Tafuta

Vatican News
Askofu mkuu  Vincenzo Paglia Askofu mkuu Vincenzo Paglia 

Askofu Mkuu Paglia:Inahitajika mabadiliko ya mfumo wa afya

Umefanyika mkutano kwa njia ya mtandao kuhusu Hati ya Taasisi ya Kipapa ya Maisha wa “Janga na Udugu wa Ulimwengu”.Wawakilishi wa shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Amerika ya Kusini Celam na Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya watu.Askofu Mkuu Paglia amesema chanjo itakapopatikana isiwe kwa ajili ya watu wachache waliobahatika.

Na Sr. Agela Rwezaula – Vatican

Janga na Undugu wa ulimwenguni ndiyo jina la Hati ya Taasisi ya Kipapa kwa ajili ya Maisha kuhusu dharura ya Covid-19 ambayo imekuwa  kiini cha mkutano kupitia mtandaoni, uliofanyika mchana tarehe 23 Juni 2020 kati ya wawakilishi wa Taasisi hiyo,  Baraza la Kipapa la Maendeleo fungamani ya watu na wawakilishi wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Amerika ya Kusini (Celam) (Colombia, America ya Kati, Cuba na  Mexico). Kwa mujibu wa maelezo ya mwakilishi wa shirikisho la Mabaza ya Maaskofu Amerika ya kusini (Celam) amesema “Tunavutiwa na mazungumzo juu ya shida za kiafya na faida za pamoja na hii ni hatua ya kwanza ya kuweza kuokoa maisha, kwani afya ni kama faida ya umma”.

Rais wa Taasisi ya Kipapa kwa ajili ya Maisha, Askofu Mkuu Vincenzo Paglia katika mkutano huo amejikita kufafanua zaidi juu ya hatua muhimu ambazo zimefanyika katika shughulu za taasisi ya kipapa. Awali ya yote  Taasisi hiyo  ilichapisha taarifa  ya kwanza, iliyopewa jina la Janga na Udugu ulimwenguni kunako tarehe 30 Machi 2020  na kusema kwamba katika siku zijazo itatolewa hati mpya ya pili ambayo itajikita zaidi katika mada ya afya ya umma:" ‘Humana commitas’, katika enzi ya janga: tafakari juu ya kuzaliwa maisha kwa  upya”

Kadhalika Askofu amebainisha kile ambacho kwa sasa wako wanatayarisha maandishi kuhusu wazee, ambao wamekuwa na wanaendelea kuwa waathiriwa wengi wa janga hilo. Ni maandishi ambayo yanamwalika kila mtu kutafakari na  kutusaidia kuelewa maana ya kile kinachoendelea kutokea katika ulimwengu wa  leo. “Tunagundua  jinsi gani maneno Papa Francisko aliyofafanua kuwa  “ hatuko katika enzi ya mabadiliko, bali ya mabadiliko ya enzi. Hakuna shaka kwamba  mfumo mzima wa afya lazima ufikiriwe tena kwa ngazi ya kikanda na kimataifa”.

Katika hati uliyoandikwa tarehe 30 Machi, Askofu Mkuu  Paglia amesisitiza kuhusu maamuzi mawili ya mwisho. La kwanza linahusu ufikiaji wa ulimwengu katika fursa bora ya kuzuia, utambuzi na matibabu, ambayo hayatakiwi  kutengwa  tu kwa wachache walio na bahati. Usambazaji wa chanjo, mara tu itakapopatikana katika siku zijazo, itakuwa uwanja muhimu wa majaribio. Hitimisho la pili linahusu ufafanuzi wa utafiti wa kisayansi unaowajibika. Uthubutu ni magumu na  unatazama maeneo mbali mbali, kutoka uadilifu wa utafiti wa kisayansi hadi uhuru wake kulingana na maswala yanayohusiana na faida ya kiuchumi. Katika muktadha huu, kunahitajika sana kufikiria tena kwa taasisi za kimataifa zinazohusu afya ya wajumbe wote wa familia ya kibinadamu wanaoishi katika nyumba ya pamoja  ambayo ni sayari.

Mshikamano na jibu la dhati dhidi ya mgogoro: Kwa kuhitimisha  Taasisi ya Kipapa ya Maisha imeomba kusindikiza  na tafakari kwa Kanisa la  Amerika ya Kusini ili kuhakikisha kuwa Kanisa lenyewe linaweza kutoa tumaini na mshikamano. “Mabadiliko ya mfumo wa afya yanahitajika, lakini  zaidi “juu ya maamuzi ya mabadiliko yote ya kuelekea katika ustaarabu wa upendo, mshikamano na udugu”, amesema Askofu Mkuu  Paglia

24 June 2020, 15:04