Tafuta

Vatican News
Watu wengi na jamuiya ndogo zinaendelea kuwa chini ya vitisho,uhasama,vurugu,vizingiti,ukosefu wa uvumilivu na zaidi kuzidishwa na mgogoro wa afya wa sasa. Watu wengi na jamuiya ndogo zinaendelea kuwa chini ya vitisho,uhasama,vurugu,vizingiti,ukosefu wa uvumilivu na zaidi kuzidishwa na mgogoro wa afya wa sasa. 

Covid-19:Vatican imehimiza OSCE kukuza uhuru wa kidini na uvumilivu!

Monsinyo Janusz Urbańczyk,Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika Shirika la Usalama na Ushirikiano barani Ulaya(OSCE),wakati wa kutoa hotuba yake kwenye vikao vitatu huko Vienna amesitizia amebainisha jinsi gani eneo la OSCE watu wengi na jamuiya zinaendelea kuwa chini ya vitisho,uhasama,vurugu,vizingiti,ukosefu wa uvumilivu na zaidi kuzidishwa na mgogoro janga la sasa la kiafya.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Kushughulikia kila aina zote za ubaguzi ambazo watu wanaweza kuteseka katika muktadha wa sasa wa janga la virusi vya corona ndiyo wito uliotolewa na Monsinyo Janusz Urbańczyk, Mwakilishi wa Kudumu  wa Vatican katika Shirika la Usalama na Ushirikiano barani Ulaya (OSCE), wakati wa kutoa hotuba yake kati ya  tarehe 25 na 26 Mei, kwenye vikao vitatu vya kufanya kazi juu ya mada ya  kutovumilia, vilivyoandaliwa na OSCE huko Vienna. Awali ya yote Mwakilishi wa Vatican amesisitiza kwamba kila mwanadamu ana hadhi sawa, ya ndani na isiyoweza kutengwa, anatakiwa  apate haki zote msingi na muhimu za wanadamu.

Ubaguzi unawakilisha ukiukwaji wa kanuni za haki

Kwa mtazamo huo ubaguzi unawakilisha ukiukwaji wa kanuni ya haki, na kwa wasiwasi mwakilishi Urbańczyk amesitiza ni kwa namna gani katika Eneo lote la OSCE watu wengi na jamuiya zinaendelea kuwa chini ya vitisho, uhasama, vurugu, vizingiti, ukosefu wa uvumilivu na zaidi kuzidishiwa na mgogoro wa afya wa sasa. Kwa kuongezea, uhalifu wa chuki unaweza kuathiri jamuiya ndogo na ambao mara nyingi wanastahili umakini sawa sawa na wengine wote.

Uhusiano kati ya uvumilivu na haki za binadamu

Mwakilishi wa Kudumu aidha amesisitizia juu ya uhusiano mkubwa kati ya uvumilivu na haki za binadamu. Heshima kwa kanuni na jitihada kwa wale ambao hawawezi kuongea na hawawezi kutengwa kwa ukiukwaji wowote ule. Kwa kuongezea, katika muktadha wa dharura ya kiafya uliosababishwa na Covid-19, Mwakilishi wa  Kudumu amewaalika wazingatie kwa namna ya pekee  mitandao ya kijamii kwa kuwa muda mwingi unaotumika umeongezeka wa kukaa katika mtandao.

Umakini katika nafasi za kidijitali 

Nafasi ya kidijitali inaweza kugeuka kuwa jukwaa la kuhamahama au kuchochea dhidi ya vikundi vya kitamaduni, kitaifa na kidini, au kwa kuhamasisha matibabu yasiyostahili na uwakilishi wa uchochezi wa alama za kidini. Na hayo yote inaweza kusababisha vurugu. Kwa  maana hiyo, kila mtu anapaswa kutiwa moyo ili kutumia uhuru wao wa kujieleza kwa uwajibikaji  hasa kwa kuweka kandoni  chuki, ubaguzi na uwongo. Askofu Mkuu Urbańczyk ametoa ushauri wa kufanyakazi kwa ajili ya jamii yenye uvumilivu na utofauti wa kidini, utamaduni na utaifa ambao unatambua thamani ya tamaduni na ulazima wa kukamilishana kiutamaduni.

Hadhi ya kila maisha na msingi wa kujieleza

Misingi miwili ya kuzingatia katika muktadha huo, ni hadhi ya kila maisha ya mtu ambayo yanategemea na asili yake au kukiri kwake na msingi wa umoja wa kila mwanadamu. Hii inamaanisha, uhakikisho  kwamba jamii ya kidemokrasia ya kweli lazima ihakikishe ushiriki wa mambo madogo ya kitaifa kama vile ya  siasa, uchumi, kijamii, kitamaduni na maisha ya kidini. Lakini kwa bahati mbaya amesema mwakilishi kutokana na janga la sasa, watu wengine wachache hawakuweza kuona haki zao msingi kama vile ufikiaji wa mifumo ya kiafya  au habari. Hata hivyo amekumbusha Mwakilish kuwa ni jinsi gani tarehe 12 Mei 2020 alikuwa amekabiliana na mada kama hii kuhusu uhuru msingi wa mtu wakati wa kipindi cha virusi vya corona. Kwa mujibu wake kuhusiana na uhuru wa dini amebainisha kuwa hiyo ni hali  ambayo haina mjadala hata katika kipindi cha janga, kwani ni kitambulisho cha haki za wanadamu.

28 May 2020, 16:00