Kipoland kwa utii wa shauku ya umoja wa Bwana.

Unabii  wa msamaha.

Vile vile iliyopuuzwa sawa na hiyo  ilikuwa kumbukumbu nyingine muhimu: ombi la msamaha wa jubilei iliyotamaniwa sana na Mtakatifu Yohane Paulo II kunako tarehe 12 Machi miaka ishirini iliyopita. Ni nguvu kubwa ya kinabii ya Papa  ambaye anaomba msamaha wa dhambi zilizofanywa na watoto wa Kanisa. Na wapozungumzia juu ya “watoto”  pia wamejumuishwa mapapa. Tunajua kwamba  wale wanaoomba msamaha kwa makosa hujiwekwa  katika hali ya hatari ya marekebisho. Wojtyla alichagua njia ya ukweli. Kanisa haliwezi na halipaswi kuogopa ukweli. Kardinali wa wakati huo Joseph Ratzinger, aliyekuwa Rais wa Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa  alisisitizia  “ishara mpya hiyo”  “kitendo cha kutubu hadharani cha  Kanisa juu ya  dhambi zake za zamani na leo”: “Papa katika jina la Kanisa ni ishara  kiukweli “mpya, lakini ambayo bado ipo katika mwendelezo wa kina  na historia ya Kanisa, na kujitambua kwake”.

Uchunguzi na vurugu:Ufahamu unaokua

Hadithi nyingi nyeusi zimetangazwa juu ya uchunguzi, nembo na uvumilivu mbali mbali wa Kanisa katika historia yake  ndefu, kwa kuzidisha kiasi, kudanganya, kusengenya na kupinga ili  kuifuta kutoka katika kumbukumbu kubwa na ya maamuzi ya Ukristo kwa ubinadamu. Na wanahistoria mara nyingi wamefuatilia nyuma upotovu na hadithi nyingi za ukweli. Lakini hii haizuii kufanya uchunguzi mzito wa dhamiri ili kutambua, II   upotovu uliopita” anasema Papa Yohane Paulo, na kuamsha tena dhamiri zetu mbele ya mwelekeo wa sasa”. Kwa hiyo ombi la msamaha kunako mwaka 2000 ulikuwa unahusu “mgawanyiko ambao umefanyika kati ya Wakristo, kutumia  dhuluma ambayo wengine wao walifanya katika kuhudumia ukweli, na kwa kwa sababu ya mitazamo ya utofauti na uhasama uliojitokeza kwa wafuasi wa dini nyingine. “Pamoja na maendeleo ya wakati  kunako mwaka  2004, Kanisa, linaloongozwa na Roho Mtakatifu, linagundua kwa njia ya dhamiri zaidi iliyo hai  daima kwa yale mahitaji ya kufuata kwake Injili ambayo inakataa njia za kutovumulia na za kutumia nguvu ambazo katika historia zimedharau uso wake”, amebainisha.

Kesi ya Galileo

Kesi yenye maana ilikuwa ni ile ya Galileo Galilei, mwanasayansi mkubwa wa Italia, Mkatoliki, ambaye Papa Yohane Paulo II alisema “alipata shida sana, hatuwezi kuificha kutoka kwa watu na viumbe vya Kanisa”. Papa Wojtyla alichunguza matukio “kwa kuzingatia muktadha wa kihistoria ya wakati huo” na “mawazo ya wakati huo”. Kanisa, ingawa lilianzishwa na Kristo, “bado linabaki kuundwa na  watu walio na vizingiti na wanaohusishwa na utamaduni wa nyakati. Pia wao hujifunza kutokana na uzoefu na matukio ya Galileo yaliyoruhusu ukomavu zaidi na uelewa wa mamlaka yake”. Kwa maana hiyo kukua kwa ufahamu wa ukweli  daima hauji kwa wakati mmoja.

Mapinduzi ya Copernican

Wojtyla anakumbuka kwamba “uwasilishaji wa jua kuzunguka dunia na ambao ulikubaliwa katika utamaduni wa wakati huo, sanjari na mafundisho ya Biblia, mahali ambamo maneno kadhaa yalichukuliwa kama halisi na yakaonekana maelezo kama kitovu chake. Shida iliyojitokeza kwa wataalimungu wa wakati huo ilikuwa ile ya utangamano wa ‘heliocentrism’ yaani nadharia ya dunia kuzunguka jua na maandiko. Kwa maana hiyo sayansi mpya pamoja na njia zake na uhuru wa utafiti ambao walidhania ililazimisha wataalimungu kujiuliza maswali  juu ya vigezo vya tafsiri ya Maandiko.

Wengi hawakuweza kufanya hivyo. “Kwa kushangazwa na Galileo, aliyekuwa mwamini wa kweli alijidhihirisha katika hatua  ya mwenye ufahamu zaidi kwa wapinzani wake wa kitaalimungu ambao waliangukia katika makosa wakijaribu kutetea imani”. Mageuzi yaliyosababishwa na mfumo wa Copernican kwa maana hiyo yalileta udadisi juu ya tafsiri ya Bibiblia. Galileo ambaye si mtaalimungu, lakini mwanasayansi mkatoliki, alianzisha  kanuni ya ufafanuzi wa vitabu vitakatifu, zaidi ya ile maana halisi, lakini kulingana na dhamira na aina ya kufafanuliwa sawa kwa kila mmoja wao kwa mujibu wa  aina ya simulizi. Nafasi hiyo ilithibitishwa na Papa Pio XII kunako 30 Septemba 1943 kwa Wosia wa “Divino afflante Spiritu” yaani  wosia unaohusu kuhamasisha mafunzo ya kibiblia.

Nadharia ya mageuzi

Kuongezeka kwa ufahamu wa Kanisa kumejionesha na nadharia ya mageuzi ambayo ilionekana kupingana na kanuni ya uumbaji. Ufunguzi wa kwanza ulikuwa ule wa Papa Pio XII na Wosia wake wa “Humani generis” mwaka 1950, ambapo tarehe 12 Agosti unatimiza miaka  70. Papa Yohane Paulo II anasema “uumbaji unasimamia katika mwanga wa mageuzi kama tukio ambalo hujipanua kwa wakati, kama 'kiumbe kinachoendelea', ambamo Mungu huonekana kwa macho ya muamini  kama Muumba wa Mbingu na dunia”.

Papa Francisko anasisitiza kwamba “tunaposoma katika Kitabu cha Mwanzo historia ya Uumbaji tunakabiliwa na hatari ya kufikiria kuwa Mungu alikuwa mganga kama wafanyavyo mwanamazingaombwe kwa njia zake anaweza kufanya vitu vyote. Lakini si hivyo. Yeye aliumba viumbe na kuwaruhusu kukua na kuendelea kulingana na sheria za ndani ambazo aliwapatia kila mmoja ili kuzikuza na kwa sababu aweze kufikia utimilifu wake(...). Big-Bang ambayo leo inapendekeza katika asili ya ulimwengu, haipingani uingiliaji wa Mungu muumba, lakini ambaye anahitaji. Mageuzi katika maumbile hayapatani na wazo la Uumbaji, kwa sababu uvumbuzi unasimamia uumbaji wa viumbe vinavyoibuka.”

Maendeleo ya dhana ya uhuru

Katika Agano Jipya, japokuwa si hilo tu, kuna marejesho makubwa juu ya uhuru ambao umebadilisha historia, lakini hugunduliwa kidogo kidogo. Papa Boniface VIII na hati yake ya “Unam sanctam” mwaka  1302, alikuwa anasisitizia ukuu wa mamlaka ya kiroho juu ya mamlaka ya kidunia. Hiyo ilikuwa ni enzi nyingine. Karibu miaka 700 baadaye, Papa Yohane Paulo II, akizungumza huko Strasbourg mbele ya Bunge la Ulaya, aliona kwamba Ukristo wa enzi za kati ulikuwa bado hajatofautisha “baina ya nyanja ya imani na ile ya maisha ya raia”.  Matokeo ya maono haya ilikuwa “majaribu kimsingi ya kuwatenga kutoka katika  jamii ya kidunia wale ambao hawakukiri imani ya kweli. Bado kunako mwaka 1791, katika barua kwa maaskofu wa Ufaransa, Papa Pio  VI alilaumu Katiba iliyopitishwa na Bunge la Kitaifa ambalo “liliweka kama kanuni ya sheria ya asili kwamba mwanadamu anayeishi katika jamii lazima awe huru kabisa, hiyo ni kusema kwamba katika masuala ya dini,  haipaswi kusumbuliwa na mtu yeyote, na anaweza kufikiria kwa uhuru kama anavyopenda na kuandika na hata kuchapisha kwa vyombo vya habari chochote kinachohusiana na Dini”.

Na kunako mwaka 1832, katika Wosia wa “Mirari vos” wa Papa  Gregory XVI unaozungumzia juu ya uhuru wa dhamiri kama “kosa la sumu” na “udanganyifu”, wakati Papa Pio IX katika mwongozo wa 1864,  analaani kati ya misingi ya makosa ya wakati wetu” wa kufikiria kwamba dini Katoliki inachukuliwa kuwa ndiyo dini ya serikali tu, bila kuwacha ibada nyingine zote hasa  zile ambazo zinataka na ukweli kwamba katika nchi nyingine za kikatoliki kumeanzishwa sheria kwamba wale ambao ni halali kuwa na mazoezi kwa umma ya ibada ya mtu mwenyewe”. Mtakaguso wa Vatican II na kutangazwa kwa Wosia wa “Dignitatis humanae” juu ya uhuru wa kidini na“Nostra aetate” kuhusu  mazungumzo na dini zisizo za Kikristo, ilileta maana kuu ambayo inakumbusha Baraza la Yerusalemu la Jumuiya ya kwanza ya Wakristo ambayo inafungua Kanisa kwa ubinadamu wote. Mbele ya kukabiliana na changamoto hizo, Papa Yohane Paulo anathibitisha kwamba “mchungaji lazima awe tayari kwa kujionesha dhabiti wa ukweli”.

22 June 2020, 16:27