Tafuta

Vatican News

Watu wa Mungu na mchungaji wao Francisko!

Maelfu ya watu wametuma ujumbe na picha kwa ajili ya kumshukuru Papa kutokana na kuwasindikiza katika miezi hii migumu ya lockdown na kuwaruhusu wote washiriki Misa ya kila siku aliyoadhimisha katika kikanisa cha Mtakatifu Marta.

Na Massimiliano Menichetti

Maelfu na maelfu ya watu wametuma ujumbe wao na picha kwa ajili ya kumshukuru Papa Francisko kwa kuwasindikiza katika kipindi hiki kigumu cha kufungiwa ndani na kuwawezesha kila siku wote kushiriki Maadhimisho ya Misa katika Kikanisa cha Mtakatifu Marta. Shukrani hizo fupi kwa ujumbe ni kama vile: “asante kwa kumleta Kristo katika kila nyumba, kwa ajili ya kutusindikiza na kutusaidia, kwaajili ya ujumbe wa matumaini, kwa ajili ya kupokea Ekaristi ya tamaa na tunasali ili kweli janga hili liweze kumalizika na kusali kwa ajili yako Papa". “Asante kwa sababu ya Misa za kila siku na ambazo tumejihisi vizuri, asante kwa maana hukutuacha peke yetu”. Kwa njia hiyo ni ujumbe mwingi uliofika kutoka kila pande za Dunia!

Hata hivyo mchakato wa Ibada za misa hizo ulianza tangu Jumatatu, tarehe 9 Machi 2020 ambapo Papa kwa kipindi hiki chote amesali kwa nia mbali mbali, hakusahau kila mantiki na hivyo alisali kwa ajili ya: wagonjwa walioambukizwa na virusi, madakatari, wauguzi, watu wa kujitolea, familia na wazee ambao walikuwa katika vituo vya mapumziko, pia kwa ajili ya wafungwa. Ni kwa siku sabini wakati virusi vinaendelea kusambaa na kulazimisha nchini nyingi kusitisha maadhimisho ya misa kwa waamini. Yote imekuwa nia ya kuepuka usambaaji zaidi wa virusi hivyo na ambapo watu wengi kwa hakika wameweza kushiriki kila siku asubuhi misa ya Papa. Papa kila siku asubuhi aliweza kutoa maneno ya matumaini na wokovu wa dhati wa Injili wakati wa kuhubiri. Na baada ya misa ilifuatia kuabudu kila siku kwa ukimya na baadaye kubariki kwa Ekaristi, akiongozwa na wimbo wa Malkia wa Mbingu kabla ya kutoka katika kikanisa.

Milioni ya watu kila siku wameweza kusali asubuhi na mapema, kwa maana muda haukuwa ni shida kutokana na kwamba kila nyumba kupitia radio, tv, internet, mitandao yote ya kijamiii imeruhusu Papa kubisha na kuingia katika  milango iliyokuwa wazi kwa kila nyumba na wao kuwaruhusu kutazama kikanisa kidogo cha Vatican! Hawa walikuwa ni watu wazima na wadogo, familia, wafanyakazi, watawa, kila watu waliweza kusikiliza neno la Mungu na kusali kwa pamoja wakizi kugundua kwa upya ile safari yao ya kiroho na ya maisha yao kwa ujumla.

Papa Francisko hakusahau yoyote na zaidi hata kutoa ushauri wa kuwasaidia hasa wale wenye matatizo akikumbuka watoto wenye njaa na wote wanaokimbia njaa; Papa Francisko ameweza kusali kwa ajili ya watawala  wa nchi ambao wanapaswa waamue mstakabali wa mataifa yao, amesali kwa ajili ya wanasayansi ili wapate suluhisho la haraka katika kipindi hiki kigumu. Alishukuru daima wale wote wanaosaidia hasa wadhaifu na wasio kuwa na mtetezi kama vile wazee na walemavu katika kipindi cha mateso na woga.

Hakika Papa Francisko alisali kwa ajili ya watawa wa kike na kiume ambao wanatoa maisha yao huku wakibaki kuwasindikiza na uchungu na majaribu watu wengi. Alisali kwa ajili ya waathirika wote wa janga la corona na familia zao. Alikumbuka kila aina ya wafanyakazi, kama vile madaktari, wafamasia na walimu, watu wanaofanya usafi, watu wanao toa hudumia ya  kuzika maiti makaburini akibainisha kuwa  wanahatarisha maisha yao. Amesali kwa ajili ya mama wajawazito ambao wanatakiwa kujifungua watoto wao katika kipindi hiki cha janga.

Alisali kwa ajili ya wale wasio kuwa na ajira, wanasanaa, wanafunzi na wale wote wanaotakiwa kufikiria baada ya janga katika kutafuta suluhisho la matatizo yanayotusubiri. Kwa hitimisho la misa zake tarehe 18 Mei, misa ilitangazwa moja kwa moja, katika Kanisa kuu la Mtakatifu Petro, kwenye Kaburi la Mtakatifu Yohane Paulo II na ndiyo ilikuwa hitimisho la misa za moja kwa moja kwa kipindi hiki ambacho ametuongozi kwa Neno la Bwana la kila siku.

20 May 2020, 16:17