Tafuta

Usafi wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro,Mtakatifu Yohane na Mtakatifu Paulo!

Baada ya miezi zaidi ya miwili sasa,inawezekana kurudi katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro kwa usalama kituo cha ukristo.,Kanisa Kuu la Mtakatifu Yohane,Mtakatifu Paulo na mengine.Hata hivyo ni lazima kufuata masharti ya usalama.Hii ni mara baada ya kufanyiwa usafi na kunyunyizia dawa makanisa makuu haya ya kipapa tarehe 15-16 Mei 2020,tayari kwa ibada kwa waamini.

Na Sr. Angela Rwezaula-Vatican

Kila kitu kiko tayari kwa ajili ya waamini ambao wanaweza kurudi na kusali kuanzia Jumatatu 18 Mei 2020 katika kaburi la Mtume Petro, kwa kufuata kanuni za sheria zinazoendelea hadi sasa ili kuzuia maambukizi ya virusi vya Corona. Na hii ni kwamba Ijumaa tarehe 15 Mei 2020 wamesafisha  na kukunyunyizia dawa ya kuua vijidudu Kanisa kuu la Mtakatifu Petro vile vila hata Kanisa Kuu la Mtakatifu Yohane Laterano kupitia kila sehemu zilizo muhimu kwa  muktadha wa virusi. Kwa upande wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro na hasa watakao kuwa wanaingia humo, hawatasahu kamwe ule uwanja na Kanisa bila kuwa na watu.

Ni sehemu ambazo zilikuwa zinatamaniwa na matumaini katika Kristo ili kuweza kuzikumbatia kwa mara nyngine tena, kwa kutazama ule msalaba Mtakatifu Marceli na Picha ya Maria Afya wa watu wa Roma na dunia nzima vilivyoonekana wakati wa sala ya Papa Francisko ambayo haitasahaulika kamwe na maadhimisho ya Pasaka. Picha zile na sala ziliwasindikiza wengi na mara nyingi katika kipindi cha janga ikiwa ni pamoja na maadhimisho ya Papa Francisko kila siku. 

Kwa mana nyingine tena milango itafunguliwa na itakuwa ni kama kurudia kupumua. Kwa mujibu wa Profesa Andrea Arcangeli Kaimu Mkurugenzi wa Afya na Usafi wa Utawala wa mji wa Vatican akihojiwa na mwandishi wa habari wa Vatican News  amesema usafi ulifanyika vema katika kuthibtisha ki ukweli kwamba jambo la (kusanitisha) kunyunyizia dawa ni utaratibu rahisi lakini ambao unajumuisha michato ya hatua.

Kwanza kabisa, unahitaji usafi kama ufanyika usafi wa kawaida na sabuni iliyochanganywa na maji. Baadaye ni lazima utumie vitu kama dawa ambavyo vimetengenezwa kwa ajili hiyo kama walivyofanya na kunyunyizia kwenye nyuso na ambazo zina lengo la kupunguza kwa kiasi kikubwa mzigo wa bakteria au virusi na katika nyuso ambazo zinaweza kubaki bakteria hizo. Ni wazi kwamba huwezi kukomesha kabisa, hiyo labda inawezekana kama ambavyo hufanyika katika chumba cha upasuaji. Lakini ni muhimu kupunguza mzigo wa vijidudu vyovyote. Vile vile amesema hawawezi kutumia madawa makali sana kutokana na kwamba kuna picha za sanaa Katika Makanisa Makuu kwa  sababu zinaweza kuharibu nyuso za thamani, yaani kazi za sanaa ambazo zimo ndani ni  utajiri mkubwa sana wa ndani ya kanisa na hivyo walikuwa makini katika usafi.

Maeneo yaliyosafishwa na kunyunyiziwa dawa ni yale ambayo yanapitiwa sana na watu kwa maana hiyo sakafu na altareni katika sakresita, ngazi, kwa namna moja sehemu zote zote zinazopitiwa kwa miguu. Hata hivyo pia ameeleza kuwa matatizo makubwa hayapo wakati wa kusanifisha kwa maana wamezoea mara nyingi kufanya kazi hiyo. Labda kwa sasa ni wazi kwamba wanatumia aina fulani ya madawa mchanganyiko na klorini, lazima wawe na umakini fulani juu ya jinsi zinavyosambazwa, lakini hawana shida fulani.

Ikumbukwe pia katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Paulo Nje ya Ukuta Roma tarehe 16 Mei 2020 limefanyiwa usafi na kunyunyiziwa dawa ya kuua vijidudu kama mchakato ambao tayari umefanyika  katika makanisa makuu mawili Ijumaa 15 Mei.

16 May 2020, 15:00