Tafuta

Vatican News
2019.09.30  Askofu  Rino Fisichella 2019.09.30 Askofu Rino Fisichella 

Ask.Mkuu Fisichella:Chanjo iwafikie wote maskini zaidi bila ubaguzi!

Mkutano wa kuwakilisha Ujumbe wa Papa Francisko wa Siku IV ya Maskini Duniani,kiini cha tafakari ya Askofu Mkuu Fisichella ni wito wa wakristo kuwa mstari wa mbele kwa wahitaji ambapo pia ndiyo idadi kubwa ya walioathirika kwa janga.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Katika Ujumbe wa Papa Francisko wa Siku ya Maskini Duniani, 2020, anasema “sala kwa Mungu na mshikamano kwa maskini na wanaoteseka ni mambo yasiyotengenishwa na lazima kujua wazi kwamba kila mtu anao muhuri wa sura ya Mungu”, kwa  njia hiyo Askofu Mkuu Rino Fisichella, rais wa Baraza la Kipapa la uhamasishaji wa Uinjilishaji mpya wakati wa kuwakilisha ujumbe huo kwa waandishi wa habari kupitia mtandao moja kwa moja kutokana na vizuizi vilivyowekwa vya maambukizi, anasisitiza kuwa wakristo lazima wawe mstari wa mbele kwani maneno hayo ni kiongozi. Mada ya sura ya Mungu iliyowekwa kwenye paji la uso wa maskini lina maana kubwa kwa sababu linalazimisha, usigeukie upande mwingine ikiwa unataka kuishi maisha ya dhati kama mkiristo. Kwa maana hii mfano kuwapa maskini ukarimu unapata thamani yake ya kina kwa sababu kuna ulazima wa kurudi katika maneno ya Bwana ambaye alitaka kujifananisha na wale wote ambao wanakosa mambo msingi na wanaishi katika hali ya kubaguliwa kijamii na kimaisha kwa ujumla.

Siku ya Maskini itaadhimishwa tarehe 15 Novemba 2020 kwa kuongozwa na kauli mbiu “Uwape maskini kwa ukarimu”. Kwa mujibu wa Askofu Mkuu Fisichella, amebainisha,  ujumbe huo unajikita ndani ya mgogoro ambao binadamu anaishi kwa sasa katika janga ambalo bila shaka, utaongeza kutafuta na kuomba msaada zaidi. Hii itakuwa ni zoezi la kila mmoja hasa kwa kuwafanya wale maskini wasikose tunaokutana nao, zile ishara za matendo hai ya kichungaji ya kuwasindikiza na yale  maalum ambayo Siku ya Maskini duniani inatarajia na ambayo kwa miaka mingi sasa yametimizwa. Akijibu maswali ya waandishi wa habari hasa kuhusiana na jitihada za Kanisa Askofu Mkuu Fisichella amebainisha juu ya Mfuko wa Mshikamano ulioanzishwa kwa matashi ya  Papa Francisko kwa ajili ya Jimbo la Roma uitwao “Mfuko: “Yesu Mungu Mfanyakazi, Ni ishara moja na wito ambao si kwa ajili ya jumuiya tu ya kikristo, lakini pia hata juu ya matendo yote ya watu wa kujitolea, wa Caritas, na wasio! Amebainisha Askofu Mkuu.

Kuhusu, utafiti wa kisayansi kwa ajili ya  chanjo, Askofu Mkuu anakumbuka kwamba wito wa  Kanisa ni kwa ajili ya manufaa ya pamoja kwa njia hiyo  sayansi inaitwa kutoa majibu, si kwa ajili ya masilahi ya sehemu kadhaa  au ambayo huwezesha hali halisi au maeneo fulani ya kijiografia. Katika suala hili, anakumbuka kile kilichotokea miaka iliyopita kuhusu virusi vya UKIMWI wakati katika maabara na matibabu walikuwa wamepata kinga na tiba, lani wakati huo ziliuzwa kwa bei isiyowezekana hasa katika kanda za Afrika. Sayansi lazima iweze kufikia wote la sivyo inakuwa si haki na inaweza kwenda kinyume na sura ya Mungu ambayo imewekwa katika paji la uso wa maskini. Ameisitiza Askofu Mkuu.  Aidha ametoa maoni juu ya  Ujumbe wa Papa, kuhusiana  na mikono mikarimu ambayo pia imewekwa katika nembo ya Siku, kuonyesha jinsi wale wanaotoa na wale wanaopokea wanahitajiana. Picha ya mikono iliyoinuliwa imetumiwa na Papa ambaye amekumbuka wakati wa janga kwa madaktari, wauguzi, wanajitolea, mapadre. Kwa upande mwingine, ameonesha mikono iliyewekwa mifukoni ambayo hairuhusu kuguswa na umaskini, kwa njia hiyo Askofu Mkuu Fisichella amesema kuwa mikono hiyo kimsingi inakusanya pesa, kwa kuwadhuru wengine ili kuishi maisha ya hali ya juu.

Haya ni maneno makali amebainisha Askofu Mkuu Fischella ambaye anasisitiza ni ukosefu mkubwa wa uwajibikaji wa kijamii ambao upo katika ulimwengu wa leo na matokeo ya mifuko mikubwa ya umaskini ambayo inaongezeka sana bila kuhesabu. Lakini bahati nzuri orodha hii ya mwisho ni fupi, ikishuhudia kwamba wema daima ni mkubwa zaidi kuliko uchoyo wa wachache. Kwa maana hiyo kuwa na kuwapa kwa ukarimu maskini ni mwaliko wa kupunguza mateso ya wale wanaoishi kwa usumbufu katika ishara za maisha ya kila siku. Papa Francisko haogopi kuwatambua watu hawa kama watakatifu wa kweli, wale wanaoishi katika milango ya jirani amesisitiza Askofu Mkuu Fischella na kwamba  wao kwa  unyenyekevu, bila kelele na kujionesha hutoa ushuhuda wa kweli wa upendo wa Kikristo. Uwepo mkubwa wa nyuso nyingi za masikini unahitaji Wakristo wawe mstari wa mbele kila wakati, na kuhisi haja ya kujua kwamba wanakosa kitu cha tahamni wakati mtu maskini anapojiwakilisha  mbele yao. Hatuwezi kuhisi kila ktu ni sawa  wakati wajumbe  wa familia ya binadamu wanabaki nyuma na wanakuwa vivuli.

Ujumbe ni mwaliko wa kutikisa sintofahamu na mara nyingi hisia ya kuwakasirikia maskini, ambapo kuna kubaki bila utulivu hadi Mungu atakapo weza kupatikana katika maskini. Askofu ameongeza kusema  kwamba siyo bahati mbaya ujumbe huu umewasilishwa kwenye sikukuu ya kiliturujia ya Mtakatifu Anthonio wa Padua, Mtakatifu Msimamizi wa masikini, kwa sababu kile tunachoweza kufanya  kipo chini ya neema ya Mungu inayosindikiza  maisha ya waamini, amesisitiza Askofu Mkuu.

14 June 2020, 09:30