Tafuta

Vatican News
Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro 

Papa awateua wanawake wawili mmoja wa maktaba ya kitume Vatican na AIF!

Antonella Sciarrone Alibrandi mwenye umri wa miaka 55,Profesa wa sheria ya Uchumi na kaimu mkurugenzi wa Chuo Kikuu Katoliki cha Moyo Mtakatifu huko Milano ameteuliwa na Papa Francisko kawa katiba bodi ya ushauri kuhusu Habari za kifedha(AIF)ambayo ni taasisi msingi ya Vatican katika mapambano dhidi ya rushwa.Papa pia amemteua hata kiongozi mkuu wa ofisi ya Maktaba ya Kitume Vatican Dk.Raffaella Vincenti.

VATICAN

Papa Francisko amemteua Profesa Antonella Sciarrone Alibrandi, aliyekuwa mkuu msaidizi wa Chuo Kikuu Katoliki cha Moyo Mtakatifu huko Milano (Italia), kuwa mjumbe wa bodi ya wakurugenzi ya Mamlaka ya Ushauri wa Fedha (AIF). Profesa Antonella Sciarrone Alibrandi alizaliwa huko Milano tarehe 2 Mei 1965, alihitimu shahada ya sheria kunako 1987. Yeye ni Profesa wa Sheria ya Uchumi katika Kitivo cha Sayansi ya Benki, Fedha na Bima kikatoliki. Alisajiliwa katika Chama cha mawakili wa Milano, aidha ni Rais wa Chama cha waalimu wa sheria za uchumi na mjumbe wa Umoja majaji Katoliki. Alifanya utafiti uliofadhiliwa na Wizara ya Chuo Kikuu na Utafiti na Jumuiya ya Ulaya. Kati ya mambo mengine pia alikuwa amejihusisha na utawala wa soko katika Umoja wa Ulaya (EU), biashara ya haki kama mshikamano ambao ni mfano mpya wa ushirikiano wa kimataifa, mtaalam wa nidhamu ya ulinzi wa data binafsi. Kati ya mambo mengine pia yeye ni mjumbe wa Bodi ya Taaluma ya Taasisi ya Benki ya Ulaya (Ebi) na ya Kamati ya Sayansi ya Ufundi ya chama kwa ajili ya maendeleo ya masomo ya benki na hisa. Kati ya majukumu ya wahariri, yeye ni mhusika wa wahariri wa waandishi wa gazeti la “Banca Borsa e   Titoli credito” yaani “Mifuko ya Banki na dhamana ya madeni”.

Bodi ya Mamlaka ya Ushauri wa Fedha ni taasisi yenye uwezo mkubwa wa Vatican/ na mji wa Vatican katika mapambano dhidi ya utapeli wa pesa na ufadhili wa kigaidi. Kwa maana hiyo katika uwezo huu, unajikita katika zoezi la kutoa habari ya kifedha na usimamizi wote kwa madhumuni yenye busara kwa lengo la kuzuia na kupambana na utapeli wa pesa na ufadhili wa kigaidi. Bodi hii ilianzishwa na Papa Mstaafu Benedikto XVI kunako 2010 na ambapo AIF imekuwa na ujumuishaji madhubuti wa mamlaka yake ya kitaasisi na Papa Francisko. Kwa ngazi ya Kimataifa, kunako 2013, Aif ilikubaliwa kuingia katika kikundi cha Egmont, jukwaa la ulimwengu ambalo kwa sasa linaleta pamoja vitengo vya habari za kifedha vya nchi 152 zenye kukubalika, na kwa muktadha huo ambao sheria na mazoea mazuri ya kushirikiana na kubadilishana yanashirikishwa habari kimataifa.

Uteuzi wa mkuu wa Maktaba ya kitume:Papa Francisko aidha tarehe 12 Juni amemteua mkuu wa Ofisi ya Maktaba ya Kitume Vatican Dk. Raffaella Vincenti, ambaye hadi uteuzi huo alikuwa katibu wa Taasisi hiyo.  Maktaba ya Kitume Vatican iliundwa miaka zaidi ya miatano iliyopita kwa jili ya maandiko ya Mapapa na tangu asili yake ilikuwa imefunguliwa wazi kwa wasomi na watafiti. Maktaba ya Kitume ya Vatican. inayo maandishi zaidi ya 80,000, ambayo hutengeneza msingi wake mahali ambapo katika mchakao wa muda kumekuwapo na makusanyo yaliyochapishwa zaidi ya milioni moja na nusu, kati yake kuna hata maandishi ya kwanza (Incunable) karibia kidogo 9000 na makusanyo makubwa kenye majalada yaliyo kwenye vitengo zaidi ya 100,000.

Kwa kuongezea, pamoja na hati halisi, vitu vingine vya kumbukumbu ya makumbusho kama michoro, magazeti, picha, sarafu na medali pia vimefika katika maktaba kwa karne nyingi. Kwa kurahisishia wasomi kwa miaka ya hivi karibuni wamenzisha kuviorodhesha kwenye teknojia ya kidigitali. Baada muda karantini kwa ajili ya kudhibiti maambukizi, Maktaba pamoja na Pango la hifadhi ya nyaraka za kitume vimefunguliwa tangu Mosi Juni 2020. Ili kuweza kwenda maktaba hiyo ni lazima kuomba kupitia mtandaoni, katika hararati za kuendeleza usalama wa kiafya.

12 June 2020, 15:06