Tafuta

Vergez:Matayarisho ya kufunguliwa makumbusho jijini Vatican!

Na Sr.Angela Rwezaula- Vatican

Ziara zisizo halisi kama za kidigitali zinahitaji kuimarishwa, lakini tunayo hitaji kubwa la ukweli, hitaji sana la kutafuta kwa nguvu zote. Tusisahau kwamba watu ndiyo wanaofanya Makumbusho kuwa hai na uzoefu halisi wa Jumba la Makumbusho hufanya watu wawe hai. Ubunifu hauwezi kamwe kuchukua nafasi ya ukweli. Na ili kufurahia sanaa inahitajika macho na moyo. Hayo ndiyo yamesema Askofu Fernando Vérgez Alzaga, Katibu Mkuu Tawala wa Jiji la Vatican  hivi karibuni katika mahojiano na Vatican News kwa matazamio ya kufungua kwa mara nyingine tena majumba ya makumbusho mara baada ya lokdown ya janga la covid-19. Katika mahojiano hayo amesema “Tukiwa katika kukaribia tarehe ya ufunguzi wa makumbusho nchini Italia, hata Makumbusho ya Vatican ikijiandaa kufungua milango yao tena, inaezekana kuyafikia  kwa kupitia maombi kwenye mtandao na kuvaa barakoa”.

Karibu milioni 7 ya watu waliotembela makumbusho Vatican kwa mwaka 2019 na kama ilivyo kwa makumbusho yote yaliyo lazimika kufungwa kwa umma. Je mmeonaje kazi ya siku hizi za kufungwa kwa  lazima na shughuli zinaendeleaje? Kwa kujibu Askofu Verges  amesema kuwa walifunga milango kwa umma kwa utambuzi wa ulinzi na usalama wa afya ya watu awali ya yote. Kwa mwezi mzima na nusu walimua kuendelea mbele na shughuli ambazo zinaweza kuitwa muhimu kwa kuwaita wafanyakazi karibia therathini kila siku. Hii ni asilimia ya chini sana kwa kuzingatia kuwa familia ya wafanyakazi katika makumbusho na washiriki wake  karibu ni watu elfu moja pamoja na walinzi, wanahistoria wa sanaa, wanaukarabati, wafanyakazi wa utawala na kampuni mbali mbali za huduma.  “Katika kipindi cha wiki mbili zilizopita, tumeanza shughuli nyingine polepole. Tunahitaji juu ya yote kuwapa wafanyakazi wetu wakati wa kuzoea itifaki mpya za usalama na kuthibitisha marekebisho yasiyoweza kuepukika ya kufunga ikiwa inawezekana hali isiyo ya kawaida na ngumu kama ile ambayo kwa sisi sote tumekumbwa kwa muda mrefu.”

Ni jinsi gani ya kukabiliana mgogoro wa Makumbusho na pia juu ya uchumi kwa miezi ujayo? Askofu amesema:Kwanza kabisa, kulikuwa na wasiwasi wa kuhakikisha mshahara wa wafanyakazi wote. Uangalifu huu ni ishara ya umakini wa Papa. Pili, mara moja tuliamua kupunguza gharama zote zisizo za haraka. Kama ilivyo katika familia yoyote nzuri, sasa ni wakati wa kuokoa na kuondoa mambo yasiofaa zaidi, kufanya sadaka kadhaa, huku tukingojea nyakati zilizo bora. Kama kwa siku zijazo, tunaweza kusema kwamba Makumbusho ya Vatican ni taasisi madhubuti, hata kwa mtazamo wa kiuchumi. Hii inaturuhusu sisi kutazama  mbele kwa ujasiri.

Siku hizi tumeshuhudia kuongezeka kwa hadhira sana ya dijitali, tangu tulipolazimika kukaa nyumbani Je! mmefikiria juu ya kuongeza mawasiliano katika eneo hili? Miezi hii miwili imekuwa miezi ya ukimya kwetu. Tulimwona Papa Francisko akiwa peke yake  katika Uwanja wa Mtakatifu Pietro. Kila siku tunaona vyumba na nyumba za majumba ya makumbusho yakiwa hayana  watu. Ukimya unahitaji maombi. Hii ndiyo sababu tulipendelea kukaa kando kidogo, kupunguza mawasiliano yetu kwa kiwango cha chini na kutoa ushuhuda kwa maana hii. Kwa namna nyingine, kwa wale ambao walitaka na bado wanataka, katika tovuti rasmi tunatoa safari nyingi za makumbusho, pamoja na Kikanisa cha Sisitina

Aidha amebanisha kuwa: Kwa miezi michache tumefungua rasmi hata  Instagram @Vatmuseums, mahali ambapo kila siku tunawasilisha kazi kutoka katika  ukusanyaji wa sanaa za kipapa. Hasa, katika kipindi hiki cha mwisho, pia tumefanya hivyo kwa kushirikiana na Habari za Vatican. Lakini ameongeza kusema kuwa  “hacha  niseme jambo moja: tunalo hitaji kubwa la ukweli, hitaji la kutokata tamaa. Tusisahau kwamba watu ndiyo wanaofanya Makumbusho kuwa hai na uzoefu halisi wa Jumba hilo la Makumbusho hufanya watu wawe hai. Ubora hauwezi kamwe kuchukua nafasi ya ukweli: ili kufurahia sanaa inahitaji macho na moyo, siyo skrini za kugusa tu.

14 May 2020, 14:24