Tafuta

Vatican News
TAHARIRI  YA ANDREA TORNIELLI TAHARIRI YA ANDREA TORNIELLI  Tahariri

Tarehe 18 Mei misa ya miaka 100 ya Wojtyla na mwisho wa misa za moja kwa moja

Jumatatu asubuhi tarehe 18 Mei Papa Francisko ataadhimisha misa katika kaburi la Mtakatifu Yohane Paulo II,katika fursa ya kilele cha miaka 100 ya kuzaliwa kwa Mtakatifu huyo.Ndiyo pia itakuwa hitimisho la misa za kutangazwa moja kwa moja kila siku katika kikanisa cha makao ya kipapa.

Dk.Andrea Tornielli, Mhariri Mkuu wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano katika tahariri yake kuhusu fursa ya maadhimisho ya Papa Francisko katika Kaburi la Mtakatifu Yohane Paulo II katika muktadha wa kukumbuka ya miaka 100 ya kuzaliwa kwake mtakatifu huyo, anabainisha kuwa itakuwa ndiyo misa ya  kuhitimisha liturujia za kila siku za moja kwa moja katika kikanisa cha makao ya Kipapa. Kwa mujibu wake anasema, hizi ni misa ambazo zimefanyika kila asubuhi saa moja kwa miezi miwili sasa na ambazo zimesindikiza milioni ya watu katika  ulimwengu mzima.

Katika fursa ya kuanza kwa upya misa wa waamini wa Italia, Papa Francisko ameamua kwa dhati kusitisha misa za kutangazwa moja kwa moja, na katika fursa ya siku hiyo itakuwa maalum kwa sababu, Papa ataadhimisha misa katika kaburi la  Mtakatifu huyo, mtangulizi wake aliyezaliwa kunako mwaka 1920 na kuchaguliwa kuwa Askofu wa Roma kunako mwaka 1978 na kifo chake maka 2005 na kutangazwa mtakatifu 2014.

Maadhimisho ya misa za kila asubuhi za moja  kwa moja kupitia radio na vyombo vya habari katika kikanisa cha Mtakatifu Marta na uamuzi wa kuadhimisha kila siku katika kipindi hiki kigumu cha kukaa ndani, zimekuwa zawadi isiyo tarajiwa na nzuri sana. Watu wengi hata waliokuwa mbali na Kanisa wamehisi kusindikizwa na ushauri wa Papa, tangu kusimamisha mguu mwanzoni mwa siku yeye alikuwa akibisha milango ya nyumba zao.

 Wengi wamejifunza umuhimu na kutiwa moyo katika kukutana kila siku na Injili. Haikuwahi kutokea namna hii kwa walio wengi kufuatilia liturujia za kila siku katika televisheni, pendekezo bila maoni na kufanya dakika chache za kuabudu kwa kimya Ekaristi Takatifu. Uzuri na urahisi wa mahubiri bila kusoma yaliyotamkwa na Papa yametuwezesa kuingia katika kurasa za Injili kama vile tulikuwapo wakati matukio yale yanatendeka. Wakati wa dharura ambayo imetulazimisha kubaki tumefungiwa katika kuta za nyumba, umeonekana wazi uthibitisho wa huduma yake ya kila siku kwa mara nyingine na thabiti katika kipindi cha ukosefu wa uhakika, wa mateso, wa uchungu na maswali mengi ya kujiuliza ya wakati ujao.

Mahubiri katika Nyumba ya Mtakatifu Marta, yanawakilisha muktadha wa maana sana katika huduma ya Papa Francisko kama Askofu wa Roma. Walio wengi walikuwa wamezoea kufuatilia kwa njia ya ufupisho uliokuwa unatolewa na vyombo vya habari Vatican, na  hata katika vitabu kutoka kwenye Maduka ya Vatican, na ambayo kila waka hutoa uwezekano wa kushirikia, japokuwa kwa umbali, maadhimisho ya kila siku, wakitazama Papa wakati anahubiri na kutafakari maandiko matakatifu bila kusoma.

Milioni ya watu tofauti wameweza kila siku kuingia katika mawasiliano ya misa hizi. Ni wengi ambao wameandika kwa kushukuru. Sasa ambapo maadhimisho yanafunguliwa kwa mara nyingine tena kwa watu wa wa Mungu katika makanisa ya Italia, kuna hatua  mpya ya mwanzo. Kwa walio wengi kwa hakika watakuwa na kumbukumbu hiyo ya misa za kila siku. Lakini kama alivyosisitiza Papa Francisko mwenyewe, kwamba kuna haja ya kurudia katika jumuiya ya kifamilia na Bwana katika sakramenti, kwa kushiriki kweli binafsi liturujia. Bila kusahau mwaliko mwingine wa Papa  wa kuzoea kila siku kungua sura ya Injili, kukutana kila siku kama ilivyokuwa misa kupitia televisheni ya Nyumba ya Mtakatifu Marta ambayo ilikuwa imetuzoeza sasa.

Unaweza kupakua kupita  hapa: https://www.vaticannews.va/content/dam/lev/forti-nella-tribolazione/pdf/it/ITALIANO_12-maggio-20.pdf

Kitabu  kiitwacho “Forti nella Tribolazione”  yaani “nguvu katika mateso” kutoka Duka la Vitabu Vatican (LEV ), kinachokusanya mahubiri yote ya Papa Francisko wakati wa misa zake kwenye Kikanisa cha Mtakatifu Marta, Vatican katika  kipindi cha janga.

13 May 2020, 14:14