Tafuta

2020.05.06 Pakua  app ya radio vaticana/vatican news. 2020.05.06 Pakua app ya radio vaticana/vatican news. 

Vatican:App "RADIO VATICANA"

Kwa sasa unaweza kupakua kupitia google-play au App-store vipindi vya Radio Vatican kwa alama inayoonekana moja kwa moja 'App RADIO VATICANA' ili usikilize moja kwa moja habari za Baba Mtakatifu, Vatican, Kanisa na ulimwengu.

Katika maendeleo makubwa ya sayansi na teknolojia ya mawasiliano ambayo inazidi kukua kwa kasi zake kila kuchao na kufikisha ujumbe wa moja kwa moja na ambapo hakuna kama nyakati hizi ambazo zimewezesha kuona taarifa zinafikia kila kona, shukrani kwa ubunifu wa teknolojia hizo watu wengi wameneemeka kwa mawasiliano na tarifa zilizo za kweli!

Kwa kurahisisha nyenzo muhimu ya mawasiliano  na katika harakati ya kukuza kiwango cha ufikiwaji wa habari, Baraza la Kipapa la  Mawasiliano Vatican limewezesha kuunda ‘APP’ kupitia  goole -play au App-store ambayo unaweza kupakua ikiwa na alama inayonekana mara moja ukiandika 'App "RADIO VATICANA” ili uweze kupata habari zake moja kwa moja na vipindi vyote.

Aidha unaweza kusoma habari ZA RADIO VATICAN moja kwa moja KWA KUBONYEZA LINK HII: http://www.radiovaticana.va/landingpage/

Unakaribisha kuendelea kupata habari za moja kwa moja za BABA MTAKATIFU, ZA VATICAN, ZA KANISA NA ULIMWENGU KWA UJUMLA KWA LUGHA ZOTE ZILIZOMO KATIKA TOVUTI YA RADIO VATICAN/ VATICAN NEWS na ambazo zinasikika katika ulimwengu mzima.

Ni mambo mengi ya kiroho na kijamii yatakusaidia katika safari yetu ya maisha. Matumaini yatakuongoza katika safari hii ikiwa na mtangulizi wake MKUU katika mtumbwi huo ambaye ni YESU  Kristo aliyeshinda mauti na YEYE NI MZIMA ALELUYA!

 

06 May 2020, 15:56