Tafuta

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Padre Bernard Marie Fansaka Biniama kutoka Jimbo Katoliki la Kenge, kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Popokabaka, DRC. Baba Mtakatifu Francisko amemteua Padre Bernard Marie Fansaka Biniama kutoka Jimbo Katoliki la Kenge, kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Popokabaka, DRC. 

Pd. Bernard M. F. Biniama, Askofu Mpya Jimbo la Popokabaka!

Askofu mteule Bernard Marie Fansaka Biniama alizaliwa 29 Juni 1959, Jimbo Katoliki la Kenge, nchini DRC. Daraja takatifu ya Upadre tarehe 21 Februari 1988 Tangu wakati huo, amewahi kufundisha Seminari ndogo ya “St. Charles Lwanga”. Baadaye alijiendeleza kwa masomo ya juu kwenye Chuo Kikuu na mwaka 1994 akajipatia Shahada ya Uzamili kwenye Masomo ya Taalimungu ya Biblia.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko ameridhia ombi la kutaka kung’atuka kutoka madarakani lililowasilishwa na Askofu Louis Nzala Kianza wa Jimbo la Popokabaka, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Congo, DRC. Wakati huo huo, Baba Mtakatifu amemteuwa Mheshimiwa Padre Bernard Marie Fansaka Biniama wa Jimbo Katoliki la Kenge, DRC, kuwa Askofu mpya wa Jimbo la Popokabaka. Kabla ya uteuzi huu, Mheshimiwa Padre Bernard Marie Fansaka Biniama alikuwa ni mlezi, Seminari kuu ya Falsafa ya Mtakatifu Augustin iliyoko huko Kalonda. Itakumbukwa kwamba, Askofu mteule Bernard Marie Fansaka Biniama alizaliwa 29 Juni 1959, Jimbo Katoliki la Kenge, nchini DRC. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 21 Februari 1988 akapewa Daraja takatifu ya Upadre kwa ajili ya Jimbo Katoliki la Kenge.

Tangu wakati huo, amewahi kufundisha Seminari ndogo ya “St. Charles Lwanga” kati ya mwaka 1981 hadi mwaka 1991. Baadaye alijiendeleza kwa masomo ya juu kwenye Chuo Kikuu “Université Catholique du Congo” na mwaka 1994 akajipatia Shahada ya Uzamili kwenye Masomo ya Taalimungu ya Biblia. Kati ya mwaka 1994 hadi mwaka 1998 akafundisha Seminari kuu ya Mtakatifu Cyprien, iliyoko huko Kikwit. Kati ya Mwaka 1998 hadi mwaka 2001 akajiendeleza zaidi kwenye Sayansi ya Maandiko Matakatifu na hatimaye kujipatia Shahada ya Uzamivu kutoka katika Chuo Kikuu cha “Catholique de Yaoundé” kilichoko nchini Cameroon. Kati ya mwaka 2003 hadi mwaka 2016 akateuliwa kuwa Paroko wa Parokia ya “Notre Dame du Rosaire” huko Bandundu-Ville. Kunako mwaka 2003 akaanzisha Kituo kijulikanacho kama “Centre des Etudes Ethnologiques et Sociologiques de Bandundu” (CEESBA), huko Bandundu-Ville. Hadi kuteuliwa kwake, alikuwa ndiye muasisi na mkurugenzi wa kituo. Mwaka 2008 akachaguliwa kuwa Katibu wa Tume ya Siasa na Jamii, Jimbo kuu la Kinsasa. DRC. Na kuanzia mwaka 2018 akateuliwa kuwa Jaalim na mlezi wa Seminari Kuu ya Falsafa St. Cyprien iliyoko mjini Kikwit.

Jimbo la Popokabaka
30 June 2020, 13:29