Tafuta

Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko ameunda Jimbo kuu la Owando, Congo na kumteuwa Askofu Victor Abagna Mossa kuwa Askofu mkuu wa kwanza wa Jimbo hili. Baba Mtakatifu Francisko ameunda Jimbo kuu la Owando, Congo na kumteuwa Askofu Victor Abagna Mossa kuwa Askofu mkuu wa kwanza wa Jimbo hili.  (ANSA)

Askofu mkuu mteule Victor Mossa: Jimbo kuu la Owando, Congo!

Baba Mtakatifu amemteua Askofu Victor Abagna Mossa kuwa Askofu mkuu wa kwanza wa Jimbo Katoliki la Owando, Jamhuri ya Watu wa Congo. Jimbo kuu la Owando tangu sasa linayajumuisha Majimbo ya Impfondo na Ouesso. Jimbo kuu la Owando lina jumla ya Parokia 22 zinazohudumiwa na Mapadre wa Jimbo 29 na Mapadre watawa 5. Lina watawa wa kiume 24 na watawa wa kike 30.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko kwa kusoma alama za nyakati na kwa kuzingatia mahitaji makubwa ya shughuli za kichungaji, ameamua kulipandisha hadhi Jimbo Katoliki la Owando na kuwa Jimbo kuu. Wakati huo huo, Baba Mtakatifu amemteua Askofu Victor Abagna Mossa kuwa Askofu mkuu wa kwanza wa Jimbo Katoliki la Owando, Jamhuri ya Watu wa Congo. Jimbo kuu la Owando tangu sasa linayajumuisha Majimbo ya Impfondo na Ouesso. Jimbo kuu la Owando lina jumla ya Parokia 22 zinazohudumiwa na Mapadre wa Jimbo 29 na Mapadre watawa 5. Lina watawa wa kiume 24 na watawa wa kike ni 30. Jimbo limebahatika kuwa na Majandokasisi 21, kadiri ya takwimu za Kanisa zilizotolewa mwaka 2020.

Askofu mkuu mteule Victor Abagna Mossa alizaliwa tarehe 18 Juni 1946 huko Makoua. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 29 Desemba 1974 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Tarehe 11 Febrruari 2011, Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI akamteuwa kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Owando na kuwekwa wakfu kama Askofu tarehe 3 Aprili 2011. Kumbe, Askofu mkuu mteule Victor Abagna Mossa amekwisha kuwaongoza, kuwatakatifuza na kuwafundisha watu wa Mungu Jimbo Katoliki la Owando kwa takribani miaka 9 kama Askofu na Miaka zaidi ya 45 kama Padre!

Jimbo Kuu la Owando, CONGO
01 June 2020, 11:06